Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kifungo cha Watoto Wahamiaji cha Trump Chadhihirisha Umbile la Kinyama Lisilokubalika la Nidhamu ya Kitaifa ya Kidemokrasia ya Amerika

Chini ya sera ovu ya uhamiaji ya ‘kutokuwa na hata chembe ya uvumilivu’ ya Raisi wa Amerika, takriban watoto 2000, wengine wao wakiwa na umri mdogo wa miaka 4 au 5, ni miongoni mwa wale walioorodheshwa kama ‘wahamiaji haramu’, wametenganishwa kwa nguvu kutoka kwa wazazi wao katika mpaka wa Amerika na Mexico katika kipindi cha wiki sita pekee. Wametiwa ndani ya vibanda vya seng’enge katika vituo vya vizuizi, ambavyo hali zake zimesifiwa kuwa ‘mithili ya gereza’. Mojawapo ya vituo hivi vya wahamiaji katika jimbo la Texas kimepewa lakabu ya La Perrera, “kibanda cha mbwa”, ambamo watoto wanalala chini sakafuni juu ya magodoro membamba na makaratasi ndio blanketi zao. Kanda ya sauti ya watoto walioathirika kimawazo na kulia imepatikana, wakililia wazazi wao. Idara zimetangaza mipango ya kujenga mahema yatakayobeba mamia zaidi ya watoto katika jangwa la Texas ambako viwango vya joto kawaida hufikia nyuzi 40.     

Soma zaidi...

Risasi Zimechukua Maisha ya Watu … Na Serikali Zinacheza Densi Juu ya Majeraha!

Kwa mujibu wa mashirika ya habari; mtoto wa miezi 8 Laila Al-Ghandour alifariki mnamo Jumanne asubuhi eneo la Mashariki mwa Gaza baada ya kuvuta gesi. Tukio hili linaongeza idadi ya mashuhadaa wa “Msafara wa Mkubwa wa Maregeo” na kufikia idadi ya 61, wakiwemo watoto 7 na majeruhi 2,800, wengi wao wakiwa ni kutokana na risasi na wengine wakiwa ni kutokana na vipande vya mabomu na gesi ya sumu wakati wa uzimaji msafara na majeshi ya umbile la Kiyahudi iliyoanza maeneo tofauti Mashariki mwa ukanda wa Gaza katika kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba, na ambayo ilipinga na kukataa kuhamishwa kwa ubalozi wa Amerika jijini Al-Quds (Jerusalem).

Soma zaidi...

Waislamu na Wanadamu kwa Jumla ni Wakati wa Kukumbuka Siku Hii

Mwishoni mwa mwezi huu mtukufu wa Rajab, mataifa ya kirasilimali na ya kikoloni baada ya kupangiliwa vizuri kwa njama na mikakati ya muda mrefu yalifaulu kuivunja Dola ya mwisho ya Kiislamu ya Khilafah Uthmaniya ambayo makao yake makuu yalikuwa nchini Uturuki, tukio ambalo lilifikia kileleni mwake mwishoni mwa Rajab 1342 H / Machi 1924 M.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu