Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  3 Rabi' II 1444 Na: 02 / 1444 H
M.  Ijumaa, 28 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miitiko ya Kisiasa kwa Wadhifa wa Kiislamu wa Hizb ut Tahrir Inathibitisha Kufilisika kwa Demokrasia

(Imetafsiriwa)

Mnamo Oktoba 7, 2022, Hizb ut Tahrir / Denmark ilichapisha kipeperushi chini ya kichwa "Waislamu Wapendwa - Demokrasia iliyokumbwa na mgogoro ni dhidi ya Uislamu wenu. Msishiriki katika tambiko lisilo na maana la uchaguzi!" Mbali na kuashiria mgongano wa wazi kati ya Uislamu na demokrasia, kipeperushi hicho, ambacho kimesambazwa katika miji kadhaa, kina ukosoaji kadhaa wa demokrasia ya kisekula, ikiwemo:

- Demokrasia kivitendo ni dhulma ya walio wengi dhidi ya wakaazi Waislamu barani Ulaya, ambapo katika muktadha wa Denmark leo ni wazi kwamba Waislamu watakuwa chini ya shinikizo na unyanyasaji zaidi wa kisiasa, bila kujali matokeo ya uchaguzi mkuu ujao.

- Demokrasia inakabiliwa na mgogoro wa kimataifa wa kutoaminiana. Nchini Denmark pia, raia wengi zaidi wanaamka na ukweli kwamba demokrasia ni mwanga mkali ambao lazima ufinike nguvu msingi ya kipote cha mabepari. Hadithi ya uamuzi wa kweli shirika kupitia kupiga kura kila baada ya miaka minne inakufa.

- Sehemu ya hadithi hii ni kwamba chaguo ni kati ya kupiga kura au kukwama kwenye kochi na kujiweka nje ya ushawishi. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir daima imekuwa changamfu kisiasa katika sehemu zote za dunia na jamii ambako tunafanya kazi, na tunawalingania Waislamu kufanya vivyo hivyo: Kushiriki kichangamfu katika jamii - kisiasa, kitamaduni, kielimu na kitaaluma - kwa masharti ya Kiislamu.

Katika makala kadhaa ya magazeti na pia makala ya redio na televisheni, wanasiasa kutoka mirengo na vyama mbalimbali wameitikia ujumbe wetu. Miitiko ya kuchafua inayotarajiwa kutoka kwa wasemaji wa vyama mbalimbali imetoa ofa za watu wengi za tikiti moja moja kwenda nchi za mbali, matakwa ya "kutuweka mbali", madai potovu kuhusu utukufu wa demokrasia na marudio rudio ya hadithi zilizo hapo juu. Kwa maana nyengine, hakuna fikra hata moja iliyo onyeshwa.

Kama ilivyo kawaida yao, wanasiasa wasaka tonge wanashindwa kabisa kukabiliana na ukosoaji wa kimsingi, na badala yake wanarudia maneno yao yaliyochakaa na yasiyo na maana.

Kwa utetezi wao duni wa demokrasia, wanasiasa hawa wanathibitisha jambo muhimu: Kama vile, licha ya mazungumzo yao yote ya uhuru, wanaanzisha sheria maalum na kufanya kampeni za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, vivyo hivyo, licha ya nyimbo zao zote juu ya utukufu wa demokrasia, hukosa kabisa hoja zozote halisi.

Wanathibitisha zaidi kwamba hawana chochote cha kuwapa Waislamu ambao wanataka kushikamana waziwazi na maadili ya Kiislamu, zaidi ya kulaani, dharau na madai ya utiifu kwa demokrasia inayougua.

Katika muktadha huu, tunarudia wito wetu kwa Waislamu wote: Msiipe pumzi ya bandia mfumo ulio katika mgogoro, unaogongana na kuupiga vita Uislamu wenu! Shauku ya wanasiasa ya kukutongozeni kwenye kibanda cha kupigia kura kamwe haihusiani na uamuzi shirika wala matarajio ya kupunguzwa chuki dhidi Uislamu, bali ni kuhusika katika misingi ya maadili na utiifu wa kisiasa. Badala yake, kama jamii ya Kiislamu, tunapaswa kuimarisha ushiriki wetu ndani ya mujtamaa uliojengwa juu ya msingi wa Uislamu na hivyo kuathiri ajenda ya kisiasa pamoja na mjadala na maoni ya umma.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu