Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  12 Safar 1442 Na: 1442/03
M.  Jumanne, 29 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uongozi wa kisekula Wadunisha Madrasa Zetu Kiasi Hiki!

Wakati tunapomshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa kupungua maambukizi ya Covid -19 humu nchini, wakati huo huo tunasikitishwa na hatua ya serikali ya kufungua vilabu vya vileo huku Madrasa za Kiislamu kutogusiwa kamwe. Suala hili la kufungua Madrasa pia halijahusishwa kwenye mjadala wa ufunguzi wa shule unaofukuta baina ya wazazi, wizara ya elimu na ile ya afya. Huu ni ubaguzi wa wazi usiofaa kwani ni jukumu la serikali kusimamia maslahi ya raia wake wote kwa ujumla. Licha ya kufahamu kwetu hali  duni ya Madrasa zetu leo ambayo kwa hakika imetokamana na kukosekanwa utawala wa Khilafah, lakini tunatambua dori muhimu ya vyuo hivi katika kuhifadhi shakhsiya za Kiislamu kwa wototo wetu.

Tawala za Kisekula siku zote hupambika na sifa mbili zenye kukinzana kwa wakati mmoja, Huku Madrasa wakiwa bado wamezifunga kwa kuhofia maambukizi, viongozi wanaonekana kwenye  mikutano wakihubiri porojo zao za kisiasa mbele ya halaiki huku wakikiuka masharti yote ya kujikinga na maambukizi. Je; ndani ya Madrasa ndio kuna maambukizi na kwenye mikutano hakuna? Fauka ya haya, kwa nini kuingiza nchi kwenye wimbi la kampeni za uchaguzi kana kwamba uchaguzi ndio mahitaji msingi ya raia? Chaguzi ngapi zimepita na bado hali za raia kila kukicha zinazidi kuwa mbaya.

Kudharau elimu ya Dini kunaingia katika ile ile itikadi potofu ya Kiilmaania inayotenganisha Dini na Maisha. Itikadi hii huwapa wanadamu nafasi ya kudharau Dini na elimu yake. Jambo hili lapaswa liamshe Waislamu wafahamu kwamba serikali yoyote inayobeba ilmaaniya katu haiwezi kudhamini waalimu wa Madrasa wala elimu ya Dini yetu. Fauka ya haya, Mfumo wa Kibepari umehujumu malengo ya elimu kwa ujumla kwa kuifungamanisha na maslahi ya kiuchumi. Kwa mtazamo huo katika serikali za kibepari, elimu ya dini huonekanwa kukosa manufaa yoyote yale ya kimada hivyo hubakia kudharauliwa.

Utawala wa Khilafah, utatoa elimu kwa watoto wote pasina na ubaguzi, kwa lengo la kuendeleza maarifa mbali mbali kama sheria, uhandisi na matibabu. Hivyo, Khilafah itajenga majengo ya taasisi za Kielimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu yataimarishwa na kuwekwa maktaba na maabara ya kutosha. Mbali na haya waalimu kwa ujumla watapewa heshima yao na kutunzwa maisha yao. Yote haya yatafanywa kwa lengo la kuwa na wataalamu na mujtahiduna watakaoletea raia ustawi wa kielimu na wa kimaisha jumla na kuwawezesha kuwa na  ufanisi sio tu wa hapa duniani bali na kesho akhera.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu