Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Muharram 1445 Na: 1445/02 H
M.  Alhamisi, 10 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Kenya Ulikutana na Sheikh Abdul Halim Hussain, Kadhi Mkuu wa Kenya
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Kenya, ukiongozwa na Ustadh Mahd Ali, mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Kenya, akiandamana na Ustadh Shaaban Mwalimu, mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir Kenya, na Ustadh Shaaban Rajab, mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahir Kenya, walikutana na Sheikh Abdul Halim Hussain, Kadhi Mkuu wa Kenya anayeishi jijini Nairobi.

Ujumbe wa Hizb ulipokewa kwa uchangamfu, na mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Mahd Ali, na Ustadh Shaaban walimpongeza kadhi huyo na kumshauri juu ya umuhimu wa kushikamana na Uislamu katika nyanja zote za maisha. Walimpa vitabu viwili, Njia (Manhaj) ya Hizb ut Tahrir ya Mageuzi na Al-Khilafah.

Ujumbe huo pia ulikutana na Sheikh Mohammed Uthman, Imamu wa Msikiti wa Landis jijini Nairobi.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu afungue nyoyo za Ulema (wanazuoni) kufanya kazi na Hizb ut Tahrir katika kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu