Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  2 Safar 1438 Na: 1438/02
M.  Jumatano, 02 Novemba 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfumo Fisadi Huzaa Maafisa Wafisadi

Kwa mara nyingine tena, kashfa nyingine ya ufisadi imeonekana. Wakati huu inawahusisha maafisa wa Wizara ya Afya wanaozuiliwa juu ya ufujaji wa zaidi ya Shilingi bilioni tatu ($300m). kama kawaida, uchunguzi umeanzishwa lakini kwa yakini hakuna atakaye shitakiwa. Kwa upande mwingine, viongozi wa kisiasa walio katika utawala pamoja na walio katika upinzani wameigeuza kadhia hii kuwa mchezo wa lawama! Kuhusiana na hili, Chama cha Kisiasa cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir kingependa kutaja yafuatayo:

Ni khiyana kubwa na dhulma kwa yale yanayoitwa mamlaka yanayo shikilia nyadhifa za umma yakidai kuwakilisha maslahi ya umma, badala ya kufanya kazi kuimarisha kiwango cha maisha ya raia; wao wanashindana kwa nguvu juu ya ufujaji wa mali za umma. Lakusikitisha, sakata hii mpya inajiri wakati ambapo maelfu ya Wakenya wako ukingoni mwa baa la njaa kutokana na ukame.

Hii ni dhahiri kuwa taasisi za kupambana na ufisadi licha ya kubadilishwa majina zimeshindwa kukabiliana na uovu huu. Uchungu ni kuwa baadhi ya wakuu wa taasisi wenyewe wamepatikana katika ufisadi. Mwishoni mwa Septemba mwaka huu, mkuu wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi Philip Kinisu alijiuzulu kutokana na kuhusishwa na Kampuni ya Esaki ambayo ililipwa kwa miamala isiyoeleweka na Huduma ya Vijana ya Kitaifa

Dhati ya ufisadi nchini Kenya na ulimwengu kwa jumla, imechipuza kutokana na hadaa ya kuukumbatia mfumo wa kimakosa wa kikoloni: Urasilimali. Mfumo huu fisidifu na uliofeli ambao kipimo chake ni kimoja pekee nacho si chengine ila kipimo cha kimada ambapo huwafanya wafuasi wake kujihusisha na ulimbikizaji wa mali kupitia njia chafu. Hivyo, ufisadi kamwe hauwezi kumalizika maadamu mfumo huu muovu unaendelea kutawala ulimwengu.  

Kwa kuwa msingi wa tatizo hili ni Urasilimali, suluhisho halisi na lenye mashiko liko katika kuuondoa mfumo huu uliofeli. Kuubadilisha kwa mfumo adilifu ambao si mwingine isipokuwa Uislamu ambao kipimo chake pekee cha vitendo vya mwanadamu ni yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyakidhia na sio manufaa ya kimada. Hivyo basi mujtama unapaswa kuhifadhiwa dhidi ya vitendo vyovyote viovu kwa sababu vinamkasirisha Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, Uislamu umeuidhinisha mujtama mzima kuamrisha mema na kukataza maovu bila ya kujali kama mhalifu ni tajiri au masikini, mtawala au raia wa kawaida.    

Uislamu pia unamtaka mtawala kumhisabu na kumwondoa afisa yeyote mfisadi bila ya uoga wala mapendeleo. Ni kupitia maadili haya; Uislamu uliyo yafungamanisha na Dola ya Khilafah Rashidah ambayo pekee ndiyo yatakayo maliza aina zote za maovu na kueneza aina zote za wema ulimwenguni. 

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu