Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 10 Jumada I 1442 | Na: 017 / 1442 H |
M. Ijumaa, 25 Disemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir cha Zindua Kampeni ya Kimataifa kwa Anwani: "Waislamu wa Sri Lanka Wananyanyaswa, Wafu na Walio Hai!"
(Imetafsiriwa)
Ili Kuzuru Ukurasa wa Kampeni Bonyeza Hapa
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yatangaza kuzinduliwa kwa kampeni ya kimataifa ya kunyanyua uelewa wa ulimwengu juu ya dhulma kubwa na unyanyasaji unaowakabili Waislamu nchini Sri Lanka, na kuitaka serikali ya Sri Lanka kumaliza sera yake ya aibu ya uteketezaji wa lazima wa miili ya wahasiriwa wa Kiislamu wa Covid-19 nchini humo. Tangu Aprili mwaka huu, Waislamu wengi ambao wamepatikana kuwa na virusi vya Korona baada ya kufa wamechomwa ikikiuka imani zao za Kiislamu ambazo zinalazimisha kuzikwa kwa wafu. Kwa kweli, Waislamu kadhaa ambao walikuwa wamechomwa hawakuwa wamepimwa COVID wala hata kupatikana bila ya virusi hivyo. Mnamo tarehe 9 Disemba, mtoto wa Kiislamu wa siku 20 aliyepima virusi vya ukimwi baada ya kufa, alichomwa bila idhini ya wazazi. Mnamo tarehe 1 Disemba, Mahakama ya Upeo ya Sri Lanka ilitupilia mbali rufaa 12 zilizoletwa na familia za Kiislamu na za Kikristo na asasi za kiraia zikipinga sera ya kuteketeza miili, ikikataa hata kusikiliza kesi zao, na kutotoa sababu yoyote ya kukataa kwake kusikilizwa juu ya suala hilo, ikiakisi jinsi gani wanyonge wamekosa nguvu chini ya nidhamu za kisekula za kidemokrasia kuondoa dhulma dhidi yao. Utawala wa kitaifa wenye nia ya kijamii, wa kibudha nchini Sri Lanka ulitoa sera ya COVID, wakijua kwamba Waislamu wanauona uchomaji wa miili kama ukiukaji utukufu wa mwili wa mwanadamu. Pia walipuuza ushauri kutoka kwa wataalam mashuhuri wa kimataifa wa virusi na magonjwa, pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni ambao walisema kwamba wahasiriwa wa COVID-19 wanaweza kuzikwa salama bila hatari yoyote kwa afya ya umma. Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba hii ni sera ya hofu kwa Uislamu inayotekelezwa licha ya idadi ya Waislamu, inayolenga kuumiza hisia zao za ndani kabisa. Kwa kweli, serikali ya Sri Lanka inalitumia janga hili la maambukizi kupata uungwaji mkono zaidi kwa utawala wake kutoka kwa Mabudha wenye hisia za kitaifa dhidi ya Waislamu katika jamii, na pia kuendeleza ajenda yake wenyewe ya kupinga Uislamu nchini humo.
Waislamu nchini Sri Lanka wamekabiliwa na ubaguzi, uchafuzi wa majina na vurugu kwa miaka mingi kutokana na kuongezeka kwa utaifa wa Wabudhi wenye msimamo mkali nchini, pamoja na vikundi kama vile Bodu Bala Sena (BBS) (Kikosi cha Nguvu cha Wabudhi) na watawa wa Wabudhi wenye misimamo migumu ambao hupewa msukumo kutoka kwa wenzao nchini Myanmar ambao waliwatesa Waislamu wa Rohingya. Kwa kweli, makubaliano dhidi ya Uislamu tayari yameshaanzishwa kati ya BBS na "Harakati ya 969" dhidi ya Waislamu nchini Myanmar ambayo ilikuwa na jukumu la kuchochea vurugu dhidi ya Waislamu wa Rohingya. Mashirika yote mawili yaliahidi kuunda muungano wa kukusanya vikundi vingine vya Mabudha dhidi ya Waislamu na Uislamu katika eneo hilo. Katika miaka ya hivi karibuni, Waislamu wamepata unyanyasaji wa kila aina: Wanawake wa Kiislamu wanaovaa Hijab wamehangaishwa na kuambiwa wavue mavazi yao ya Kiislamu wanapoingia kwenye maduka kadhaa, majengo ya serikali, shule, na hata wanapotafuta matibabu hospitalini; marufuku ya Niqab ilitekelezwa kwa jamii; kumekuwa na wito wa biashara za Waislamu kususiwa; Uwekaji vibandiko vya halal kwenye bidhaa umeondolewa; kumekuwa na ukamataji wa kiholela wa mamia ya Waislamu na misako ya kibaguzi ya nyumba za Waislamu wa nyenzo za Kiislamu; na kumekuwa na mashambulizi mengi ya kutisha ya umati kwenye misikiti na nyumba za Waislamu na maduka. Sasa, pamoja na haya yote, Waislamu wanateseka na uchungu wa kutoweza hata kutekeleza ibada za mwisho za kidini kwa wapendwa wao na kufa kwa heshima.
Kama inavyotarajiwa, serikali za ulimwengu, pamoja na tawala za ardhi za Waislamu zimeshindwa kuwasaidia Waislamu wa Sri Lanka, kwa mujibu wa tabia yao ya kawaida ya kuwatelekeza Waislamu waliodhulumiwa ulimwenguni. Lakini, sisi Ummah wa Uislamu kamwe hatutawatelekeza kaka na dada zetu Waislamu nchini Sri Lanka. Sisi katika Hizb ut Tahrir tutapaza sauti ulimwenguni kuwaunga mkono na dhidi ya dhulma kubwa ambayo wanaipata. Na, tutafanya kazi na juhudi zetu zote kusimamisha tena mlezi, ngao na mlinzi wao: Nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt) - Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itatoa makao kwa wanyonge na kusimama kama mlinzi wa haki na Dini ya Waislamu bila kujali wanakoishi. Tunatoa wito kwa wale wote wanaosimama kwa ajili ya haki kuunga mkono kampeni hii muhimu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
﴾وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴿
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [al-Anfaal: 72]
Kampeni hii yaweza kufuatiliwa katika: http://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/afisi-kuu-ya-habari/1316.html na katika ukurasa wa Facebook: https://www.facebook.com/womenscmoht/
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |