Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 008
M.  Jumanne, 27 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto Wapendwa wa Ash-Sham Wafariki Baada ya Boti za Wakimbizi Kuzama. Je, Tunapoteza Wangapi Zaidi Bila Khilafah?!

(Imetafsiriwa)

BBC iliripoti mnamo tarehe 23 Septemba 2022 kwamba wakimbizi wahamiaji 71 walipatikana katika mashua inayozama nje ya pwani ya Syria. Makumi wameripotiwa kufariki. Watu 20 kati ya walionusurika walipelekwa katika jiji la Tartus kutibiwa hospitalini. Wanawake na watoto wa Lebanon, Syria na Wapalestina walikuwa miongoni mwa watu 120 hadi 150 waliokuwemo ndani. Mustafah Mesto alikuwa mmoja wa ndugu wa Ummah ambaye alifariki akiwa na binti zake wawili na mwanawe wa kiume. Mama yake Adla amehuzunishwa na msiba huo lakini hana njia ya kupata majibu ya jinsi janga hili lilivyotokea. Amenukuliwa akisema: “Alikimbia umaskini na hali mbaya waliyotuacha nayo. Wanasiasa hawa hawakuweza kujali hata kidogo maisha yetu. Hakuna kitakachomrudisha kwangu, hakuna kitakachowarudisha watoto wake wadogo kwangu.”

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Lebanon inawahifadhi takriban wakimbizi milioni 1.5 wa Syria, na karibu 14,000 kutoka nchi nyingine. Inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi kwa kila mtu duniani. Waangalizi wa kimataifa wamesema kuwa vivuko hivyo hatari kwa boti vimeongezeka kwa zaidi ya 70% huku mzozo wa kiulimwengu ukiongezeka bila ya kuonekana mwisho. Zaidi ya 80% ya wakaazi wa Lebanon wang’ang’ana kumudu chakula na dawa. Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, uondokaji kutoka nchi hiyo pekee ulikaribia kuwa maradufu katika 2021 kutoka 2020.

Hali mbaya ya maelfu ya wakimbizi waliozama inaonyesha kwamba hali hii mbaya ya baharini imekuwa desturi ya kimataifa. Sekta nzima inapatikana katika majaketi bandia ya kuokoa maisha na biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu ambayo haidhibitiki na kila shirika la kutekeleza sheria ya kimataifa. Watoto wetu wadogo wasio na hatia wanapelekwa katika ukweli bandia wa maisha bora ila tu kusalitiwa imani yao.

Khilafah chini ya uongozi wa ikhlasi wa Khalifa anayechunga mambo ya Ummah kamwe haingekubali hasara hii katika maisha ya binadamu na hali ya kukata tamaa ya muda mrefu. Kuhama kwa kulazimishwa ni uhalisia wa kusikitisha wa Waislamu waliokata tamaa kwani wamepoteza matumaini kabisa. Hakuna mzazi ambaye angeweka watoto wake hatarini kwa hiari isipokuwa alikiria sababu za uhai na kifo; kwa upande mwingine, ni mlezi gani wa kiume angepeleka mke na watoto wake mikononi mwa kifo? Je, mnaweza kufikiria utisho wa kujua kwamba unazama na hakuna mtu anayekuja na kwamba lazima ushuhudie watoto wako wakipiga kelele za kuomba msaada, lakini huwezi kufanya chochote?

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) tusishuhudie uchungu na huzuni kama hiyo, na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amrudishe mlinzi na ngao yetu hivi karibuni - Khilafah kwa njia ya Utume itakayouondoa Ummah huu kutokana na hali hii ya kutapatapa ya mateso na ukandamizaji wa wanadamu na kurudisha usalama na ulinzi kwa Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلاَئِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الأَرْضِ خَلِيفَةً قَالُواْ أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاء وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لاَ تَعْلَمُونَ)

“Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.” [Al-Baqara: 30].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu