Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  13 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 011
M.  Jumapili, 09 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Afghanistan na Unafiki wa Kimagharibi
(Imetafsiriwa)

Tangu utawala wa Marekani uondoke Afghanistan na serikali ya Taliban kuchukua madaraka, maamuzi ya nchi za Magharibi yalianza kuongezeka, hasa baada ya kundi la Taliban kuchukua maamuzi ambayo Magharibi inayaona kuwa hayaendani na hadhara na mtindo wake wa maisha, kama vile kulazimisha niqab kwa wanawake na kutenganisha madarasa kati ya wanaume na wanawake, pamoja na maamuzi mengine.

Vyombo vya habari vya Magharibi vimeunda kimbunga cha ripoti na habari ambazo kwazo vinauonyesha Uislamu wa kisiasa, kimsingi Taliban, kama zimwi ambalo linaweza kuwatia hofu Wamagharibi kutokana na Uislamu.

Umoja wa Mataifa na mashirika yanayohusiana nao yote yamekuwa na wasiwasi juu ya watoto wa Afghanistan, na kwamba wanawaogopea watoto hao kutokana na Taliban! Na katika picha ambayo mara nyingi hukaririwa, huruma ya Magharibi ilifurika hadi ikajaza upeo wa macho yetu, ikipiga kelele juu ya mateso ya watoto wa Afghanistan ambao wamenyimwa elimu, wanaoteseka kutokana na ubaguzi kwa misingi ya jinsia, na wanaolazimishwa kufanya kazi na ukimuuliza mmoja wao matamanio yao ni nini hawajui wanataka nini! Katika ripoti moja iliyoandaliwa na shirika la ‘Save the Children’ na kuchapishwa na ABC News, ilisema imefanya uchunguzi wa watoto 1,400 na karibu walezi 1,400. Matokeo yake ni kwamba asilimia ya familia zilizosema kuwa na mtoto wanaofanya kazi ilipanda kutoka 18% hadi 22% kutoka Disemba hadi Juni. "Hiyo inaweza kuashiria zaidi ya watoto milioni moja kote nchini wanafanya kazi," ripoti hiyo iliongeza.

Ripoti hizi za vyombo vya habari hazina weledi na usahihi, kwa vile ziliandikwa kwa kuegemea matakwa na maoni yaliokwisha undwa tangu awali, na watu milioni 40 walichukuliwa uamuzi kutokana na uchunguzi wa watoto 1,400! Kisha ripoti ikasema kwamba kuna watoto milioni moja wanaofanya kazi, na kwamba uingizaji wa idadi unakuwa habari iliyothibitishwa wakati akili ya Magharibi inapobuni kwa matakwa yake wenyewe na kuitumia kuwashawishi watu juu ya kile inachofikiri!

Huruma ya Wamagharibi inafurika kwa huzuni juu ya watoto wa Afghanistan wanaofanya kazi ngumu katika mazingira ya majira ya baridi na kiangazi ili kuzipatia familia zao chakula, lakini haitambui rasilimali za nchi ambayo inaziiba ili kuishi kwa ustawi! Wamagharibi wanalia juu ya mtoto wa Afghanistan ambaye anafanya kazi ili aendelee kuishi, na msichana ambaye amejifunika uso, lakini wanafumbia macho miaka ya uvamizi ambapo maelfu ya watoto waliuawa, na nchi ikaonja majanga! Wamagharibi wanawafumbia macho watoto wa Yemen na Afrika ambao utajiri wao unaibiwa na nchi za Magharibi, ambao wameachwa kufa kwa njaa! Na kuwafumbia macho watoto wa Syria na Palestina wanaouawa na Mayahudi na Warusi, lakini wanajali tu watoto wa Ukraine, labda kwa sababu wana ngozi nyeupe na macho ya samawati, tofauti na Waafghan na Waislamu kutoka Mashariki ya Kati!

Jaribio la Magharibi la kupotosha sura ya Uislamu kwa kupinga uwezo wa Taliban katika kusimamia masuala ya nchi ni jaribio ovu na lisilofanikiwa, ikiwa Mwenyezi Mungu atapenda, kwa sababu Uislamu ni sheria ya haki ya Mwenyezi Mungu isiyoathiriwa na batili. Uislamu hauwakilishwi na Taliban, bali ni Taliban ndio wanaojulikana na kuhukumiwa na Uislamu.

Uislamu, pamoja na mifumo yake ya kiuchumi na sera ya kuchunga mambo ya Ummah, una uwezo wa kufikia maisha ya starehe na ya kutosheka na kumpa kila mtu haki yake kamili ya chakula, mavazi na makaazi, lakini pale tu unapotekelezwa kwa usahihi na kikamilifu ndani ya dola isiyo na mgawanyiko na bila ya utabikishaji wa hatua kwa hatua, na bila kurudi katika mamlaka yoyote isipokuwa mamlaka ya Mwenyezi Mungu, Mmoja, Asiyeshindika. Na kwamba haya yatatokea karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Na ndilo ambalo Magharibi inalijua vyema na inajaribu kula njama ya kulizuia na kuwafukuza watu kutokana nalo. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ametupa ahadi, na tuna yakini na maregeo yake matukufu ambayo umma wetu utapata izza, watoto wetu watapata mustakbali mwema, na adui yetu atachukua kile anachostahiki, ikiwa Mwenyezi Mungu atapenda.

(أَمْ يُرِيدُونَ كَيْداً فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ)

“Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.” [At-Tur: 52-42]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu