Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  22 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 013
M.  Jumanne, 18 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Palestina Wanalilia Majeshi ya Waislamu
(Imetafsiriwa)

Tangu mwanzoni mwa 2022, zaidi ya watoto 45 wa Kipalestina wameuawa shahidi, na uvamizi wa Kiyahudi umeongezeka katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem, katika wiki chache zilizopita, ambao umesababisha vifo vya watoto zaidi, wa mwisho wao akiwa ni mtoto Mahmoud Al-Samoudi, mwenye umri wa miaka 12, ambaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata. Ilifanyika katika uvamizi wa Jenin, na kabla ya hapo tukio la kutisha lilitokea ambapo mtoto wa miaka 7, Rayan Suleiman, aliuawa shahidi baada ya kupata mshtuko wa moyo kutokana na hofu wakati akiwakimbia wanajeshi wa Uvamizi.

Pia kuna wanawake na watoto wengi wanaoteseka kutokana na mzingiro uliowekwa na vikosi vya uvamizi dhidi ya maelfu ya familia katika kambi ya Shuffat, mji wa Anata, kambi ya Al-Aroub na Nablus, na pia kutokana na mashambulizi ya walowezi kwenye nyumba na mali. ikiwa ni pamoja na kuvunja madirisha, na kuteketeza mashamba na magari.

Haya yote yanatokea huku kila mtu akitazama. Watetezi wa haki za binadamu, haki za watoto, na sheria za kimataifa wako kimya, isipokuwa kwa kushambulia kile kilicho katika utabikishaji wa hukmu yoyote ya Uislamu inayohusiana na wanawake au watoto. Wanazingatia Sheria ya Uhuru na Ulinzi wa Familia, na wakati mwingine na Sheria ya Ulinzi wa Mtoto, ambayo imefungika tu na kumlinda mtoto kutokana na baba na mama yake, na sio kutokana na uvamizi wa kikatili wa umbile la Kiyahudi.

Kwa upande wa Mamlaka ya Palestina, bado ingali inaiomba jumuiya ya kimataifa kuwalinda watoto hawa, na bado inalalamikia mhusika wa uhalifu kumuonea huruma mwathiriwa. Mwakilishi wa Kudumu wa Mamlaka ya Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour, alituma barua tatu zinazofanana kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama mwezi huu. (Gabon) Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mauaji ya kila siku, kujeruhiwa, kukamatwa, kudhalilishwa na kiwewe kwa Wapalestina, hasa vijana na watoto, mikononi mwa vikosi vinavyovamia kwa mabavu, alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama, kuchukua hatua mara moja kwa kuzingatia sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayokariri rekodi hiyo hiyo iliyovunjwa ya haja ya uingiliaji kati wa kimataifa ili kuwalinda watu wa Palestina, hususan watoto ambao maisha na mustakabali wao uko katika hatari kubwa kutokana na uvamizi huo haramu wa kikoloni wa utawala wa kibaguzi. Vile vile amewataka wachukue hatua za haraka za kuiwajibisha dola ya Kiyahudi, jeshi lake na walowezi kwa sera na mienendo yote haramu katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu ikiwemo Jerusalem Mashariki!

Enyi Waislamu popote pale, Enyi Majeshi ya Waislamu:

Watoto wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wanatafuta msaada wenu kila siku na kila saa. Mtoto shahidi Rayan anakuombeni kwa moyo wake mdogo, ambao ulisimama kwa hofu kutoka kwa viumbe vidhalilifu zaidi vya Mwenyezi Mungu, kwamba mulipize kisasi kwa ajili yake dhidi yao. Hii ni pamoja na mamia, ikiwa si maelfu, ya watoto na wanawake waliokufa mashahidi, au waliojeruhiwa, waliolemazwa, waliokosa makao, au waliopoteza baba zao na walezi wao. Je, kuna jibu au mtoaji usaidizi?! Mwenyezi Mungu asema:

(وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ)  

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia,” [Al-Anfal:72]. Je, munafanya nini?!

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu