Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  16 Rajab 1443 Na: H.T.L 1443 / 07
M.  Alhamisi, 17 Februari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Ujumbe kutoka Harakati ya Jihad Al-Islami nchini Palestina

kwa Afisi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon
(Imetafsiriwa)

Ndani ya muundo wa ziara za pande zote kati ya Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Lebanon na vyama vya kisiasa vya Lebanon na Palestina, ujumbe wa ndugu katika Harakati ya Jihad Al-Islami nchini Palestina mnamo tarehe 16/2/2022 ukiongozwa na Mkuu wa Mahusiano ya Kiislamu wa Harakati ya Jihad Al-Islami nchini Lebanon Hajj Shakib Al-Ayna, na mbele ya uwepo wa Hajj Muhammad Rashid, Afisa wa Mahusiano ya Kijamii wa Harakati hiyo nchini Lebanon, na Ustadh Jihad Muhammad, afisa wa faili wa UNRWA wa Harakati hiyo nchini Lebanon, ulitembelea Afisi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon katika mji wa Sidon. Ujumbe huo mtukufu ulipokelewa na Mhandisi Bilal Zaidan, mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Wilayah hii ya Hizb, na wanachama wa Kamati ya Shughuli upande wa kusini, Mhandisi Wajdi Hussein, Hajj Hassan Nahas na Hajj Imad Abu Al-Hija. Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir ulikuwa umewatembelea ndugu hawa wa Harakati ya Jihad katika Kambi ya Burj al-Shamali mnamo tarehe 12/2/2022.

Katika mikutano hiyo, majadiliano yalilenga juu ya haja ya watu wetu katika kambi za Wapalestina kutoingizwa katika mizozo yoyote au kutumia silaha katika mapatano baina ya makundi ya mielekeo tofauti, haswa kwa kuzingatia dhurufu za kieneo na kimataifa, ambazo zinawakilishwa katika michakato ya usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, ambao tawala zinashindana katika nchi za Kiislamu kwa ajili yake. Na kwa kuzingatia majaribio ya kuongeza utawala wa Marekani juu ya Lebanon, ambapo Marekani inajenga ubalozi wake wa pili kwa ukubwa katika eneo hili, licha ya kuikashifu Lebanon na wanasiasa wake kama wafisadi. Hili linaonyesha kiwango ambacho Lebanon itakabiliana nacho mbele ya udhibiti huo wa moja kwa moja, na kile ambacho njia hii inahitaji kwa Lebanon kufanya kuhusiana na faili ya usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi. Hii ni changamoto kubwa kwa wale ambao lengo lao ni kupambana na mnyakuzi mvamizi huyu wa Ardhi Tukufu ya Palestina. Hizb imesisitiza kuwa kiungo muhimu zaidi cha kadhia ya Palestina ni Uislamu huu mtukufu. Kwa hivyo, iwapo kadhia hii litakosekana au kufifia katika maandishi na mazungumzo kutokana na baadhi ya mahesabu, Qur’an Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) zitaendelea kulihuisha na kulinyanyua jina lake, kwani ndio msingi wa kauli ya Mola Mlezi wa walimwengu wote:

(سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ)

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Isra: 1]. Imehifadhiwa kwa ulinzi wa Mwenyezi Mungu wa Qur'an hii.

Hizb pia iliweka wazi kwa ujumbe huo mtukufu kwamba kuendelea kupambana na adui kunahitajika kwa kila mtu ambaye anatabanni hatua za kisilaha kupigana na umbile hilo la Kiyahudi, huku ikisisitiza kuwa nususi zote zinaashiria kuwa ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kutoka mikononi mwa Mayahudi umejengwa juu ya msingi wa kuasisiwa nguvu ya Waislamu, sio kuwa Wapalestina au Walebanon au kwa njia nyenginezo za mipaka iliyochorwa na mkoloni, bali kwa wao kuwa Waislamu, waja wa Mwenyezi Mungu, kama ilivyotajwa katika Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kama ilivyosimuliwa na Al-Bukhari: «يَا مُسْلِمُ يَا عَبْدَ اللهِ» “Ewe Muislamu, Ewe mja wa Mwenyezi Mungu.”

Mwishoni mwa mkutano huu, Hizb ilitaraji kuwa Harakati hii itakuwa na dori katika kutoruhusu damu ya wale waliojitoa mhanga katika njia hii kutumiwa katika meza za mazungumzo na maridhiano, ambapo Ummah umeteseka katika maisha yote ya kadhia hii, na kwamba dori yao katika kambi za Wapalestina ndani ya uwanja wa Lebanon ni kumaliza mzozo wowote, na sio kuruhusu kuburuzwa ndani ya miradi inayoongozwa na dola za kieneo na kimataifa.

Kwa kutamatisha, tunaweza tu kuwashukuru ndugu katika Harakati ya Jihad Al-Islami kwa ziara hii ya ukarimu, tukitarajia kuendelea kwa mawasiliano kwa manufaa na maslahi ya umma, kwa watu wetu ndani ya Palestina na kambi za Wapalestina nchini Lebanon, na hata kwa umbo pana zaidi lenye kuwaunganisha watu wa Palestina na Lebanon, Umma wa Kiislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu