Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  13 Jumada I 1444 Na: H.T.L 1444 / 03
M.  Jumatano, 07 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Vichwa vya Kutiliwa Shaka kama vile Jinsia, na chini ya Kisingizio cha Kutiliwa Shaka cha Mikataba ya Kimataifa!

Jamii na makundi yanayofadhiliwa na Magharibi yanajaribu kueneza sumu yao miongoni mwa Waislamu

(Imetafsiriwa)

Siku chache zilizopita, tuliona makundi, vyama, na taasisi zinazofungamana na Umoja wa Mataifa zikifanya kampeni zenye vichwa vinavyobeba maana zinazokinzana na herufi za kimsingi za Waislamu kwa upande mmoja, na hazina uhalisia wowote miongoni mwetu kwa upande mwingine. Badala yake, ni majaribio ya kuonyesha matatizo ya nchi za Magharibi na ufisadi wa mifumo yake ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwenye uhalisia wetu! Kama vile wito wa kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake, kuzuia unyanyasaji dhidi ya kile walichokiita jinsia, na ufeministi! Katika kupotoka kwa vyama na taasisi hizi kutoka kwa asili ya kazi zao ambazo watu wamezikubali kutokana na hali ngumu ya maisha na fedha zinazotolewa na taasisi hizi, kuwa vyama na mashirika ya kutetea upotovu wa kimwili na kiakili, chini ya jina la uhuru ambao jamii za Magharibi zimerithi, jambo ambalo halihitaji maelezo mengi. Na tunawaambia wao wote:

- Katika Dini yetu na katika duru zetu, kiasili wanawake hutazamwa kama kina mama na wake nyumbani na kwamba wao ni heshima ambayo lazima ihifadhiwe, na hii haizuii ushiriki wao katika maisha ya umma, kazi na maendeleo ya Waislamu ndani ya udhibiti uliowekwa na Mwenyezi Mungu, Muumba wa kila kitu. (وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَى) “Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike” [An-Najm 53:45]. Ambaye, Utukufu ni Kwake, aliufanya uhusiano unaotokana na kukutana kwa mwanamume na mwanamke kuwa mfumo kamili unaojulikana kama mfumo wa kijamii.

- Mtazamo wa wanawake katika dini yetu unatokana na yale Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake (saw) waliyowaambia Waislamu, kama kauli yake katika Surat An-Nisaa: (وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ) “Na kaeni nao kwa wema.” [An-Nisa 4:19]. Ni kama Hadith yake (saw):

«إِنَّمَا النِّسَاءُ شَقَائِقُ الرِّجَالِ» “Hakika wanawake ndugu toka ni toke za wanaume”. Na yeye (saw) amesema: «اسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْراً» “Watendeeni wema wanawake”. Je, kuna kitu kikubwa zaidi kuliko hicho katika kitabu kitukufu kabisa cha Waislamu, Qur'an Tukufu, ambacho Waislamu hukisoma usiku na mchana, kuliko kwamba moja ya sura zake tukufu zaidi ni sura inayoitwa Surat An-Nisaa?

- Wito wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake ni wito wenye shaka na uliopunguzwa, kwa sababu Uislamu hauuhitaji, kwani unapinga unyanyasaji dhidi ya wanawake, wanaume, wavulana, wapumbavu na wendawazimu, ambao wako chini ya hukmu za Sharia, na sio tu wanawake pekee. Ajabu ni kwamba wanaotoa wito wa kuwatetea wanawake ndio wanaowafanya kuwa nyenzo za propaganda, vyombo vya habari na ponografia! Ambapo kusudi likiisha, atatupwa, katika nchi yao, kando ya barabara!

- Iwapo baadhi ya Waislamu watakengeuka kwa sababu ya dini yao mbaya na maadili mabaya katika kuamiliana na wanawake, wanaume au watoto, basi ni haramu na ni mapungufu kwa waliofanya jambo hili, na udhibiti wa Uislamu katika kushughulikia mambo haya na kurudisha haki kwa mmiliki wake iko wazi na isiyo na utata.

- Kinachotetewa juu ya suala la jinsia na aina ya kijamii, yaani, kuukubali ushoga ni hali ya kimaumbile, hakutokani na msingi wa sheria rahisi za sayansi na dawa ambazo zimethibitisha kuwa jambo hili sio la kuzaliwa. Bali ni kwa sababu ya kulegeza msimamo kunakotokea katika jamii za Kimagharibi na wazo la kwamba mwanadamu ameumbwa kwa ajili ya starehe, ambapo mara kwa mara anatafuta starehe mpya, hata kama zinapingana na ghariza ya mwanadamu, hata ghariza ya wanyama, hadi magonjwa ya kuambukiza yakatokea ndani yao ambayo hatuhitaji kuyaorodhesha. Na iwapo kesi za namna hii zipo miongoni mwetu, basi zinashughulikiwa kwa mujibu wa vile wanazuoni wa fiqhi, matibabu na utaalamu wanavyosema, na si wakurugenzi, wajumbe na bodi za wakurugenzi wa vyama wanaonufaika na ufadhili.

Enyi wamiliki wa vyama na masekula na wale wanaowaunga mkono: Jueni kwamba kuna wanaume miongoni mwa Waislamu na nchi zao ambao wameifanya hamu yao kuwa ni kulinda nchi yao licha ya dhurufu zote ngumu, mpaka Mwenyezi Mungu Ajaalie nusra yake na tamkini yake kwa waja wake. Wanaume hawa watakuwa ukuta imara ambao juu yake jaribio lolote la kutia shaka na ovu litavunjiliwa mbali, hata kama pesa na juhudi zote zitatumika juu yake, kwa sababu tunazingatia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ)

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal 8:36].

Enyi Waislamu: Kampeni ni kali dhidi ya nchi yenu ya kujaribu kuiondosha Dini yenu na heshima yenu, na hapa tunawakumbusha kutafakari hadith hii tukufu kutoka katika mkusanyiko wa maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«يا مَعْشَرَ المهاجرينَ! خِصالٌ خَمْسٌ إذا ابتُلِيتُمْ بهِنَّ، وأعوذُ باللهِ أن تُدْرِكُوهُنَّ: لم تَظْهَرِ الفاحشةُ في قومٍ قَطُّ، حتى يُعْلِنُوا بها، إلا فَشَا فيهِمُ الطاعونُ والأوجاعُ التي لم تَكُنْ مَضَتْ في أسلافِهِم الذين مَضَوْا، ولم يَنْقُصُوا المِكْيالَ والميزانَ إِلَّا أُخِذُوا بالسِّنِينَ وشِدَّةِ المُؤْنَةِ، وجَوْرِ السلطانِ عليهم، ولم يَمْنَعُوا زكاةَ أموالِهم إلا مُنِعُوا القَطْرَ من السماءِ، ولولا البهائمُ لم يُمْطَرُوا، ولم يَنْقُضُوا عهدَ اللهِ وعهدَ رسولِه إلا سَلَّطَ اللهُ عليهم عَدُوَّهم من غيرِهم، فأَخَذوا بعضَ ما كان في أَيْدِيهِم، وما لم تَحْكُمْ أئمتُهم بكتابِ اللهِ عَزَّ وجَلَّ ويَتَخَيَّرُوا فيما أَنْزَلَ اللهُ إلا جعل اللهُ بأسَهم بينَهم»

Enyi Muhajirina, kuna mambo matano mtakayojaribiwa, na najikinga kwa Mwenyezi Mungu msije mkawa hai mkayaona. Uasherati hautadhihiri kwa watu kiasi kwamba wanaufanya waziwazi, isipokuwa itajitokeza tauni na maradhi ambayo hayakujulikana miongoni mwa watu wao waliotangulia. Hawatapunja katika mizani na vipimo isipokuwa watapigwa na njaa, balaa kali na dhuluma ya watawala wao. Hawatanyima Zaka ya mali yao, isipokuwa mvua itazuiliwa kutoka mbinguni, na lau si wanyama, mvua kamwe isingewanyeshea. Hawatavunja ahadi yao na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atawasaliti kwa maadui zao kuwashinda na kuchukua baadhi ya yale yaliyomo katika milki yao. Na viongozi wao hawatatawala kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa na khiari katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, isipokiwa Mwenyezi Mungu atawafanya wapigane wao kwa wao.” Basi jihadharini, enyi Waislamu, amrisheni mema na mukataze maovu, na fanyeni hima kujadidisha ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ahadi ya Mtume wake (saw) na kuregesha hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ili iwe katika mikono ya Waislamu wenye ikhlasi chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inamchunga kila mtu anayeishi ndani ya boma lake, sio kama wema na upendeleo, bali kama jukumu kwa hukmu Shariah.

Na sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon hatutasita hata dakika moja katika kutetea matukufu, heshima na maslahi ya Waislamu. Na kampeni yetu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu itaendelea kudhihirisha ufisadi na uwongo wa yale ambayo hawa na mabwana zao wanayalingania katika Magharibi mkoloni kafiri, na mikataba yote ya kutiliwa shaka kama vile CEDAW au yale yaliyotolewa na yatatolewa na kupitia makongamano ya watu, yatakuwa ni shabaha ya mishale yetu na chini ya miguu yetu na miguu ya waumini wote, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tukizingatia kauli ya Mola wetu Mtukufu:

(مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعاً إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَكْرُ أُولَٰئِكَ هُوَ يَبُورُ)

“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na a'mali njema Yeye huitukuza. Na wanao panga vitimbi vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya hao vitaondokea patupu.” [Fatir 35:10].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu