Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  6 Dhu al-Hijjah 1444 Na: H.T.L 1444 / 12
M.  Jumamosi, 24 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutabikisha amri ya Mwenyezi Mungu katika Takbir, Tahlil, na Tahmid ndio usalama wa kweli, sio wa vyombo vya usalama na vyumba vyeusi!
(Imetafsiriwa)

Katika siku kumi za mwanzo za Dhul Hijjah, Uislamu umetutaka kutangaza waziwazi Takbir, Tahlil na Tahmid katika maeneo ya umma. Hivyo basi, Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon ilitoa wito wa msafara wa gari yakiwa na Rayat (bendera) ya "La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah." Taratibu muhimu zilifuatwa kumjulisha Gavana wa Beirut na mkuu wake wa polisi. Baada ya msafara huo kuanza saa 6:00 jioni ya tarehe 6 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 24 Juni 2023 M, watu walionyesha furaha yao, na huku msafara huo ukizunguka theluthi mbili ya njia yake bila tatizo lolote, watu pembeni mwa barabara walikuwa wakitukuza, wakitazama, na kuonyesha furaha yao nyuso mwao.

Licha ya hayo yote, Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Lebanon jijini Beirut ilichukua hatua kinyume cha sheria na bila ya msingi wowote wa kisheria kwa kusimamisha baadhi ya magari yaliyoshiriki na kuyazuia yasiendelea. Walitaka hata kuondolewa na kufichwa kwa bendera za Kiislamu! Walitaka kuutawanya msafara huo, wakijichukulia wao ndio wenye mamlaka ya usalama zaidi ya gavana na mkuu wa polisi! Mawasiliano yalikuwa wazi kutoka kwa uongozi wa Ujasusi kwenda kwa wanachama wake walioko uwanjani kuharakisha kusitisha msafara huo kwa sababu waliona kuwa ni mandhari ya bendera za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika mojawapo ya miji ya Uislamu, ambayo baadhi yao wanataka kuifuta kitambulisho chake halisi.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir walihakikisha hawafanyi mzozo wowote. Makusudio ya maandamano haya ni kueneza hali ya utulivu kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anapaswa kukumbukwa zaidi, na kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu iliyo juu ya amri zote.

[وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَاناً فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ * الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ]

“Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi hamkhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, kama nyinyi mnajua?” [Al-An'am:81]

Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi kuliko mamlaka yoyote fisadi na udhibiti wa vyombo vya usalama.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu