Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  17 Shawwal 1443 Na: 1443 / 64
M.  Jumanne, 17 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Iwe ni Mpango wa London au Maandamano ya Islamabad, Chini ya Demokrasia, Watu Wanachunwa Ngozi wakiwa Hai

(Imetafsiriwa)

Wachambuzi wa habari wanajaribu kuwashirikisha watu katika mjadala kuhusu Mpango wa London na Maandamano ya Islamabad, kana kwamba kuna matumaini yoyote kwamba mipango hii na ujanja huu wa kisiasa yatasuluhisha matatizo ya watu. Awe Maryam Aurangzeb, Shahbaz Gul au Rana Sanaullah, maneno yao ni kama ya Nadr bin Harith, kiongozi wa Maquraishi, ambaye alisoma hadithi za Rustam na Asfandyar, ili kuwapotosha watu kutoka kwenye ujumbe safi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wachambuzi wa habari hata hawaibui maswali halisi. Je, bei za umeme, mafuta na gesi hazitapanda baada ya Mpango wa London? Je, masharti ya IMF yatakataliwa? Je, Bilawal Bhutto atakataa kwenda Marekani kuchukua maagizo mapya? Je, Rupia haitaendelea kuporomoka mbele ya dolari? Je, mzigo utaisha na umeme kuanza kuwa nafuu? Je, ruzuku zitadumishwa? Je, suala la Kashmir halitazikwa? Hapana, bila shaka sivyo. Midomo hii inawashughulisha watu katika mijadala duni kati ya serikali na upinzani, ili matatizo halisi ya wananchi yasiweze kujadiliwa.

Je, Imran Khan anaweza kudai leo kwamba hata akiunda serikali endapo kutakuwa na uchaguzi wa mara moja, hatakwenda IMF? Je, Imran Khan yuko tayari kudai hadharani kwamba atafunga njia ya anga ya mawasiliano, "Boulevard," iliyowekwa wazi kwa ajili ya Amerika? Je, Imran Khan yuko tayari kuwaahidi wananchi, hadharani, kwamba hataitisha tena ‘vifurushi’ vya mkopo wa riba? Je, Imran anaahidi kuhamasisha majeshi yetu mashujaa na yenye uwezo kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir? Bila shaka hapana. Mithili ya kundi lake pinzani, la hasha. Makundi hayo yanajihusisha na mivutano duni ya juu ya ni nani atapata udhibiti wa utawala na rasilimali za Pakistan. Makundi haya mawili sio machaguo yanayostahiki; wanawachuna tu watu ngozi wakiwa hai!!!

Enyi Waislamu wa Pakistan! Yakataeni makundi haya mawili kwa sababu demokrasia si chochote ila ni utumwa, udhalilishaji na ukoloni. Ni Khilafah ambayo kusimama kwake kunaanza na Pakistan inshaAllah, ndio itakayoziunganisha dola zenye nishati nyingi za Waislamu kuwa dola moja, hivyo Khilafah haitalazimika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa. Kwa mujibu wa Uislamu mafuta, gesi na umeme ni mali ya umma, hivyo hutozwa kwa bei inayohalisi au kwa bei ya gharama tu. Khilafah ndiyo itakayotoa afueni ya moja kwa moja kwa watu na wafanyabiashara, kwa kuondoa kodi zote zilizopo za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zisizo za Kisheria. Haitawatoza masikini na wenye deni, huku ikikusanya mapato ya Kishariah kutoka kwa wenye uwezo wa kifedha, kama vile Kharaaj kutoka kwa wamiliki wa ardhi ya kilimo na Zakah kutoka kwa wenye viwanda na biashara ya juu ya Nisaab. Khilafah itaondoa malipo ya riba ya trilioni tatu, na kutoa fedha za kuwachunga watu. Khilafah italipa kiasi kikubwa cha deni kutoka kwenye utajiri wa ziada wa watawala wafisadi, ambao walichukua mikopo hii wakati wa utawala wao, na haitaweka mzigo wa kulipa madeni haya haramu kwa watu. Khilafah ndiyo itakayopigania ukombozi wa Kashmir na Kibla cha Kwanza, ili Modi na wafuasi wake, wanaowadhulumu kaka na dada zetu, wakamatwe, huku umbile la Kiyahudi litatokomezwa. Enyi Waislamu! Ni Khilafah pekee, ambapo Ummah utaibuka kwenye jukwaa la dunia, katika kutawala. Demokrasia si chochote zaidi ya mivutano duni kati ya makundi yenye nguvu. Kwa hiyo jitokezeni na muwatake jamaa zenu katika jeshi la Pakistan waipe Nusra Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu