Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Muharram 1444 Na: 1444 / 04
M.  Ijumaa, 26 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uongozi wa Kisiasa na Kijeshi wa Pakistan Umefungwa ndani ya Mapambano Duni ya Kung’ang’ania Utawala, Huku Maeneo Makubwa ya Nchi Yakikumbwa na Mafuriko

(Imetafsiriwa)

Maeneo makubwa ya Pakistan yanakumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika. Kulingana na NDMA, tangu Juni 12, watu 903 wamekufa, watu 1293 wamejeruhiwa, karibu nyumba 300,000 zimeharibiwa kwa kiasi na nyumba 200,000 zimeharibiwa kabisa. Mafuriko yanasomba watoto wa wahasiriwa. Watu hawana malazi wala chakula. Maeneo mengi yamekatwa. ilhali, serikali haionekani.

Mafuriko ni hali ambayo dola inapaswa kuhamasishwa, mchana na usiku, bila kuacha juhudi zozote za kutoa misaada. Hata hivyo, msimamo wa watawala ni kana kwamba msiba huu haujawapata wanadamu halisi, bali ni sinema tu ya maafa, inayotoa hisia za muda mfupi na fursa ya kutoa maoni yaliyopita. Hamu halisi kwa uongozi wa kisiasa na kijeshi ni mapambano yao duni ya kung’ang’ania madaraka na idhini ya kifurushi cha uokozi cha IMF, ili kuizamisha nchi katika mikopo yenye riba zaidi na masharti kandamizi.

Uongozi wa sasa wa Pakistan unakanyaga haki za watu, hata huku ukidai kuwa mchungaji wao, wakati wa mafuriko. Haijui hata hali halisi ya watu, ambao inadai kupata. Inawaacha watu kama mayatima, kuteseka na kufa peke yao. Siasa chini ya Demokrasia sio kutumikia wengine, ni kujisaidia kwa utajiri wa nchi. Tuliona msimamo huo wakati wa mafuriko ya Sindh na Karachi hapo awali. Kwa kweli, tumeona msimamo huo mara kadhaa hapo awali wakati wa dharura za kitaifa, kwa miongo kadhaa.

Iwe ni mafuriko yanayodumaza au mfumko wa bei unaovunja mgongo, iwe ni ulinzi wa heshima ya Mtume Mtukufu (saw) au ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, iwe ni huduma za afya na elimu au sheria na utulivu, iwe bili za umeme au bei za mafuta ya petroli, Demokrasia imetuangusha kabisa. Hata leo, ni Muislamu wa kawaida wa Pakistan ndiye anayejitokeza kuwasaidia ndugu na dada. Ama kuhusu watawala wa Pakistan, ima wanashughulika na kuiomba IMF au kupiga tarumbeta zao juu ya Jeshi la Pakistan kuwa usalama wa kina kwenye kombe la dunia la kandanda, kana kwamba lengo lake pekee ni kupata dolari.

Ni Khilafah kwa Njia ya Utume pekee ndiyo inayoweza kuwa mchungaji wetu, wakati wa mafuriko au shida yoyote tunayokabiliana nayo. Khalifah sio tu kwamba anatabikisha Uislamu kikamilifu pekee, pia huzingatia ustawi wa watu kama wajibu wake, kwa kuogopa kuhisabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Khalifah Muongofu wa pili, Umar Ibn Khattab (ra), alisema:

 "لَوْ مَاتَتْ شَاةٌ عَلَى شَطِّ الْفُرَاتِ ضَائِعَةً لَظَنَنْتُ أَنَّ اللهَ تَعَالَى سَائِلِي عَنْهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ"

Lau kondoo aliyepotea atakufa katika kingo za mto Furaat, Naamini Mwenyezi Mungu (swt) ataniuliza kumhusu Siku ya Kiyama.” (Chanzo: Kitabu cha Abu Naeem, ‘Haliya Awaliya’).

Kupitia upuuzaji wake mkubwa wakati wa mafuriko, ubaya wa Demokrasia sasa uko wazi kwa wote. Sasa inafaa tu kuzikwa. Kwa hivyo, enyi maafisa wanyofu wa Jeshi la Pakistan! Jitokezeni mufanye mabadiliko. Uhurumieni Ummah wetu mtukufu wa Kiislamu. Tumieni uwezo na nguvu zenu, alizokupeni Mwenyezi Mungu (swt)  na atakuhisabuni kwazo, ili kuleta afueni kwa Waislamu watukufu wa Pakistan. Jitokezeni muipe Nussrah yenu Hizb ut Tahrir, sasa, kusimamisha Khilafah mara moja, itakayohamasisha ndani ya dakika na saa chache, kwa nguvu kamili na umakini, kuwapa misaada wahanga wa mafuriko.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu