Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Safar 1444 Na: 1444 / 07
M.  Jumamosi, 17 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili jinsia ni Shambulizi dhidi ya Uislamu na Maadili ya Familia. Watawala wa Pakistan, Ni Watumwa wa Magharibi, Wanaotafuta Kuangamiza Kizazi Chetu Kipya

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 5 Septemba 2022, Seneta wa Pakistan Mushtaq Ahmad aliwasilisha mswada wa marekebisho katika Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili Jinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Haki za Kibinadamu. Katika mkutano huo, Seneta Mushtaq Ahmad, alisema kuwa, "‘Transgender’ ni neno la Kimarekani, halina nafasi katika Uislamu, na sheria kuhusu jamii ya watu waliobadili jinsia ni kinyume na Qur'an na Sunnah na itapigia debe ushoga." Tunataka kubainisha uhalisia ili mdahalo uweze kuhitimishwa kwa namna inayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt).

Magharibi imejenga hadhara yake juu ya fahamu kwamba mwanadamu yuko huru kutokana na mwongozo wa kiwahyi, kipengele kimojawapo ni uhuru wa kibinafsi. Fahamu ya ukombozi wa wanawake imehitimisha kuwa dori ya mwanamke katika jamii lazima iamuliwe na uhalisia wake wa kibaolojia. Katika siku za hivi karibuni, Magharibi imehitimisha kuwa jinsia ya mwanamke haipaswi kuamuliwa na uhalisia wake wa kibaolojia. Mwanamke anaweza kuamua kujitambulisha kama mwanamke kwa kuzingatia hiari yake mwenyewe na mtazamo wa kibinafsi. Jamii haiwezi kulazimisha kitambulisho hiki, kwani hilo ni kinyume na fahamu ya msingi ya uhuru. Fahamu hiyo hiyo pia iliwasilishwa na Magharibi kuhusu wanaume. Kwa hivyo fahamu ya Kimagharibi ya uhuru inamruhusu mtu kuamua, kwa hiari yake mwenyewe, awe mwanamume, au mwanamke, au muunganiko wa mwanamume na mwanamke au la au kitu chengine. Ni fahamu hii ndio iliyoibua fahamu ya mtu aliyebadili jinsia.

Watawala wa Waislamu, ambao wanashindana wao kwa wao katika utumwa wa Magharibi, walitunga Sheria ya Kuwalinda Wanaobadili Jinsia kwa kuzingatia fahamu hii angamivu na sasa wanafanya marekebisho. Sheria hiyo inasisitiza kwamba kitambulisho cha kijinsia hakiamuliwi na kuzaliwa bali huathiriwa na mambo ya kisaikolojia na kijamii, yanayobadilika chini ya ushawishi wa mambo haya. Sheria hii inaamua kwamba mtazamo wa mtu binafsi kwamba yeye ni mwanamke ni hisia ambayo lazima si tu kuheshimiwa, ni lazima ipewe ulinzi wa kisheria. Ufafanuzi wa mtu aliyebadili jinsia, katika sheria hii, unajumuisha mtu yeyote ambaye ana mtazamo tofauti wa jinsia tofauti na kitambulisho cha kijinsia alichopewa wakati wa kuzaliwa, kupitia uhalisia wa kibaolojia. Yaani, mtu yeyote kisheria anaweza kutabanni kuwa mwanamume au mwanamke au mchanganyiko wa mwanamume na mwanamke, au kitambulisho chengine chochote mbali na hao, kupitia kuelezea mtazamo wao binafsi wakati wowote. Katika muktadha huu, hakuna uchunguzi wa kimatibabu au wa kisaikolojia wa mtu huyu unaoweza kufanywa.

Chini ya Sheria ya Ulinzi wa Watu waliobadili jinsia, pindi mwanamume anapojieleza na kujifanya kuwa mwanamke kisheria, atapata haki zote za wanawake, kama vile kupata vyumba vya wanawake, matumizi ya vyoo vya wanawake, kujiunga na shule ya wanawake na haki ya kuolewa na mwanamume. Vile vile mwanamke anapojitambua kuwa ni mwanamume kisheria, sheria za mirathi za wanaume zitatumika kwake katika masuala ya mirathi na anaweza kumuoa mwanamke yeyote. Kuitekeleza sheria hii ni uthibitisho kwamba watawala wetu wamevuka mipaka yote katika utumwa wa Magharibi na wanafanya kazi kwa bidii katika kujaribu kuwatenga Waislamu na dini yao. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّهِ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا]

“Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.” [Surah An-Nisaa 4:119]. Imesimuliwa katika Tirmidhi kwamba, «لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ الْمُتَشَبِّهَاتِ بِالرِّجَالِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْمُتَشَبِّهِينَ بِالنِّسَاءِ مِنَ الرِّجَالِ»Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume na wanaume wenye kujifananisha na wanawake.”


Enyi Waislamu wa Pakistan! Sheria ya Ulinzi wa Wanaobadili jinsia ni kuhukumu kinyume  na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Ni Taghut ambayo inapaswa kukataliwa na kukufuriwa. Sheria hii itajenga maadili yetu ya kijamii kwa msingi haramu, na kuangamiza muundo wetu wa familia. Kwa kutoa wanya wa kisheria kwa mwanamume kuoa mwanamume na mwanamke kuoa mwanamke, sheria hii inahalalisha dhambi, ambalo kwalo watu wa Lut (as) waliadhibiwa. Baada ya kujua ukweli wa sheria hii chukizi na haramu, ni wajibu wetu kuikataa sheria hii, kama ambavyo ni wajibu wetu kupambana kwa ajili ya utabikishaji wa Dini yetu kwa ukamilifu wake.

Kinyume na vifungu vya Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili jinsia, kuna jinsia mbili tu za kisheria katika Uislamu, wanaume au wanawake. Jinsia huamuliwa kwa misingi ya kibaolojia. Uchukuaji upya wa jinsia kwa msingi ya mtazamo wa kibinafsi, bila kujali baolojia, hauruhusiwi. Endapo kuna shaka yoyote juu ya jinsia ya mtu, basi ikiwa sifa za kike zinatawala ndani yake kutoka kwa upande wa kibaolojia, atachukuliwa kuwa mwanamke, na ikiwa sifa za kibaolojia za kiume zitatawala, atachukuliwa kuwa mwanamume. Na ikiwa, pamoja na haya yote, kuna nafasi ya shaka, wataalamu wa matibabu watafanya uchunguzi wa kisaikolojia na wa kimatibabu wa watu wanaohusika, kuamua ikiwa mtu huyo ni mwanamume au mwanamke.

Khilafah kwa Njia ya Utume itatabikisha Dini, iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), ambayo kwayo Khilafah itaondoa maovu yaliyoletwa na hadhara ya Kimagharibi. Pia itawatoa watu wote katika utiifu wa mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt), kulingania utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kuuonyesha ulimwengu njia ya uongofu.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya Qur'an Tukufu,

[اتَّبِعُوا مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ قَلِيلاً مَا تَذَكَّرُونَ]

“Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka.” [Surah Al-A’raf, 7:3].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu