Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 25 Rabi' I 1444 | Na: 1444 / 13 |
M. Ijumaa, 21 Oktoba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uamuzi wa Kesi ya Mauaji ya Shahzaib ni Uthibitisho wa Kushindwa kwa Idara ya Mahakama ya Pakistan
Idara ya Mahakama ya Shariah ya Khilafah ndio Suluhisho Pekee
(Imetafsiriwa)
Mnamo Oktoba 18, benchi la majaji watatu wa Mahakama ya Upeo ilimwondolea mashtaka mshtakiwa Shahrukh Jatoi, kwa mauaji katika kesi maarufu ya mauaji ya Shahzeb. Ingawa hukumu hii ilizua shutuma za umma, haikuwa isiyotarajiwa. Katika makumi ya hukumu za awali, zikiwemo kesi za Nazim Jokhi, Raymond Davis, Abdul Majeed Achakzai, mahakama zimewapa wakoloni na watu wengine wenye nguvu njia ya kutorokea kupitia mianya mbalimbali ya kisheria. Kesi ya mauaji ya Shahzeb imethibitisha kwa mara nyengine tena kwamba mfumo umeporomoka. Dola ya Pakistan imekuwa ni dola ya kuwahudumia mabwenyenye wachache, ambapo mtu wa kawaida hana hisa. Wakati umewadia sasa wa kubadilisha mfumo ulioporomoka kwa kuweka Khilafah, iliyojengwa juu ya msingi imara wa Uislamu!
Katika kesi ya mauaji ya Shahzeb, vyombo vyote vya dola vilihusika katika kumuokoa mshtakiwa, katika kila hatua. Kuzuia usajili wa kesi, kutomkamata mshtakiwa, kumhamisha nje ya nchi, kugeuza gereza kuwa hoteli ya nyota tano, kutoa huduma za kifahari hospitalini, kulazimisha ridhaa na kisha, kwa msingi wa vifungu vya ugaidi, mwanzoni walikataa idhini ila tu baadaye kukubali, kupitia Mahakama ya Upeo. Ni wazi kwamba kila ngazi, idara ya mahakama ya Pakistan imeporomoka. Mfumo wa rufaa wa mahakama wa hatua tatu huwapa watu wenye nguvu wakati, nafasi na urahisi wa kuhujumu haki. Kupitia mfumo wa rufaa, hukumu za kifo hubadilishwa kwanza na kuwa kifungo cha maisha, kabla ya kuondolewa mashtaka, kama ilivyotokea katika kesi hii. Kipindi kirefu cha miaka kumi hutoa fursa kwa kipote cha mabwenyenye kuwakatisha tamaa warithi kutokana na kupata haki, na kuwalazimisha kuridhia, kupitia matumizi mabaya ya sheria ya Kiislamu ya Diyah (Kulipiza kisasi). Babake Shahzeb, DSP Aurangzeb, alikufa akimkumbuka mwanawe.
Kama kungekuwa na mfumo wa Uislamu leo, katika mahakama ya Qadi Aam, Shah Rukh Jatoi angelipiza kisasi inapopatikana hatia, ndani ya vikao vichache. Warithi ambao hawakuridhia, wasingeshinikizwa. Hawangelazimishwa kutoa idhini kwa sababu ya kufadhaika. Idatra ya Mahakama ya Uingereza ya Demokrasia haiwezi kamwe kutoa haki, kwa sababu, katika mfumo huu, watu wenye nguvu ndio hutunga sheria kwa maslahi yao wenyewe, kupitia kuliteka nyara bunge.
Hata hivyo, Khalifa wa kwanza wa Waislamu, Abu Bakr Siddiq, alianza Khilafah kwa kauli hii:
ألا إن أقواکم عندي الضعیف حتی آخذ الحق له وأضعفکم عندي القوي حتی آخذ الحق منه
“Jueni hakika wenye nguvu kwenu kwangu mimi ni wanyonge mpaka niichukue haki kutoka kwao, na wanyonge kwenu kwangu ni wenye nguvu, mpaka niwarudishie haki yao.” Al-Badaya Wal-Nahiya, Tabari, Ibn Hisham)
Enyi Maafisa Wanyofu wa Kijeshi katika Vikosi vya Wanajeshi vya Pakistan! Iwe ni mfumo wa serikali ya kidemokrasia ya kisekula ya Pakistan, mfumo wa uchumi wa kirasilimali, idara ya mahakama ya Uingereza inayoegemea sheria za kawaida au mfumo wa elimu ya kisekula, kila kitu kimeporomoka. Ingawa mfumo wa kijamii umeendelea kuwepo hai kwa kiasi fulani kutokana na maadili ya Kiislamu ndani ya Waislamu, huo nayo pia unakabiliwa na tishio kutokana na sera za kiliberali. Sera ya kigeni iliyojengwa juu ya utumwa wa mfumo wa kimataifa imeigeuza Pakistan kuwa dola iliyofeli. Haya yote yalitokea licha ya ukweli kwamba sisi tuna nguvu ya nyuklia, tulio na idadi ya vijana ya milioni 220 na rasilimali nyingi, tuliobarikiwa na Dini ya Uislamu. Hivyo hamasikeni na uanzishe Khilafah kuanzia Pakistan. Kataeni mfumo wa dola ya kitaifa na utumwa wa mfumo wa kimataifa, unaofanywa na Magharibi. Serikali na vyama vya upinzani vya kisiasa havina suluhu ya matatizo ya Pakistan. Ni Hizb ut Tahrir pekee iliyoko mbele yenu, ndio imejitayarisha kikamilifu na yenye uwezo wa kuanzisha mabadiliko ya kimapinduzi, ndani ya masaa machache. Basi jitokezeni na mtoe Nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«وَمَنْ مَاتَ وَلَیْسَ فِی عُنُقِهِ بَیْعَةٌ مَاتَ مِیتَةً جَاهِلِیَّةً»
“Na atakaye kufa na hana katika shingo yake ahadi ya utiifu (kwa Khaleyfah), basi huyo amekufa kifo cha Kijahiliya.” (Muslim)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |