Alhamisi, 17 Safar 1446 | 2024/08/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 14
M.  Jumatatu, 24 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuondolewa kutoka kwa Orodha ya Kijivu ya FATF Hakulingani na Mapinduzi ya Kiuchumi. Kuna Maanisha tu kuwa Mshiko wa Marekani kwa Pakistan Umeongezeka

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 21 Oktoba 2022, FATF ilitangaza rasmi kuondolewa kwa Pakistan kutoka kwenye orodha ya kijivu. Watawala wa Pakistan wanasherehekea, kana kwamba wametekeleza wajibu mkubwa wa Shariah. Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa nchi, pamoja na upinzani, wote wametekeleza nukta 34 za FATF, kana kwamba ni maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hakika, nukta hizi za vitendo zinawakilisha kwa uwazi kabisa usaliti kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), na waumini. Wanavunja mgongo wa Jihad-e-Kashmir na kunyonga kila aina ya usaidizi wa kifedha kwa ajili yake.

Vibaraka hawa wa Marekani waliwasilisha madai ya FATF kana kwamba ndio kizuizi pekee cha mapinduzi ya kiuchumi nchini Pakistan. Wanawasilisha kuondolewa kutoka kwenye orodha ya kijivu, kana kwamba tuko kwenye ukingo wa mapinduzi ya kiuchumi, kabla ya Juni 2018, wakati Pakistan haikuwa kwenye orodha ya kijivu ya FATF. Iwe ni hadhi ya GSP Plus kutoka Muungano wa Ulaya au kifurushi cha IMF, daima wanasema kwamba Pakistan itastawi kiuchumi. Hata hivyo, si mipango 22 ya IMF, wala kuondolewa kutoka kwenye orodha ya kijivu ya FATF, wala mradi wa CPEC, wala mikopo ya wakoloni wa China, zilizowahi kamwe kubadilisha mchezo.

Badala yake, hali yetu ya kiuchumi imekuwa mbaya daima. Wakati kulipokuwa na serikali ya Congress nchini India, Jihad huko Kashmir ilikuwa kwa maslahi ya kimkakati ya Amerika, kutawala India. Kwa hivyo Washington ilifunga macho yake juu ya kila aina ya msaada wa Pakistan kwa Jihad hii. Hata hivyo, wakati serikali ya BJP inayounga mkono Marekani ilipoingia madarakani nchini India, Marekani ilitangaza Jihad katika Kashmir kuwa ‘ugaidi.’ Ilidai kwamba uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan uyapige marufuku mashirika ya Jihad ya Kashmir na kukomesha uungwaji mkono wote. Hivyo Musharraf alipiga marufuku mashirika ya Jihad ya Kashmir. Kwa kutekeleza masharti ya FATF, usaidizi wowote wa kifedha kwa Jihad huko Kashmir umefanywa kutowezekana. Pia, utekelezaji wa FATF umeharibu uchumi wetu hatua kwa hatua. Imefanya shughuli za kifedha za kila siku kuwa ngumu sana kwa mtu wa kawaida.

Chini ya pazia la kusitisha ‘ufadhili haramu,’ FATF hufuatilia mtiririko wa fedha katika nchi zilizoteuliwa. Inahakikisha kwamba fedha hazitumiwi dhidi ya maslahi ya Magharibi. Ni suala la muda tu kabla ya FATF kuinasa Pakistan, katika mpango wake wa kukabiliana na kuenea kwa silaha za maangamizi makubwa. Kisha inaweza kuitaka Pakistan ifungue akaunti zake za siri za benki, kwa ajili ya kudumisha na kulinda mpango wa silaha za nyuklia uliopatikana kwa bidii kubwa.

Mataifa ya Magharibi, na taasisi zao za kifedha, zenyewe ni chanzo kikuu cha shughuli haramu za kifedha. Wameficha mali zetu nje ya nchi, baada ya kuporwa na ukoloni wa moja kwa moja na watawala vibaraka. Kwa hivyo akili za wahalifu wa Kimagharibi hulazimisha nchi zinazoendelea kuzingatia viwango, ambavyo wao wenyewe huvipuuza. Isitoshe, maadui zetu wanaendelea kufadhili miradi ya ugaidi kinyume na sheria dhidi yetu.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Majeshi yao! Kwa kutimiza matakwa ya taasisi za kikoloni, kama vile IMF na FATF, chini ya mfumo wa kimataifa ulioanzishwa na Amerika, ubwana wa kiuchumi, kifedha, kigeni na wa ndani wa Pakistan unaondolewa. Kufuatia maagizo haya, nchi yenye idadi ya watu milioni 220, ambayo ina jeshi la sita kwa ukubwa zaidi duniani na silaha za nyuklia, sasa kivitendo inabeba hadhi ya Nepal au Bhutan. Uongozi wetu wa kisiasa na kijeshi ni watumwa wa Marekani, ingawa Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya kuhusu madhara ya kufuata amri za makafiri. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوَاْ إِن تُطِيعُواْ الَّذِينَ كَفَرُواْ يَرُدُّوكُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُواْ خَاسِرِينَ)

“Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.” [Surah Aali-Imran, 3:149]. Kwa hivyo wakati umefika wa kukomesha udhalilifu. Simamisheni Khilafah kwa Njia ya Utume. Ndio pekee itakayopinga mfumo wa kilimwengu wa Marekani na vyombo vyake, taasisi za kikoloni, huku ikikusanya majeshi kwa ajili ya Jihad-i-Kashmir na Ufunguzi wa India.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu