Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Rabi' II 1444 Na: 1444 / 15
M.  Ijumaa, 04 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chaguzi, Maandamano Marefu na Kulaani ndani ya Demokrasia Kamwe Hayataleta Mabadiliko ya Kweli! Mapinduzi ya Halisi Yatakuja wakati Demokrasia itakapong'olewa na Khilafah Kusimamishwa

(Imetafsiriwa)

Ni wazi sasa kwamba kushiriki katika Demokrasia, siasa za kidemokrasia, maandamano marefu na kulaani ndani ya Demokrasia kamwe hakutaleta mabadiliko yoyote ya kweli. Uongozi wa sasa wa kisiasa na kijeshi unahakikisha kwamba washiriki wote ndani ya Demokrasia wanafuata kanuni na sheria zao. Wanafanya kazi kuzuia mabadiliko ya kweli, kuhifadhi tu maslahi yao, pamoja na yale ya mabwana zao wa kikoloni. Hakuna mabadiliko yatakayokuja kupitia siasa za kidemokrasia, na ushiriki katika mfumo wa kidemokrasia kupitia maandamano marefu, kulaani na chaguzi. Kwa hakika, vitendo hivyo vya kisiasa, ndani ya mfumo wa sasa vinasaidia tu kuongeza uhai wa mfumo huu. Sio theluthi mbili ya wingi wa kura, wala kuhama kutoka kwa mfumo wa utawala wa bunge hadi wa urais, kutawahi kamwe kuleta mabadiliko yoyote ya kweli. Shina la matatizo yetu ni Demokrasia yenyewe, bila kujali ni chama gani cha kisiasa kinachotawala kwayo. Maadamu Demokrasia inabakia, shida zetu zitabaki na kuwa mbaya zaidi.

Demokrasia daima huzusha mizozo miongoni mwa kipote kinacho tawala, kama tunavyoona sasa. Mapigano haya ni kati ya vyama vya kisiasa, au kati ya vyama vya kisiasa na mahakama, au kati ya mahakama na jeshi, au kati ya jeshi na vyama vya kisiasa. Mapigano hayo yote huishia tu katika mpango mpya wa kugawanya mamlaka, ambapo kipote hicho ndicho hufaidika kwa gharama yetu. Demokrasia kamwe haijawahi kutoa manufaa yoyote kwetu. Daima imepoteza tu nguvu za wafanyikazi wanyoofu wa kisiasa.

Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ambayo kivitendo itafikia mabadiliko ya kweli tunayohitaji. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayotutawala kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Ni Khilafah ndiyo itakayounganisha Ulimwengu mzima wa Kiislamu kama dola moja, yenye nguvu na yenye ufanisi. Khilafah ndiyo itakayoifurusha Marekani na taasisi zake angamivu za kimataifa kutoka katika ardhi zetu. Ni Khilafah ndiyo itakayozikomboa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, kama vile Kashmir na Palestina, kupitia kuhamasisha majeshi yetu katika Jihad.

Sunnah ya Mtume inabainisha kwamba njia pekee ya mabadiliko ya kweli ni kutafuta Nusrah kutoka kwa watu wenye nguvu, na silaha za kijeshi, kwa ajili ya kutawala kwa Uislamu. Mtume (saw) aliitafuta Nusrah kutoka kwa makamanda wa kijeshi, wakiwemo wale wa kabila la Taif, Banu Thaqif. Ibn Ishaq amesimulia, فَخَرَجَ رَسُولُ اللّهِ ﷺ إلَى الطّائِفِ، يَلْتَمِسُ النّصْرَةَ مِنْ ثَقِيفٍ، وَالْمَنَعَةَ بِهِمْ مِنْ قَوْمِهِ وَرَجَاءَ أَنْ يَقْبَلُوا مِنْهُ مَا جَاءَهُمْ بِهِ مِنْ اللّهِ عَزّ وَجَلّ “Mtume (saw) akatoka kwenda Taif, ili kutafuta Nusrah kutoka kwa Thaqif na ulinzi wao kutokana na watu wake (mjini Makkah), akitaraji watamkubalia aliyowajia nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).” Kwa hiyo, ni lazima tuyatake majeshi ya Pakistan yatoe Nusrah yao kwa ajili ya kutawala kwa Uislamu, sasa.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Komesheni mzunguko huu wa fujo wa mapigano ya kipote kati ya vyama vya kisiasa vya Pakistan, jeshi na idara ya mahakama. Kipote hiki kinajali tu uwezo mamlaka, nyadhifa, urefushaji muhula na marupurupu. Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), waokoeni watu wetu kutokana na masaibu zaidi, ing'oeni Demokrasia na toeni Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal 8: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu