Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Muharram 1442 Na: 1442/12
M.  Jumatano, 16 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sudan na Ushahidi wa Uwongo katika Makubaliano ya Khiyana na Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Jana, Jumanne, 15/09/2020, Amina Aqareb; Msimamizi wa Mambo ya Ubalozi wa Sudan jijini Washington, na Naibu Balozi alishuhudia kutiwa saini kwa Imarati na Bahrain pamoja na umbile la Kiyahudi Mkataba wa Khiyana Kubwa kwa Palestina; Ardhi ya Isra na Miraj ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na balozi wa Sudan jijini washington, Nurdin Sati, akataja hatua hiyo, katika taarifa kwa gazeti la Al-Tayyar lililochapishwa siku ya Jumatano tarehe 16/09/2020 kuwa: "Sio suala la kubariki au kutobariki makubaliano" Na akaelezea matumaini yake kuwa hatua hii itasababisha amani ya kweli katika eneo hilo!!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunalaani vikali ushahidi huu wa uwongo kutoka kwa wawakilishi wa Sudan nchini Amerika, dola ya khiyana, na tunathibitisha ukweli ufuatao:

Kwanza: Kile ambacho vidola vya Imarati na Bahrain vimefanya; bidhaa mbili za ukoloni wa Kiingereza, katika kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, ni jinai na khiyana kubwa kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw) na waumini wa kweli mpaka Siku ya Kiyama.

Pili: Ikiwa ushiriki wa Sudan sio jambo la kubariki, kama balozi anavyodai, basi ni katika mlango wa ushahidi wa uwongo ambao tumetaja, na muumini wa kweli hasemi uwongo. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَاماً]

“Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao.” [Al-Furqan: 72].

Tatu: Hakika kauli ya Balozi Sati kwamba (anatumai hatua hii itasababisha amani ya kweli katika eneo hilo ...), basi (bwana) balozi na ajue kuwa umbile la Kiyahudi ni mnyakuzi wa ardhi ya Kiislamu; Bali wa Ardhi Iliyobarikiwa ambayo ndani yake mna Msikiti wa Al-Aqsa; kibla cha kwanza katika vibla viwili, na wa tatu kwa utukufu katika Misikiti Mitakatifu Mitatu! Ni amani gani inayotarajiwa kwa wale wanaochafua na kukiuka matakatifu, na kumwaga damu ya watoto, wazee na wanawake, bali uadui wao umepanuka hadi kwa miti na mawe?!

Nne: Namna watawala wa Rawaybidha watakavyo sawazisha mahusiano, au vibaraka kubariki usawazishaji huo, hakika Palestina Ardhi Iliyobarikiwa, Ardhi Takatifu, Ardhi ya Isra na Mi'raj, iko ndani ya nyoyo za Waislamu, hata wakitahiniwa kwa watawala wanaowatii makafiri wakoloni badala ya kumtii Bwana wa Walimwengu wote. Palestina itarudi kwa Waislamu, na Msikiti wa Al-Aqsa utasafishwa kutokana na najisi ya Mayahudi siku itakayoshuhudiwa, itakayojaa kelele za takbira kutoka kwa vikosi vya majeshi ya Waislamu, wakati watakapopigana na Mayahudi wanyakuzi wa Ardhi Iliyobarikiwa. Ni ahadi isiyo ya uwongo kutoka kwa Al-Sadiq Al-Masduq (mkweli na mwaminifu) (saw):

«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ، حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ»

 “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na mtawauwa, hadi jiwe litasema: Ewe Muislamu Yahudi huyu hapa basi njoo umuue.” (Imepokewa na Muslim).

Na tuna utulivu juu ya ahadi hii, ambayo itatimizwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), mikononi mwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo itahukumu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), na kuunganisha majeshi ya Waislamu, yenye kuitetemesha ardhi chini ya miguu ya umbile la Kiyahudi na kuliondoa kutoka juu ya ardhi safi, na kuirudisha Palestina yote katika makaazi ya Uislamu.

Basi njooni, enyi Waislamu, mufanyeni kazi na Hizb ut-Tahrir; kiongozi asiyewadanganya watu wake mpaka tupate ushindi wa Mwenyezi Mungu kupitia Khilafah na tamkini katika ardhi, na bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ya kusimama Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka katika Ardhi Iliyobarikiwa.

 [ذَلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ]

“Hiyo ni ahadi isiyo kuwa ya uwongo.” [Hud: 65]

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu