Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  2 Safar 1442 Na: 1442/13
M.  Jumamosi, 19 Septemba 2020

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

(وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri* Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 155-156]
(Imetafsiriwa)

Kwa nyoyo zilizojaa imani na kuridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu, na kwa macho yenye machozi, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan inamuomboleza mwenye kusamesewa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu:

Yusuf Hamid Is’haq

Mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa El Obeid; ambaye iliubeba ulinganizi huu licha ya ugonjwa wa kisukari, ambao alisababisha kukatwa kwa sehemu ya mguu wake, na pia kusababisha nuru ya macho yake kupungua, na haya yote hayakumvunja moyo kuubeba ulinganizi huu, na kuipenyeza popote alipokuwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aliye Mkarimu zaidi, Bwana wa Kiti cha Enzi, amfunike kwa upana wa rehema yake, amsamehe, ayakirimu mashukio yake, na aupanue mlango wake, na aibariki familia yake, na atushushie na ndugu zake wabebaji ulinganizi, na familia yake na jamaa zake, subira na faraja njema.

Hakika moyo unahuzunika, na hakika macho yatatokwa na machozi, na hakika sisi kwa kufarikiana nawe, ewe Yusuf, ni wenye huzuni, na hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mola wetu:

(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu