Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Jumada I 1442 Na: 1442/08
M.  Alhamisi, 07 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuwasilisha Elimu ya Ngono katika Kongamano la Kielimu Kunajiri katika Muktadha wa Kisiasa wa Serikali Ambayo Imetangaza Vita Vyake juu ya Hukmu Zilizobakia za Uislamu na Kuhalalisha Maadili ya Hadhara ya Magharibi
(Imetafsiriwa)

Katika Kongamano la Mtaala wa Elimu wa hatua za shule za kati na za upili, ambao ulianza kazi yake tarehe 05/01/2021, chini ya kauli mbiu: "Kwa ajili ya mtaala unaosimamia maadili ya kibinadamu, unaosherehekea utofauti na amani na unaoendana na sayansi na usasa", Mohamed Al-Amin Al-Tom, Waziri wa Elimu, alielezea, akikusudia kile kinacho nyamaziwa kimya juu yake kuzungumziwa, na tabia ya wengi kutokwenda kwenye maswala ya afya ya ngono, na kuona haya kuyajadili, na akasema kwamba hatujapatanishwa na miili yetu, haswa wanawake ambao kila wakati huamua kwenye mwelekeo wa kufinika sehemu zao za mwili. Pia alikusudia maswali yanayotokana na watoto kuhusu jambo hili, akionyesha kuwa ni kawaida kwao kutambua kazi za mwili, kwa sababu katika siku za usoni watahamia katika dori ya baba au mama, na Al-Tom akasisitiza haja ya upatanisho na mwili, na kuupuuza mtazamo wake kuwa umeumbwa kwa ajili ya raha na kuzaa pekee, haswa katika ulimwengu wa Kiislamu. Al-Tom alitoa wito wa kushughulikiwa suala hili, ndani ya muundo wa shule, kwa njia ya kisayansi. (SUNA).

Uwasilishaji wa elimu ya ngono katika kongamano la kielimu unakuja katika muktadha wa kisiasa wa serikali ambayo imetangaza vita vyake juu ya hukmu zlizobakia za Uislamu, na malezi ya watoto kwa maadili ya hadhara ya Magharibi, kwa hivyo suala sio suala la maridhiano, bali ni suala la kielimu linalotegemea fikra na fahamu, na kwa sababu hii Waziri wa Elimu lazima awajibike kwa fikra hizi chafu, na ilikuwa ni lazima kudai ukweli wa yaliyomo, sio fomu, na taarifa ya ni yapi maadili ambayo elimu hii ya ngono inayategemea.

Haishangazi kwamba Waziri wa Elimu katika serikali ya vibaraka wa mkoloni alizungumza, akizingatia kwamba mwanamke anayefinika mwili wake ni kufeli kujipatanisha na nafsi yake mwenyewe, na kwamba matibabu ya afya ya kijinsia hufanyika ndani ya muundo wa shule kwa ajili ya watoto. Kwa sababu kuamini makubaliano ya kimataifa na ya kikanda, na kujitahidi kuyafanya yawe msingi wa sheria na kanuni, imekusudiwa kuwatenga watu wa Sudan kutoka kwa kitambulisho cha Kiislamu na kuwaowanisha ndani ya mfumo wa kielimu wa Kimagharibi; Baada ya kutia saini Mkataba wa Kiafrika juu ya Haki za Mtoto, ambao unajengwa juu ya hadhara ya Kimagharibi, hapa tunakuja kwa kile kinachoitwa elimu ya ngono, na mengine, Mwenyezi Mungu atuepushie, yatakuwa mabaya zaidi.

Alitoa ufafanuzi wa wazo la elimu ya ngono kama "kuwapa vijana maalumati sahihi ya kisayansi ya kijinsia, kuunda maadili chanya na kupata ustadi wa kufanya maamuzi sahihi na ya uwajibikaji kulingana na maarifa, ili wasiache fursa ya kuwatumia vijana." Hapa tunajiuliza ni nini maadili chanya, ni ujuzi gani uliopatikana, na ni ipi haja ya watoto wa Kiislamu kuvutwa kwenye maalumati haya? Na je! Maalumati katika hatua ya utoto na ujana kuhusu maswala ya kijinsia yanaupungufu katika sheria za Kiislamu mpaka yatafutwe katika hadhara ya kikafiri?

Maadili yanayoitwa ya kibinadamu yanamaanisha maadili ya hadhara ya Kimagharibi. Kwa maana nyengine, hadhara ya makafiri wa kikoloni ambao, kutokana na wivu wao wenyewe, wanataka kumburuta mwanamke wa Kiislamu, familia, na mtoto ndani ya kinamasi cha hadhara yao iliyooza.

Hakika hayo ndio maagizo ya nchi za Magharibi ambazo Sudan imedhoofika chini ya madeni yake makubwa, na bila aibu serikali ya mpito inajibu, ikifanya kazi kupitisha miradi yao michafu, kupotosha jamii yetu, na kugonga maadili yetu ya Kiislamu. Kama vile kuingizwa kwa "elimu ya ngono" katika mitaala yetu ya elimu, ambayo ni kiungo katika safu ya sheria za Magharibi ambazo zimelazimishwa juu ya dola za nchi za Kiislamu; Kama vile kuhalalisha ushoga, usawa katika urithi, na mengine, na kwa sababu hii mazungumzo hayo hayahusiani na fahamu ya elimu, wala hayahusiani na uhalisia wa tabia ya ngono na jinsi inavyodhibitiwa kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu, na haihusiani na dori ya Uislamu kupitia hukmu zake na mfumo wake katika kuwaelekeza watoto katika tabia sahihi. Uislamu una njia yake ya kulea watoto, kuelimisha vijana, na kuwaangazia vijana, na hukmu za Uislamu zinawiana na zinatabikishwa na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake
katika Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu