Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Jumada II 1443 Na: Na: HTS 1443 / 20
M.  Ijumaa, 21 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu wa Sudan, Hakuna Kheri Yoyote Inayotarajiwa kutoka kwa Wajumbe wa Amerika na Ujumbe wa Usalama wa Umbile la Kiyahudi, kwa kuwa wao ni Maadui!
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 19/1/2022, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Amerika anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Molly Phee, na mjumbe wa Rais wa Amerika katika Pembe ya Afrika, David Satterfield, waliwasili nchini Sudan. Walikutana, kulingana na habari, na vikundi vya wanawake na vya kiraia, chama cha wataalamu, na vikosi vya kisiasa na vyama, na pia walikutana na Rais wa Baraza Kuu, Abdel Fattah Al-Burhan na naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo [Hemedti]. Wakati huo huo, wajumbe wa usalama walifika kutoka kwa umbile la Kiyahudi. Ilisemekana kwamba watakutana na Al-Burhan, Hemedti, na mkuu wa upelelezi, kulingana na kile Gazeti la Al-Sharq al-Awsat lilichapisha mnamo Alhamisi asubuhi, 20/1/2022. Ziara kama hizo hazikuwa za kwanza na hazitakuwa za mwisho maadamu Sudan inategemea dola za kikoloni na zana zake, wakiwemo Mayahudi na wengineo, na watawala wake ni vibaraka tu wa dola za kikoloni za Magharibi.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir/Wilayah ya Sudan tunawaonya watawala na wanasiasa, wanajeshi na raia kutokana na matokeo ya kuangukia mikononi mwa makafiri wa kikoloni, na tunasisitiza yafuatayo:

Kwanza: Amerika ni dola koloni ya kikafiri ambayo haiwatakii kheri Waislamu wa Sudan. Iliasisiwa juu ya magofu na mafuvu ya Wenyeji wa Amerika baada ya kuangamizwa kwao. Iliendelea kucheza mchezo wake wa kuua watu; haswa Waislamu wa Iraq, Syria, Yemen, Afghanistan na wengineo. Ndiyo iliyolitenganisha eneo la Sudan ya kusini, na sasa inatafuta kusambaratisha na kugawanya maeneo mengine yaliyobakia ya Sudan, hivyo hakuna kheri inayotarajiwa kutoka kwa wajumbe wake.

Pili: Wajumbe wa Amerika hawakuja ili kutatua matatizo ya Sudan, bali kuweka vibaraka wao kutoka kwa uongozi wa kijeshi. Wanachofanya katika mawasiliano na wasio wanajeshi ni ili kujishindia baadhi ya raia. Ama kauli za kulaani mauaji na uhalifu mwingine wa utawala uliopo ni kuwahadaa watu tu.

Tatu: Ziara ya ujumbe wa usalama kutoka kwa umbile la Kiyahudi sio ya kwanza ya aina yake, ambayo inathibitisha kwamba usawazishaji mahusiano unaotekelezwa na jeshi, haswa Al-Burhan na familia ya Dagalo, unaendelea kwa ujasiri chini ya meza, kwa sababu wanajua kwamba Waislamu wa Sudan hawatakubali, kama Waislamu wengine katika sehemu zote za dunia, kusawazisha mahusiano na umbile katili la Kiyahudi, ambalo limeunyakua Msikiti wa Al-Aqsa, cha kwanza katika vibla viwili na wa tatu ya Misikiti miwili mitukufu, na ardhi ya Israa ya kipenzi chetu Muhammad (saw).

Nne: Mawasiliano na umbile la Kiyahudi ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini; na watawala vibaraka watahisabiwa kwa ajili yake hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, itakaposimamishwa dola ya Kiislamu, Khilafah Rashidah ya Pili kwa njia ya Utume.

Kwa kutamatisha, ni Uislamu mtukufu pekee ndio unaotatua matatizo ya Sudan, na sio wajumbe wa Magharibi ambao hawathamin maagano wa mafungamano na Waislamu. Khilafah itakayoregea hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, itawaondoa makafiri.

Enyi watu wa Sudan, enyi wanasiasa, enyi askari waaminifu, amkeni na muweke mikono yenu mikononi mwa wana wa Ummah waaminifu, na toeni Nusra (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo ndani yake umo wokovu wenu, na utukufu wenu, na radhi za Mola wenu Mlezi.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu