Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Jumada II 1443 Na: HTS 1443 / 19
M.  Ijumaa, 21 Januari 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. [Al-Baqarah: 155-156]
(Imetafsiriwa)

Kwa kujisalimisha kikamilifu kwa Qadhaa na Qadar ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan inamuomboleza mmoja wa wanachama wake, ambaye alitumia ujana wake kubeba ulinganizi wa kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu, kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, aliye samehewa kwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):

Mubarak Abdul Hameed

ambaye alifariki mnamo siku ya Ijumaa, 11 Jumada al-Akhir 1443 H sawia na 14/1/2022 M, baada ya kutahiniwa na maradhi kwa miaka mingi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ammiminie rehema zake, alifanye kaburi lake kuwa bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi na atujaalie sisi na familia yake subira na ukumbusho mzuri.

 [إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea [Surah Al-Baqarah: 156]

 Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu