Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  21 Muharram 1445 Na: HTS 1445 / 02
M.  Jumanne, 08 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Wokovu kutoka kwa Uhalisia huu wa Mateso kwa Wanawake isipokuwa kupitia Dola inayotetea Haki

Khilafah Rashidah kwa Njia ya Utume
(Imetafsiriwa)

Mwanachama wa zamani wa Afisi ya Utendaji ya Chama cha Madaktari wa Sudan, Mtaalamu katika tiba ya ndani, majanga, na maradhi ya kuambukiza, Dkt. Adibah Ibrahim al-Sayyid, alifichua usajili wa kesi 316 za ubakaji, pamoja na kesi zinazohusisha watoto, kulingana na vyanzo vya matibabu jijini Khartoum Na Darfur. Alithibitisha usajili wa kesi 61 za ubakaji jijini Khartoum, kesi 55 huko Nyala, na kesi 200 katika mji wa El Geneina, akisema labda wahusika wa uhalifu huo wanatoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka. (Chanzo: Gazeti la Al-Jarida, Agosti 7, 2023).

Kujibu uhalifu huu wa kinyama, tunafafanua yafuatayo:

Kwanza, ubakaji ni uhalifu muovu, na Sharia safi (sheria ya Kiislamu) ina msimamo wazi wa kuuharamisha na kuweka adhabu kali kwa wahusika wake.

Pili, Sharia imekabidhi utabikishaji wa adhabu ya Sharia kwa Khalifa wa Waislamu na kwa kukosekana Khalifa, inakuwa ni jukumu la Waislamu kufanya kazi kwa bidii katika kuwepo kwake. Hii ni faradhi inayoungwa mkono na dalili za pamoja kutoka katika Quran, Sunnah, na makubaliano (ijmaa) ya Maswahaba.

Tatu, kwa wale wanaokimbilia kwa mashirika ya kimataifa, kikanda, au ya ndani, wakitumaini kwamba haki itatekelezwa au kuadhibiwa kwa ajili ya wahasiriwa hawa wa ubakaji, wanapaswa kugundua kuwa mashirika haya ni zana tu mikononi mwa dola kuu, haswa Marekani. Haipaswi kutarajiwa kwamba yatatoa azimio la kulaani dhidi ya upande wowote unaotumikia dola zinazo zozana katika harakati ya kutekeleza maslahi ya Marekani, ambayo ilichochea vita kati ya majenerali wake wawili, Burhan na Hemeti, bila kujali utukufu wa uhai au heshima.

Kwa kumalizia, tunasema kwamba Khilafah inayokuja, Bi idhnillah, ndio wokovu kutokana na ulisia huu wa mateso kwa wanawake. Ulisia huu umesababishwa na kukuzwa na serikali hizi za kihalifu za ukandamizaji, ambazo zimeweka mbali Uislamu na utawala na uchungaji wa mambo ya watu na kujitupa katika kumkumbatia kafiri mkoloni.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu