Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Muharram 1445 Na: HTS 1445 / 01
M.  Jumatatu, 24 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Khilafah ndiyo Inayoyaelekeza Majeshi Kulinda Heshima
(Imetafsiriwa)

Wavuti wa Showtime ulichapisha rekodi ya raia, ambayo kwayo anawaomba raia wa Jimbo la Khartoum kufuatilia habari za binti zao waliopotea tangu kuanza kwa vita, na inasema kwamba wanamgambo walianza kuuza wasichana waliotekwa nyara kutoka mji mkuu, lakini pindi juhudi zao zilipofeli, walianza kudai fidia ya kuachiliwa kwao huru. (Wavuti wa Showtime, Julai 22, 2023).

Habari na video zimewasilisha kupitia mitandao ya kijamii, picha za kuogofya za mauaji, kuchanwa chanwa, na kukatwa/kupunguzwa kwa viungo vya wanadamu, na baya zaidi, ubakaji wa wanawake, kulingana na mashirika ya kimataifa yaliyofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka, kuendelea kudhalilisha hadhi ya watu wa Sudan na kupuuza heshima, operesheni ya utekaji nyara wanawake na familia zao, kuwaweka kwa mauzo, na kuitisha fidia, kama ilivyo kwenye habari za hapo juu.

Enyi Waislamu: Mwanamke katika Uislamu ni mstari mwekundu, na hili linajulikana na Ummah wa Kiislamu, ambalo liliufanya iwe tofauti na Ummah nyenginezo ambazo hutukana hadhi ya wanawake, na hawajali kuhusu heshima. Uislamu umehifadhi na kuwaheshimu wanawake, kuharamisha unyanyasaji wao, na umehifadhi hadhi na heshima yao. Bali, umewazingira kwa ngome ya Ahkam (hukmu) ambazo ziliwadhaminia maisha ya hadhi na heshima, na kumwaga damu kwa gharama yoyote kwa ajili yao.

Enyi Watu Wanyoofu Miongoni mwa Watoto Wetu katika Majeshi Haya: Ummah wa Muhammad (Saw), daima umehamasisha majeshi ili kuhami heshima ya wanawake wa Kiislamu, katika zama zote za Dola ya Kiislamu, na kamwe haujawahi kusita kumnusuru mwanamke wa Kiislamu, kwa kufuata Kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mwenyezi, na kufuata mfano wa Sunnah ya Mtume Wake (Saw) ambaye aliwafukuza Mayahudi wa Banu Qainuqa kutoka Madina pindi walifunua uchi (awra) wa mwanamke mmoja wa Kiislamu, na katika historia yote, nchi kama Amuriyah na India zilikombolewa kwa kilio cha mwanamke mmoja aliyesema, "Wa Islamaa", majeshi ya Waislamu yasonga kunusuru heshima yetu. Chukueni mfano kutoka kwa mababu zenu, na musonge ili kuziachilia huru familia za dada zenu walio katika mazingira magumu miongoni mwa wanawake wa watu wa Sudan.

Enyi Waislamu: Daima mumetafuta masuluhisho na tiba kwa migogoro mingi iliyokusanyika, ambayo imetesa roho zenu kabla na baada ya vita, kutamani maisha bora. Na kwa hiyo, ilikuwa mihanga yenu isiyo na maono, kwani mumekuwa mukizalisha mazingira yale yale ya kisiasa kila wakati, na viongozi waliohusishwa na nchi za kikoloni wenyewe, kwa hivyo mihanga ilikuwa bure bilashi! Siri katika mchakato wa mabadiliko ni ufahamu wa mfumo mtukufu wa Uislamu, na juu ya uhalisia huu wa mateso, pamoja na ufahamu wa kisiasa, yaani kuutazama ulimwengu kutoka kwa pembe maalum, kutoka kwa mtazamo wa Uislamu.

Kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan kinakualikeni mufanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kuleta usafi wa Uislamu madarakani kusimamisha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu