Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  11 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: HTS 1445 / 44
M.  Jumapili, 19 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vibaraka wa Makafiri wa Magharibi na Ukakamavu wa Kuendelea na Mradi wa Kuigawanya Sudan
(Imetafsiriwa)

Abdul Wahid Nur, kiongozi wa Vuguvugu la Ukombozi wa Sudan, na Waziri Mkuu wa zamani Abdalla Hamdok walitia saini tangazo jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Mojawapo ya vifungu vyake muhimu zaidi ni pamoja na: Kifungu cha 4, nukta (d), ambacho kinataka kuanzishwa kwa serikali kisekula ambayo itasalia kutoegemea upande wowote na iliyo ya kati na kati kidini, kitamaduni na vitambulisho vyote. Nukta (e) inataka kuanzishwa kwa serikali ya majimbo ya kiraia ya kidemokrasia nchini Sudan ambayo inahakikisha kuundwa kwa serikali ya kiraia. Pia inajumuisha vipengee vya uhuru wa dini na fikra, na inadhamini utambulisho wa kitamaduni, kikabila, kidini na kikanda. Tangazo hilo linahitimisha kifungu hiki kwa kusema: "Ikitokea kwamba kanuni hizi hazijajumuishwa katika katiba ya kudumu, watu wa Sudan wana haki ya kujiamulia wenyewe."

Kwa kuzingatia tangazo hili, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunathibitisha ukweli ufuatao:

Kwanza: Sudan imetawaliwa na mfumo wa kisekula tangu kuingia kwa majeshi ya wakoloni wa Uingereza mwaka 1899 hadi leo, ambapo katiba ilianzisha maisha kwa msingi wa kutenganisha Dini na maisha.

Pili: Sababu ya msingi ya matatizo yote ya Sudan ni fikra ya usekula, au demokrasia, ambayo ni wazo moja linalomaanisha utekelezaji sheria zilizotungwa na binadamu kupitia mabunge na mabaraza ya kutunga sheria, na kutengwa kwa hukmu ya Muumba, Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tatu: Msisitizo wa viongozi hawa, wawe wanasiasa au wanajeshi, katika kutabikisha usekula unalenga kutekeleza maamrisho na maagizo ya dola za kikoloni zinazojitahidi kuupiga vita Uislamu na kuuzuia kutawala na siasa, hivyo kupambana na wabebaji na watetezi wake.

Nne: Kuanzisha maisha juu ya itikadi ya kutenganisha Dini na dola kunamaanisha kuendelea na maisha ya shida, mateso, na kufeli katika kusimamia nyanja zote za maisha, iwe ya kisiasa au ya kiuchumi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha:124].

Tano: Kufanya kazi ili kutabikisha majimbo, kujitawala wenyewe, na kujiamulia wenyewe ni kuiweka nchi katika mashini ya ugawanyaji na uharibifu, na ni kazi chafu inayotekelezwa tu na vibaraka walioanguka.

Kwa kumalizia: Tangazo hili linathibitisha jinsi vibaraka wa dola za kikoloni wanavyofanya njama usiku na mchana kutekeleza mpango wa mabwana zao nchini Sudan, ambao unazunguka pembetatu ovu: ukiondoa Uislamu na kupigana na wabebaji na watetezi wake kwa kuweka ubaguzi wa kidini, kuigawanya Sudan kupitia majimbo, kujitawala wenyewe, na kujiamulia wenyewe, na kisha kupora rasilimali kupitia wawekezaji wa kigeni na makampuni ya kibepari ya kikoloni.

Wajibu wa watu wa Sudan ni kuchukua msimamo dhidi ya viongozi hawa wasaliti, kuwafichua, na kusimamisha Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hili litaunganisha Ummah chini ya kitambulisho cha Uislamu, licha ya tofauti za rangi na lugha, ambapo hakuna aliye mbora kuliko mwengine isipokuwa kwa taqwa (uchamungu). Kupitia bayah (ahadi ya utiifu) halali kwa Khalifa ambaye anasimamia uadilifu, anayehakikisha usalama, na anayempa kila mtu haki yake inayostahiki.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum:5]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu