Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Rabi' II 1446 Na: HTS 1446 / 17
M.  Jumamosi, 26 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwa Anwani:
Makubaliano ya Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na Kupuuza kwa Watawala Maslahi Muhimu ya Ummah
 

(Imetafsiriwa)

Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehma na amani zimshukie aliyetumilizwa kuwa rehma kwa walimwengu wote, na kiongozi wa wachamungu, bwana wetu na kipenzi chetu Muhammad, rehma na amani zimshukie na jamaa zake. Ama baada ya hayo,

Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Kuzungumza juu ya makubaliano ya maji na mabwawa ni jambo muhimu na zito, ikizingatiwa kuwa maji ni muhimu, na kupitia kwayo watu wanaishi, bali ndio msingi wa uhai wote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ]

“Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai.” [Al-Anbya 21:30].

Kulikuwa na msururu wa makubaliano yanayosimamia mtiririko wa maji ya Mto Nile na mito yake mingi kati ya nchi za Bonde la Mto Nile, ambayo ilifanya hali kuwa tulivu kati ya nchi hizi kwa miaka mingi. Hata hivyo, hivi majuzi, makubaliano hayo yalikiukwa na makubaliano mipya, kama vile Makubaliano ya Entebbe, ambayo yalihitimishwa katika mji wa Entebbe nchini Uganda Mei 2010, ambapo Ethiopia, Uganda, Rwanda, Tanzania, na Burundi zilitia saini kile kilichoitwa Makubaliano ya Bonde la Mto Nile, huku yakikataliwa na Misri na Sudan bila hatua zozote za dhati kutoka kwao za kubatilisha makubaliano haya.

Suala hatari zaidi lililojiri katika Makubaliano ya Entebbe ni yafuatayo:

1- Matumizi sawa ya maji ya Bonde la Mto Nile. Madhumuni ya makala haya ni kuhitimisha hisa za kihistoria za Misri na Sudan, yaani, mita za ujazo bilioni 55.5 kwa Misri, na mita za ujazo bilioni 18.5 kwa Sudan, kwa sababu ibara ‘matumizi sawa’ ni ibara huru. Kwa hivyo, ni nani anayeamua kiwango cha usawa huu kwa kuzingatia kifungu kinachosema kwamba maamuzi hupitishwa na wengi na sio kwa kauli moja kama ilivyokuwa hapo awali?

2- Makubaliano hayo pia yaliweka masharti ya kuundwa kwa tume, baada ya nchi zisizopungua 6 kupitisha makubaliano hayo kupitia mabunge yao, na makao makuu ya tume hiyo yatakuwa Uganda. Mabunge ya Ethiopia na Rwanda mwaka 2013, Tanzania 2015, Uganda 2019 na Burundi 2023 tayari yameidhinisha, huku Kenya bado haijapitisha.

Mnamo tarehe 15/7/2024, Sudan Kusini iliidhinisha makubaliano hayo, na kwa kuidhinisha kwake, idadi ya kisheria ya kuanzisha Tume ya Bonde la Mto Nile ilikamilika, siku 60 baada ya Sudan Kusini kuweka uidhinishaji wake wa makubaliano hayo.

Kwa sababu Misri na Sudan hazishughulikii kwa umakini, kama tulivyotaja, walitoa tamko la pamoja siku moja tu kabla ya makubaliano hayo kuanza kutekelezwa. Taarifa yao iliyotolewa Jumamosi, tarehe 10/12/2024, ilisema kwamba Makubaliano ya Mfumo wa Bonde la Mto Nile hayalazimiki kwa yeyote kati yao, si tu kwa sababu hawakujiunga nayo, bali pia kwa sababu yanakiuka kanuni za sheria za kimataifa; kimila na kimkataba. Siku moja baada ya taarifa hii ya Misri na Sudan, ambayo hainenepeshi wala kuridhisha, Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, aliandikwa tweet kwenye jukwaa la X mnamo Jumapili, 13/10/2024, akielezea kuanza kwa utekelezaji wa Makubaliano ya Mfumo wa Bonde la Mto Nile kama zama za kipekee.

Haya ni kuhusu Makubaliano ya Entebbe ambayo yanaonyesha wazi njama dhidi ya haki za maji za Misri na Sudan, kiwango cha uzembe wa watawala wa Misri na Sudan, na msimamo wao dhaifu kuelekea njama zinazofanyika.

Pia, miongoni mwa makubaliano mapya yaliyokiuka makubaliano ya awali yanayohifadhi haki za Misri na Sudan kwenye maji ya Mto Nile ni Azimio la Kanuni za Makubaliano yaliyosainiwa na marais wa Misri na Sudan, na Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Khartoum tarehe 23/10 /2015. Ni makubaliano mabaya zaidi kuliko Makubaliano ya Entebbe yaliyotiwa saini mwaka 2010, kwa sababu yanajumuisha utambuzi kamili wa ujenzi wa Ethiopia wa bwawa la maafa, na haki yake ya kuhifadhi maji, ikizingatiwa kuwa bwawa hilo lilijengwa ndani yake; yaani, nchini Ethiopia, na ubwana lazima uwe sawa kwa sawa, kwani Sudan ina ubwana wake kama vile Misri na Ethiopia.

Kwa saini hii ya usaliti, makubaliano yote ya awali yalibatilishwa, na Ethiopia ilipewa haki ya kujenga mabwawa yoyote inayotaka kwenye Blue Nile. Huu unachukuliwa kuwa ni upuuzaji wa watawala wa Misri na Sudan wa haki za Ummah za usalama wa maji.

Swali linalojitokeza sasa ni je, nchi hizi zilizosaini Makubaliano ya Entebbe zinafanya kazi kwa utashi wao na hitaji lao la maji, au kuna uingiliaji wa nje unaotaka kucheza na suala hilo?!

Amerika iliingilia kati mapema suala la maji la Bonde la Nile. Wataalamu kutoka Afisi ya Marekani ya Uhifadhi wa Ardhi, kwa uratibu na Ethiopia, walifanya tafiti za kina katika eneo la Benishangul na miradi ya maji kote Ethiopia. Tafiti ziliandaliwa kwa ajili ya miradi 33, ikiwa ni pamoja na mabwawa manne, na tafiti hizi ziliambatana na wazo la kujenga Bwawa Kuu nchini Misri kwa miaka kadhaa, na zilikamilishwa mnamo 1964, lakini Ethiopia haikuweza kutekeleza miradi hii wakati huo.

Wakati Ethiopia ilipanga kudhibiti Mto Nile, miradi ya umbile la Kiyahudi iliibuka kupata hisa ya maji ya Mto Nile, yakisafirishwa kwa mabomba, lakini rai jumla nchini Misri inakataa kabisa hili, na Rais wa zamani wa Misri Sadat alijaribu kupata idhini kutoka kwa rai jumla ya umma. Gazeti la Asharq Al-Awsat liliripotiwa katika Toleo lake la 11211 lililotolewa tarehe 8/8/2009, na Anis Mansour, ambapo aliandika: “Rais Sadat aliniomba nichapishe habari ambayo ingekuwa puto la majaribio, kiini chake ni: Rais Sadat anaota siku ambayo maji ya Mto Nile yatafika Al-Qudsi ili Waislamu waweze kutawadha na kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa.”

Katika makala ya gazeti la Lebanon la Al-Mustaqbal la tarehe 20/10/2010, yafuatayo yalielezwa: ‘Israel’ inafadhili ujenzi wa mabwawa matano ya kuhifadhi maji ya Mto Nile nchini Tanzania na Rwanda, kufuatia ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa ‘Israeli’ Avigdor Lieberman kwa nchi za bonde hilo. Kitabu cha mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Marekani Michael T. Klare, ‘Resource Wars: The New Landscape of Global’, pia alifichua mpango wa Kiyahudi wa kudhibiti maji ya Bonde la Mto Nile, akisema: ‘Israel’ imekuwa na dori kubwa na nchi za Bonde la Mto Nile kukiuka mikataba ya kimataifa ambayo inadhibiti usambazaji wa maji ya Nile, na yaliyofichika ni makubwa zaidi.

Hii inathibitisha kwamba nchi zinazoitwa za bonde ni ala tu zinazotumiwa kuishinikiza Misri na Sudan kuhusu suala la Bonde la Mto Nile.

Kuna habari muhimu, ambayo ni kwamba nchi hizi zinazofanya njama dhidi ya Misri na Sudan hazihitaji maji, kwani ziko katika eneo la tropiki lenye mvua nyingi, na wataalam wa maji wanakadiria kiwango cha maji cha kila mwaka kwa nchi za mabonde kwa zaidi ya mita za ujazo bilioni 1000. Yote ambayo Sudan na Misri huchukua hayazidi mita za ujazo bilioni 75 kwa mwaka.

Ndugu wapendwa, maji ni muhimu, na watu hawawezi kuishi bila maji, kwani ni moja ya mahitaji muhimu ambayo hayawezi kubadilishwa. Msimamo huu wa aibu unaowakilishwa na tawala za Misri na Sudan ndio iliozipa moyo nchi hizi hasa Ethiopia. Katika taarifa ya hivi punde zaidi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, iliyochapishwa katika Al Arabiya Net mnamo tarehe 20/10/2024, alithibitisha kwamba njia za mazungumzo yaliyofanyika na upande wa Ethiopia katika kipindi cha miaka 13 ziliishia patupu! Kauli hii inaonyesha ukubwa wa udhaifu na udhalilifu wa tawala hizi za vibaraka wateja, kwani mazungumzo ya kipuuzi yaliyotajwa na waziri hayakuishia patupu, bali yaliishia kwa ujenzi wa Bwawa la maafa la Al-Nahdha, ambalo limefikia hatua za juu, na inasemekana kwamba sasa linahifadhi mita za ujazo bilioni 60 za maji, na hivyo limekuwa bomu linalosubiri wakati na kizungumkuti ambacho tawala za Misri na Sudan hazitaweza kufanya chochote zaidi ya kauli ambazo hazinenepeshi wala kukidhi njaa.

Udanganyifu wa watawala wa Misri na Sudan kuruhusu ujenzi wa Bwawa la Al-Nahdha ni kupuuza maslahi ya Ummah, na unakiuka sheria za Kiislamu kwa sababu zifuatazo:

1- Inazuia watu kupata maji, na hii ni haramu. Mtume (saw) amesema: «ثَلَاثٌ لَا يُمْنَعْنَ: الْمَاءُ، وَالْكَلَأُ، وَالنَّارُ» “Vitu vitatu haviwezi kunyimwa kwa yeyote: maji, malisho na moto” (Sunan Ibn Majah). Na akasema, rehma na amani zimshukie: «وَالنَّار النَّاسُ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي الْمَاءِ، وَالْكَلَأِ،» “Watu wanashirikiana katika vitu vitatu: maji, malisho na moto.” Maji ya Mto Nile si mali ya utawala wa Marekani, wala dola ya Kiyahudi au Ethiopia kuyazuia watu, wala si mali ya serikali ya Misri na Sudan ili kuyafuja, bali ni mali ya umma ambayo haifai kuzuiliwa.

2- Inawapa nguvu Makafiri juu ya shingo zetu, hivyo watakuwa na udhibiti zaidi juu yetu kuliko wanavyofanya sasa, na hili ni haramu na ni lazima lizuiliwe. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa 4:141]. Kisichoacha nafasi ya shaka ni kwamba bwawa hili lilijengwa ili kuwatiisha zaidi watu wa eneo hilo, kuwaingiza katika mizozo na mapigano, na kumwongoza mkoloni Kafiri kwenye vita hivi. Kwa upande mwingine, inaiwezesha dola ya Kiyahudi kujipatia maji kutoka Mto Nile! Hii ni zaidi ya kuwa na nguvu juu ya Ummah, na hili limeharamishwa na Sharia.

3- Ina madhara ambayo ni vigumu kuyahesabu kutokana na wingi wake, na mingi yake yametajwa. Madhara haya ni haramu na lazima yaondolewe. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ» “Hakuna kudhuru (watu wengine bila ya sababu), wala kudhuriana (baina ya makundi mawili).”

Lau Sudan na Misri zingekuwa sehemu ya Khilafah Rashida, nchi duni, kizazi cha ukoloni na zana zake, zisingesubutu kutishia maslahi muhimu ya Khilafah, bila kujali Uislamu na Waislamu. Khilafah ni dola ya kimfumo inayotaka kushika nafasi ya mbele ya hali ya kimataifa, hivyo orodha ya maslahi muhimu ya Khilafah Rashida ni ndefu sio fupi, na kwanza hakuna nchi ingesubutu kutishia maslahi haya.

Historia ya Khilafah ina mafunzo na maadili juu ya izza yake na kuhifadhi maslahi ya Waislamu, kupitia nguvu ya matendo yake ya kisiasa, fahari na kiburi cha wapatanishi wake na wanadiplomasia, kiburi na fahari yao, na tishio lake la kutumia nguvu za kijeshi, kisha matumizi yake halisi, na inaungwa mkono na mamilioni ya wanaume wanaotazamia kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ni dola ya utukufu na heshima, ambayo kila Muislamu anapaswa kushirikiana na wale wanaofanya kazi ya kuisimamisha kwa ajili ya maisha mema ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambayo wakaazi wa mbinguni na ardhini wanaridhishwa nayo.

Wa Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu