Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  16 Jumada I 1438 Na: 1438/02
M.  Jumatatu, 13 Februari 2017

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Madawa ya Kulevya Nchini Tanzania na Mchango wake katika Mapato ya Kirasilimali

Vita dhidi ya madawa ya kulevya vinaonekana kuzidi kasi nchini Tanzania baada ya Kamishna wa Eneo la Dar es Salaam kuamuru msururu wa ukamataji wa watu wenye haiba ya juu na maarufu. Vita hivi vilitiliwa nguvu zaidi na taarifa ya Rais kuwa vita hivi ni ajenda pana ambayo inapasa kujumuisha taasisi zote na uteuzi wake wa Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Mihadarati (Taasisi ya Kutekeleza Udhibiti wa Madawa ya Kulevya (DCEA)).

Kuhusiana na hili, sisi katika Hizb ut Tahrir Tanzania tunataka kuweka wazi yafuatayo:

1. Vita dhidi ya mihadarati nchini Tanzania vinaendeshwa kwa uhadaifu, kwani mfumo wa kirasilimali unaotawala ulimwengu leo umejengwa juu ya msingi wa maslahi, ambapo kila kitu hupimwa kwa kipimo hicho. Zaidi ya hayo, siasa katika nidhamu ya kidemokrasia hufadhiliwa na warasilimali ambao mara nyingi huwa ni washikadau wakuu wa biashara ya madawa ya kulevya. Hivyo ni wazi kuwa vita hivi dhidi ya madawa ya kulevya vinakosa ikhlasi, ni mwito mtupu wa kuwahadaa na kuwapurukusha watu kutokana na kufeli kwa serikali katika kadhia nyingi. Nyuma baadhi ya wanasiasa wenye vyeo vya juu walijigamba kuwa orodha ya wafanyi biashara wa madawa ya kulevya iko mikononi mwao, ilhali licha ya mamlaka yao makubwa hawakusubutu kuwataja.

2. Nidhamu ya kidemokrasia inapigia debe na kukuuza fikra ovu na hatari ya 'uhuru wa kibinafsi' katika watu wake inayo washajiisha watu wengi kuingia katika matumizi ya mihadarati kama sehemu ya kufurahia uhuru wao. Hivyo basi, matumizi ya madawa ya kulevya yana mahusiano ya moja kwa moja na fikra ya uhuru ambayo ndiyo fikra kuu katika demokrasia.    

3. Mfumo wa kirasilimali hususan nidhamu yake iliyo filisika ya kiuchumi imewatumbukiza wanadamu katika mateso mabaya ambayo yamewapelekea kupata msongo wa mawazo kutokana na athari yake ngumu na mbaya, mwishowe imewasukuma baadhi kudhani kuwa kujiingiza katika madawa ya kulevya kutawaondolea mateso ya kiakili au hata kupata afueni ya muda. Urasilimali unakosa suluhisho la kiroho la kumtuliza mwanadamu wakati wa shida. 

4. Zaidi ya hayo, nidhamu ya kidemokrasia katika kuongeza maslahi ya kiuchumi inawasukuma watu kujisalimisha na kiasi kuwaabudu wasanii kama viigizo vyao vyema, ambao baadhi yao ni watumizi wa madawa ya kulevya. Natija yake vijana wengi waliopagawa wametumbukia ndani ya shimo la mihadarati.   

5. Nidhamu ya kidemokrasia pamoja na mbinu yake ya kisekula katika sheria iliyo tungwa na wanadamu kamwe haiwezi kumaliza tatizo la madawa ya kulevya, kutokana na tabia yake ya undumakuwili ya kuhalalisha baadhi ya aina za ulevi na kuharamisha nyingine. Huku kiuhalisia ikiwa aina zote za pombe zina madhara kwa wanadamu. Vipi utakuwa na ujasiri na maadili kupambana na madawa ya kulevya, ilhali unaruhusu aina nyingine za madawa ya kulevya?

Uislamu ndio mfumo pekee ulio na nguvu na imani na sheria kulinda mujtama kutokana na madawa ya kulevya; na kukabiliana na vita hivi kikamilifu kupitia kupiga marufuku aina zote za ulevi. Wakati umewadia sasa hususan kwa wasiokuwa Waislamu kufurahia uadilifu wa Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah inayofanya kazi bila ya kuchoka kulinda hadhi ya wanadamu, mali, imani nk.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu