Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  2 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441/45
M.  Alhamisi, 23 Julai 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukabidhi Mamlaka kwa Hizb ut Tahrir
Ndio Hatua ya Kwanza katika Kumchukua Umar bin Al-Khattab (ra) kama Kiigizo Chema
(Imetafsiriwa)

Kwa muda mrefu, Raisi Kais Saied amemchukua bwana wetu Umar Al-Faruq, Khalifah Muongofu, (ra), kiigizo chake chema. Mara ya mwisho kumnukuu Umar bin Al-Khattab (ra) ilikuwa ni Jumatano, 22/7/2020, alipokuwa akizungumza kuhusu mojawapo ya mambo ya ufisadi katika mahakama za Tunisia, alisema: "Unajua alilosema siku moja, "Endapo nyumbu atavunjika mguu (akiwa barabarani) nchini Iraq, Mwenyezi Mungu ataniuliza kwa nini hukutoa njia kwa ajili yake Umar?" nitasimama mbele ya Mwenyezi Mungu na sitamuogopa yeyote isipokuwa Yeye, Mola wa Walimwengu, ataniuliza kwa nini nilibakia kimya kuhusu haki hii kwa sababu ndio haki na yeyote atakaye nyamazia kimya kuhusu haki basi yeye ni shetani bubu."

Taarifa hizi za Raisi Saied zinagongana na vitendo vya Umar Al-Faruq (ra):

Umar ibn Al-Khattab (ra), alikuwa makini sana katika kutabikisha hukmu halisi ya Mwenyezi Mungu na Sunnah safi ya Mtume Wake (saw), mpaka Mtume akampa jina la Al-Faruq; kwa sababu alipambanua baina ya haki na batili katika uamuzi wake juu ya mnafiki ambaye hakutosheka na hukmu ya Mwenyezi Mungu. Ama Raisi Kais Saied, yeye yuko makini katika kuhukumu kwa yale ambayo hakuyateremsha Mwenyezi Mungu. Mara kwa mara amesisitiza kwamba amejitolea, yuko makini, na ni mdhamini wa katiba asili iliyo simamiwa utunzi wake na Myahudi Noah Feldman!

Vilevile, Umar bin Al-Khattab (ra), alikuwa na hamu na Uislamu na Khilafah, hivyo alikuwa wa kwanza kutoa ahadi ya utiifu (Bay'ah) kwa Abu Bakr (ra) kama Khalifah, alipewa Khilafah katika hali ambayo ni muhimu sana baada ya kifo cha Abu Bakr, kipindi ambacho Waislamu walikuwa wanapigana na dola mbili kubwa zaidi duniani. Na wakati ambapo Majusi alimdunga kisu, alichora mpango ulio na ufafanuzi wa jinsi wa kumchagua Khalifah (mrithi), ambapo inaonyesha kwamba umoja wa Waislamu una thamani zaidi kuliko damu ya maswahaba endapo watarudi nyuma katika kutoa ahadi ya utiifu kwa Khalifah, na maneno yake maarufu alisema: "Hakuna Uislamu bila ya jamaa, hakuna jamaa bila ya uongozi, hakuna uongozi bila ya utiifu." Ama katika zama za Raisi Saied, Uislamu umeondolewa katika utawala na wabebaji ulinganizi wake wanapigwa vita na wanachama wa Hizb ut Tahrir wanakamatwa na kushtakiwa kwa mashtaka ya kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume!

Ni upi msimamo wa Raisi Saied kuhusiana na dhulma hii?! Je, hajui kwamba Umar ibn Al-Khattab alikuwa ni mtetezi wa ulinganizi wa Uislamu dhidi ya maadui zake, ambapo Abdullah bin Masoud alisema kuhusu hilo: "Bado tungali washindi tangu Umar asilimu"?!

Wasifu wa Khalifah Umar bin Al-Khattab (ra) unajulikana. Hakuwatawala watu kwa hukmu ya kikafiri na hakulegeza msimamo kwa maadui wala kutafuta ridhaa yao, hakuirahisisha nchi yetu, maji yetu, anga yetu na mtiririko wa rasilimali zetu kwa maadui zetu. Alikuwa ni shabiki wa Uislamu na Khilafah na mmoja wa wafanyikazi wake. Hatua ya kwanza ambayo Raisi Kais Saied ni lazima aifuate katika kumchukua kumchukua Al-Faquq Umar kama kiigizo chema, ni kuunga mkono mradi wa Khilafah, kupitia kukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah na kutabikisha Uislamu na kuiokoa nchi hii kutokana na upuuzi wa kidemokrasia na ushawishi wa kigeni.

Tunamkumbusha maneno ya Al-Faruq (ra): "Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu ametupa utukufu kupitia Uislamu. Na pindi tutakapo tafuta utukufu kupitia kitu chochote chengine, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha tena."

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu