Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  17 Shawwal 1434 Na: 1434/159
M.  Jumamosi, 24 Agosti 2013

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Ubwana Unaodaiwa Umeuzwa Kwa Bei Nafuu!

(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al Shari’ liliripoti Jumamosi tarehe 14 Agosti, 2013, katika toleo la Na: 589 makala iliyopewa jina:  "Makubaliano ya siri ya Kijeshi kati ya Yemen na Amerika" na ilisema yafuatayo:  "Jeshi la Amerika lilipewa uhuru wa kuruka juu ya ardhi yote na anga ya Yemen kwa kufanya uchunguzi wakati wowote kila siku. Na ndege za Amerika zilipewa uhuru wa kutua na kuondoka kwa siri kutoka katika Uwanja wa ndege wa Sana'a na kwa mahitaji ya dharura na Jeshi la Majini la Amerika lilipewa uhuru wa kutembea katika maji ya Kitaifa ya Yemen kutumia ukanda wa pwani nchini Yemen. Na idadi ya askari wa Amerika iliongezeka huko Al-Anad na Sana'a, na uwepo wa meli saba za kivita za Amerika na meli nne za kivita za Uingereza kusafiri katika maji ya Yemeni, na muda wa makubaliano ni miezi sita na inaweza kuongezeka."

Huduma hizi maalum kwa Wamarekani ni kubadilishana kwa ahadi ya Washington kutatua upungufu wa bajeti ya Yemen na kuongeza muda wa Rais Hadi na kuishawishi Amerika na Saudi Arabia kutoa dola bilioni 1.7 ili kufidia upungufu wa bajeti na kujenga ukuta wa kugawanya kati ya nchi hizo mbili na kueneza vikosi vya Yemen hapo ili kuzuia magendo kati ya nchi hizo mbili.

Kabla ya mpango huu, Amerika iliitumia Yemen idadi ya wanajeshi huko Anad na Sana'a chini ya kile kiitwacho "vita dhidi ya ugaidi". Swali ambalo linahitaji kuulizwa: Je wanajeshi wa Marekani waliopo sasa, meli za vita za Marekani na Uingereza, droni za Marekani na kambi za kijeshi za Marekani zilizoko Anad zote hizo ni kwa ajili ya kupambana na kile kiitwacho ugaidi? Ambao umeanzishwa na kuundwa na Amerika? Au ni hoja na kisingizio cha kuifanya nchi ijisalimishe chini ya ushawishi wa Kafiri Mmagharibi hata zaidi ya usalimishaji wake wa sasa na kujiuzulu?

Baada ya kusoma katiba ya Yemen, kifungu cha kwanza kinasema kuwa Jamhuri ya Yemen ni nchi huru ya Kiarabu. Hata ingawa hatuko hapa kufichua mgongano katika katiba ya Yemeni na bado lazima tusimame na kutafakari juu ya neno ubwana.

Ni ubwana upi ambao nchi ya upigia baragumu, wakati unakiukwa kwa njia hii na makubaliano kama ya baharini, hewani au ardhini? Je! Uwepo wa magaidi huko Yemen kama inavyodaiwa na Amerika, umewapa haki ya kukiuka ubwana wa Yemen na kuwapa uhuru wa kuwatafua magaidi hao na kuwaua kwa droni. Je waufanyao Amerika sio ugaidi wenyewe? Kutokana na ujanja na uwerevu wa Amerika ni kwamba ilifanya makubaliano kwa miezi sita tu na hiyo ni kujaribu maji; ikiwa watu wa Yemen watakaa kimya, basi makubaliano haya yanaweza kuongezwa hadi mwaka mmoja, miwili au zaidi.

Je ubwana wa nchi hiyo ungekiukwa au kuruhusu damu ya watu kumwagwa kwa nyongeza ya muda wa urais, au malipo ya upungufu wa bajeti? Na je kuongezwa muda kutawekwa kwa upande mmoja na uuzaji wa Socotra kwa upande mwingine? Au ni jukumu la kuwa na mpango wa kiuchumi ambao unahuisha nchi kupitia mfumo wa uchumi wa Kiislamu chini ya kivuli cha Khilafah badala ya wakati mwingine kuomba milangoni mwa Mashariki na mara nyingi kutoka Magharibi?

Wacha wale wanao simamia hatima ya watu na nchi; na kusalimisha mambo ya umma kwa Kafiri Mmagharibi  wajue kwamba kutakuwa na athari kubwa juu ya kutenda dhambi kubwa. Yeyote anayetambua uovu huu (Munkar) na asiwakataze, atakuwa mwenziwao katika uhalifu na dhambi.

Tunawasihi watu mukhlisina wa Yemen kutoka katika jeshi na watu wakweli wa makabila tukufu ambao walikuwa wa kwanza kumpa Nusra Mtume (saw), kusimama dhidi ya njama hizi na kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kuondoa serikali mbovu ambayo ilipandwa na Wamagharibi kutekeleza maagizo yake na kuizamisha nchi, kuitawanya vipande vipande na kuwakabidhi wenyewe.

Tunatoa wito kwa umma mtukufu kusimama na Hizb ut Tahrir ili kukubali wazo lake na mradi unaotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake (saw) ambaye ndiye mwokoaji wa Ummah na binadamu kupitia mradi wa Khilafah ya Kiislamu na inayotawala kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameteremsha. Kwani Mwenyezi Mungu atakuuliza kuhusu msaada kwa Dini Yake na atakuhesabu kwa kuachana kwako kwa haki yake.

((إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ))

"Hakika, wale waliokufuru hutoa mali yao ilikuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa; kisha yatakuwa juu yao majuto; na kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal: 36]

Abdul-Mumin Az-Zaila'i

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu