Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kazi ya Kisiasa Juu ya Msingi wa Uislamu ni Wajibu wa Kisharia na Hitajio Muhimu la Maisha

(Imetafsiriwa)

Siasa muda wote imekuwa ni njia ya kuwaweka kando watu walio makini na waaminifu wanao sitasita kuchunguza fedha za umma. Watu wanashauriana wao kwa wao kujiweka kando na siasa ili wasije wakazama ndani ya matope yake na ndani ya ufisadi uliotapakaa.

Hakuna shaka kuwa kitovu cha siasa kwa hakika ni eneo lililojaa ufisadi, na mandhari inayoitawala iko mbali na Dini na maadili mema na imetawaliwa na ufisadi, fikra ya kuangalia faida na manufaa tu.

Lakini kujiweka kando na siasa sio suluhisho. Karibuni tumetoka katika janga la maradhi ya maambukizi, tuliambiwa wakati huo kwamba, kaeni majumbani, msijiangamize kwa virusi bila kujitambua. Mbora kati yetu ni yule anaekosha mikono yake kwa sabuni na maji mara tatu kwa siku. Ilikuwa wazi kwetu wakati huo udhaifu wa mfumo wa sekta ya afya na kushindwa kwake kutoa vitu vya msingi kwa matibabu. Leo tupo hapa, tunaishi ndani ya siku hizi ziliozongwa na mzozo wa kiuchumi ikiwa ni matokeo ya upunguaji mkubwa wa thamani ya fedha na upandaji mkubwa wa bei za bidhaa, na kupelekea ugumu mkali wa maisha na watu wengi kuteseka. Pamoja na hayo pia, maangamizi ya kijamii, yanayotokana na kushajiishwa ufisadi na kutetewa wazi wazi kwa ubaradhuli na kuoza kwa maadili. Hali hizi bila shaka ni matokeo ya njama haribifu na sera zilizofeli au sera zinazoweka maslahi ya wanasiasa na wafanyi biashara juu ya maslahi ya watu.

Imekuwa wazi kwa kila mtu kuwa kuiwacha nyanja ya siasa kwa mafisadi, na fikra ya uwongo ya kwamba maisha yanaweza kuendelea kuwa tulivu hata kama watu wenye busara wakijiweka mbali na siasa ni udanganyifu mkubwa. Leo tunalipa gharama kubwa kwa uwongo huu. Wakati upatikanaji wa mahitaji muhimu ya msingi (makaazi, chakula, elimu, usafiri, matibabu) yamekuwa yakihodhiwa na wachache katika jamii, wasiozidi asilimia kumi, tunatambua kwa kiasi gani tumepotoshwa. Na kwa kuhifadhi akili na maadili ya watoto wetu kuwa ni mzigo mzito unaotia wasiwasi familia, tunafahamu uzito wa hali hii. 

Kuingia katika siasa hivi leo imekuwa ni jukumu, takriban ni fardh ‘ain (faradhi ya lazima kwa kila mtu), na sio anasa ya wasomi au jambo la kipote cha tabaka fulani. Umasikini unaomnyemelea kila mtu, na ufisadi unaomlenga kila mtu, na milima ya majanga yanayobebwa na kila mtu na yaliotuzunguka kila kona, yanamhitajia kila mtu kufikiria upya kwa umakini kile kilichotuzunguka; katika upande wa kiuchumi, kisiasa na nidhamu za kijamii zinazotumika juu yetu, katika vipaumbele, katika misingi ambayo mahusiano ya ndani na nje yanapaswa kujengwa, katika nidhamu za sheria na jinai, katika elimu na vyombo vya habari, katika vigezo kwa ajili ya kuchagua wanasiasa… katika kila kitu.

Hakuna shaka kuwa kazi hii sio rahisi, na hakuna shaka kuwa hili sio jambo ambalo watu wote wanaliweza, lakini kwa upande mwengine, haihitajiki kwa kila mtu kugeuka kuwa mwanafikra na mchunguzi, lakini kila mtu anatakiwa kuishutumu hali hii na mara moja kujiepusha na mafisadi waovu ambao ndio sababu ya kuwepo hali hii. Wasiwaunge mkono, hata ikiwa kwa maneno, na waungane na wale wanaowaona wana wema na uwezo wa kutoa tiba muafaka. Mtume (saw) amesema: 

«إِذَا عُمِلَتْ الْخَطِيئَةُ فِي الْأَرْضِ، كَانَ مَنْ شَهِدَهَا فَكَرِهَهَا كَمَنْ غَابَ عَنْهَا، وَمَنْ غَابَ عَنْهَا فَرَضِيَهَا كَانَ كَمَنْ شَهِدَهَا»

Mtume (saw) amesema: “Pindi uovu ukitendwa katika ardhi, yule aliyeushuhudia na kutoridhia juu ya uovu huo, huwa ni kama asiyekuwepo, na kwa yule asiyekuwepo na akauridhia atakuwa kama aliyeushuhudia.” [Sahih Al Jami’ kwa Al-Albani, Hassan].

Uislamu umetufundisha kuwa siasa ni kushughulikia mambo ya watu, kuwahudumia na kusimamia mambo yao, na bila shaka hilo ni jambo la daraja la juu na tukufu na sio jambo la kifisadi na chafu kama inavyoonyeshwa na kufanywa na masekula, vyenginevyo Mitume wasingejishughulisha nalo, Mtume (saw) amesema:

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ، قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ، وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ الَّذِي جَعَلَ اللَّهُ لَهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Walikuwa Banu Isra'il siasa zao zikiongozwa na Mitume. Kila Mtume anapofariki hufuatiwa na Mtume mwengine; lakini hakutakuwa na Mtume baada yangu bali kutakuwa na Makhalifah na watakuwa wengi. Maswahaba wakasema: Basi unatuamrisha nini (kutapotokea Makhalifah zaidi ya mmoja)? Mtume (saw) akasema: “Wapeni bay’ah mmoja baada ya mwengine na wapeni haki zao (yaani watiini) ambazo Mwenyezi Mungu amewapatia, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya alichowatawalisha.” [Sahih Al Jami’ kwa Al-Albani].

Tunapozungumzia juu ya kuingia kwenye kazi za kisiasa kuwa ni jukumu la Kisharia na hitajio muhimu la maisha, bila shaka hatumaanishi katika kuingia kwenye vyama vya kisiasa ambavyo vimeundwa na kudhaminiwa na tawala zilizopo kuendeleza na kuunga mkono hali iliyopo. Hatumaanishi kushiriki katika michezo ya chaguzi ambayo huzipatia uhalali tawala ambazo tayari zimeshafeli. Badala yake, tunakusudia kuingia katika vyama vya kimfumo vinavyobeba fikra iliyokamilika na ya kivitendo vinavyotokana na Shariah, juu ya dola, vyombo vyake na namna vinavyofanya kazi. Bila kazi hii, hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana, bali juhudi zitakwisha, muda utapotea, na kupatikana misiba na mazito zaidi.

Tokea miaka ya 1950, Hizb ut Tahrir imetayarisha fikra ilio wazi na kamili ya dola inayotokana moja kwa moja na hukmu za Shariah, inayoanzia na katiba na kupitia katika vyombo mbali mbali vya dola na nidhamu; vitabu hivi vinapatikana kwenye mitandao yake kwa wale wanaotaka kuvisoma. Tokea mwanzoni, Hizb ut Tahrir imekuwa ikiwalingania Waislamu kuungana nayo na kuiunga mkono katika muendelezo wa kazi zake za kuirejesha njia kamili ya maisha ya Kiislamu ili kuwatoa kutoka hali ya chini kabisa ambayo wafuasi wa ukoloni wameiweka, na kuwaweka tena kwenye nafasi yake stahiki ya uongozi iliyoporwa kwa karne kumi. Kazi hii imepiga hatua kubwa, kwa rehema za Mwenyezi Mungu (swt), na mwamko wa leo wa Waislamu juu ya umuhimu wa Dola ya Khilafah unaikumba mitaa ya Rabat hadi Kuala Lumpur.

Basi njooni kwenye utukufu wa dunia hii na furaha ya Akhera. Njooni kwenye kile kitakachokupeni maisha mazuri na ya furaha, itayokulindeni na kukuhifadhia heshima yenu kutokana na upotovu wa waovu.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Abdullah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu