Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

COP26: Jinsi Warasilimali Wanavyougeuza Uchafuzi wa Mazingira Kuwa Faida

(Imetafsiriwa)

COP26 itazihimiza nchi 195 kutekeleza ahadi walizotoa walipokuwa wakikubaliana juu ya Mkataba wa Paris wakati wa COP21 mwaka 2015. Moja ya malengo muhimu zaidi ya mkataba huu ilikuwa ni kupunguza kiwango cha cha chafuzi zenye kudhuru - haswa CO2, ambayo ndio mada ya makala haya - ili kushusha kiwango cha joto duniani chini ya 2C na kukidhibiti hadi 1.5 C, ambapo wanachukulia kama sababu kuu ya mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake mbaya.

Njia ya kufikia malengo yao madhaniwa ni kama inavyotarajiwa ya kirasilimali tu. Katika siku ya kwanza ya COP26, Mwanamfalme Charles kwa mfano alisema, "kuweka thamani kwenye kaboni, na hivyo kufanya ufumbuzi wa kukamata kaboni kuwa wa nafuu zaidi, ni muhimu mno", wakati akitoa wito wa hatua "ili kukabiliana na kaboni iliyoko angani tayari". Vile vile chansela wa Ujerumani, Angela Merkel alitoa wito wa "kutabanniwa kwa bei ya kaboni duniani" ili kushajiisha mabadiliko ya nishati safi. Ni wazi kwamba COP26 ni ukumbi wa biashara, ambapo mazungumzo ya bei yapo mezani kwa bidhaa mpya ya kirasilimali "CO2".

CO2 ni bidhaa ya aina gani na inauzwa katika soko gani?

Msingi wa kuunda mikopo ya kaboni uliwekwa katika Itifaki ya Kyoto na Mpango wa Biashara ya Uzalishaji Gesi wa EU (EU ETS). Nchi zote, zilotia saini maamuzi ya COP, kama vile Mkataba wa Paris, zinalazimika kuweka kikomo kwa kiasi cha gesi chafuzi zitakazotolewa kwenye anga. Iwapo kampuni itavuka kikomo cha uzalishaji uliowekwa, ni lazima inunue au itumie mikopo iliyohifadhiwa ili kukaa chini ya kiwango cha juu cha uzalishaji. Ikiwa kampuni itasalia chini ya kiwango hicho, inaweza kuokoa au kuuza mikopo hiyo. Hili linajulikana kama soko la "cap-and-trade". Kwa hivyo CO2 imekuwa bidhaa, ambayo bei yake inafafanuliwa kulingana na kanuni za "Ugavi na Mahitaji". Hii ina maana, kwamba mikataba hii ya hali ya hewa na COP kimsingi huunda msingi wa kisheria wa kuzipa kampuni haki za mali ili kuchafua, yaani, haki ambayo inaweza kupatikana na kuuzwa na kampuni za kibinafsi!

Ukweli ni kwamba; Tani 1 ya carbon dioxide iliyoondolewa kwenye anga inauzwa kama "deni la kaboni" na kuuzwa kwenye kile kinachojulikana kama "soko la kaboni". Kulingana na Ecosystem Marketplace [ii], iliyotolewa mwezi Mei 2021, takriban masoko 64 yaliyo afikiana na kanuni za kaboni sasa yanafanya kazi kote ulimwenguni, ambapo bei ya kaboni ilizalisha $53 Bilioni katika mapato mwaka wa 2020-21. Masoko makubwa zaidi ya yaliyo afikiana na kanuni za kaboni yako katika Muungano wa Ulaya, China, Australia na Canada.

Kama vile masoko mengine, soko la kaboni hutumia utaratibu wa usambazaji na mahitaji kwa kiwango chake kamili, yaani, kampuni ambazo zina ziada ya hisa za CO2 huuza kwa kampuni zingine zinazozitumia kuongeza uchafuzi wa mazingira. Kwa hivyo kuwekeza katika teknolojia mpya za kupunguza uzalishaji wa kaboni hakutapunguza utoaji wa kaboni.

Soko la kaboni linaimarishwa kupitia sera mbalimbali, kama vile Mbinu Safi za Maendeleo (CDM), ambazo zilifafanuliwa katika Itifaki ya Kyoto, ambayo zinafafanuliwa kwa upotoshaji kama mradi wa kupunguza uzalishaji katika nchi zinazoendelea. Ingawa katika hali halisi CDM huruhusu nchi zilizoendelea kiviwanda kuongeza hisa zao za CO2 kupitia ununuzi wa mikopo ya CO2, ambao wana njia muhimu (za kifedha na kisiasa) za kuongeza viwango vyao vya CO2 kupitia ununuzi wa mikopo ya CO2 kutoka nchi zinazoendelea. Kwa hivyo, badala ya kupunguza uchafuzi wa mazingira, wanatayarisha njia kwa kampuni hizi kuendelea na uchafuzi wa mazingira. Mfano kama huo ni kiwanda cha kemikali katika jimbo la Gujarat nchini India, kinachomilikiwa na Gujarat Fluorochemicals Limited, ambacho msingi wake mkuu uko London na sehemu ya miradi ya "kijani" ya UN. Kiwanda kiliuza madeni yake ya kaboni kwa wachafuzi wa Ulaya, ambayo haijasababisha kupunguzwa kwa uzalishaji si nchini India wala katika EU. Zaidi ya hayo kiwanda hiki kilichafua maji katika eneo jirani kiasi kwamba hayanyweki. Maji hayo sasa yanajulikana kama maji ya kifo. Kutokana na hayo, mavuno yameharibiwa na maeneo ya karibu ya ardhi hayalimiki tena.

Athari nyingine ya mfumo huu wa mikopo ya kaboni ya Cap-and-Trade ni kwamba viwanda vichanga (ikilinganishwa na vile vya Magharibi) vinakabiliwa na matakwa ya nchi za Magharibi kupunguza utoaji wao wa kaboni kwa kutia chumvi tathmini ya hisa. Kwa hivyo, wanalazimika kuzuia sekta yao na ustawi wa kiuchumi ili kubaki ndani ya viwango vyao vya CO2 vilivyowekwa. Maendeleo ya sekta, hata hivyo, yanahitaji kuongezeka kwa uzalishaji wa viwanda, ambapo inajumuisha kuongezeka kwa uzalishaji wa kaboni badala ya kupungua. Inapozingatiwa kuwa sehemu kubwa ya nchi zisizo za magharibi, zikiwemo nchi za ulimwengu wa Kiislamu, hazina viwanda halisi, maendeleo yao yatazuiliwa moja kwa moja. Zaidi ya hayo watalazimika kuuza hisa zao za CO2 kwa nchi zilizoendelea - na matokeo mithili ya India. Matokeo yake ni kuongezeka kwa uzalishaji wa madhara kwa gharama ya binadamu na maumbile kulingana na mahitaji na matakwa ya Magharibi.

Zaidi ya hayo ni lazima mtu ajue kwamba mfumo wa cap-and-trade uliundwa kwa makusudi ili kuongeza gharama ya kawi. Chini ya mgogoro wa sasa wa kiuchumi, sera ghali ya kawi haina tija kwa biashara ndogo ndogo na watumiaji. Hata hivyo hilo halina umuhimu wowote kwa serikali za kirasilimali, kwani zitapata ongezeko la ziada la mapato ya serikali kupitia biashara ya kaboni. Kando na hili inadaiwa kuwa kupunguzwa kwa matumizi ya umeme ya watumiaji kutapunguza utoaji wa kaboni unaosababishwa na umeme. Maoni mafupi ya ziada: Ng'ombe wanatuhumiwa kuwa chanzo nambari 1 cha kilimo cha gesi chafuzi duniani kote. Kwa hivyo warasilimali wanadai kupunguzwa kwa mifugo, na badala yake kuwabadilisha kwa mkutano bandia ili kulea wanadamu. Majaribio haya duni yanasaidia tu kufinika unafiki na ulafi wa wanasiasa na kampuni za kibepari za Kimagharibi.

Kwa kumalizia, masuluhisho na makubaliano ya kimagharibi yaliyowekwa kama majibu kwa tatizo la hali ya hewa si chochote bali ni hakikisho kwa kampuni za Kimagharibi kwamba hali ya hewa na mazingira haziwi ni kikwazo kwa ukuaji wao wa kiuchumi na kufikia faida. Tunapaswa kujikumbusha kuwa kimsingi ni uroho wa mabepari ndio uliosababisha mgogoro wa mazingira.

Zaidi ya hayo ni dhahiri, hakuna nafasi ya kufikia maelewano endelevu kati ya mahitaji ya mwanadamu na uzuri na neema zilizoumbwa kwenye sayari hii, isipokuwa kwa kurudisha hukmu kwa Yule aliyeziumba zote mbili. Na ni mfumo wa Uislamu pekee, utakaotabikishwa chini wa chini ya utawala wa Khilafah, ndio ulio na uwezo wa kuumaliza mfumo wa kirasilimali wa kiulimwengu.

#أزمة_البيئة     #EnvironmentalCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu