Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mashirika ya Misaada ya Kibinadamu Hatimaye Yalazimika Kujifinika Barakoa Zao Mbele ya Wanawake na Wasichana wa Kiislamu wa Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Afisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 10 Januari 2022, iliibua wasiwasi kuhusu hali ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan. OCHA ilisema wasichana na wanawake wa Afghanistan wananyimwa haki za kimsingi: “Haki za kimsingi za wanawake na wasichana wa Afghanistan zinashambuliwa”. Pia ilisema wanawake na wasichana wa Afghanistan wanahitaji msaada wa Umoja wa Mataifa na mshikamano kwa sasa kuliko hapo awali. Takriban wanawake na wasichana milioni 11.8 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Kwa mujibu wa afisi hiyo ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kibinadamu lazima yalenge kuongeza msaada kwa wanawake na wasichana kwa kutoa chakula, huduma za afya, elimu na fursa za maisha na huduma za usalama.

Swali ni kivipi iaminike kuwa OCHA na Umoja wa Matiafa na mashirika mbali mbali na mataifa mengine yanajali sana wanawake na wasichana wa Afghanistan? Kwani hawakuivamia Afghanistan miaka 20 iliyopita ili kuwasaidia wanawake na wasichana? Ukweli unaonyesha kuwa, hawakusaidia chochote kwa wanawake na wasichana wa Ummah huu katika miaka ya hivi karibuni isipokuwa misingi mibovu ya kidemokrasia Iliyo wahujumu wanawake wa Afghanistan katika ngazi ya kisiasa kufuatiwa na hali mbaya ya kiuchumi na njaa pamoja na fursa duni za kielimu, ukosefu wa huduma za afya na hali ya usalama isiyoweza kuvumilika nchini. Mwanasiasa wa kigeni Jurgen Trittin alielezea hali yao wenyewe nchini Afghanistan vizuri aliposema “tunakabiriana na kushindwa kwa pamoja”.

Ukweli kuhusu Afghanistan ni kwamba kadi zote zimefichuliwa sasa. Inatosha sasa kwa msaada wa bandia na mahusiano na mashirika ya kinafiki ambayo yanataka kurudi tena kucheza mchezo wa kujifanya walinzi wa wanawake na wasichana wa Kiislamu nchini Afghanistan. Baadhi ya mambo yalioorodheshwa hapa chini yanaonyesha ni nini hasa huwasaidia wanawake wa Kiislamu Afghanistan na duniani kote:

1. Wanawake na wasichana wa Kiislamu nchini Afghanistan na duniani kote, kamwe hawataweza kulinda utu wao, usalama na heshima yao kutoka kwa mashirika haya yenye kujali maslahi au mataifa katili. Wanawake wa Kiislamu wanahitaji dola ya kweli ambayo inawaheshimu pamoja na kuwalinda inavyopaswa. Katika ibara ya 108 ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah ya Hizb ut Tahrir, imetajwa kwamba wanawake ni heshima ambayo lazima ilindwe. Ni sheria gani ya serikali za kileo inawapa wanawake kipaumbele hiki na kumsifu kama heshima ambayo lazima ilindwe? Shirika la afya duniani WHO lilipoti kwamba karibu mwanamke mmoja kati ya watatu wapatao milioni 852 ulimwenguni kote, wanakabiliwa na unyanyasaji katika maisha yao yote. Kwa hivyo haya ni matokeo ya juhudi za dola na mashirika haya hivyo watawezaje kuwasadiia wanawake wa Kiislamu? 

2. Wanawake wa Kiislamu wanahtaji dola ambayo inahakikisha haki sawa kwa raia wake wote, awe mwanamume au mwanamke, na kushughulikia masuala yao bila kubagua au kuwaona kuwa wao ni duni. Katika ibara ya 6 ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah imeandikwa kwamba raia wote wa dola watashughulikiwa kwa haki na usawa bila kujali dini, rangi au jambo lolote lile. Serikali imekatazwa kuwabagua baadhi ya raia wake katika mambo yoyote ima ya kiutawala au kimahakama au katika kushughulikia mambo yao. Wanaharakati wa haki za wanawake wanalia kwa miongo kadhaa dhidi ya ubaguzi wa haki za raia wanawake, na jambo hili kamwe haliwezi kufikia kikomo chini ya sheria mbovu za kidemokrasia. Kwa hivyo Umoja wa Mataifa uzingatie vyema wanaharakati wanaolia badala ya kutafuta suluhu kwa wanawake wa Afghanistan kuwarudishia haki zao za msingi. Ni kwa sheria tukufu ya Uislamu pekee, kunyimwa kwa wanawake wa Kiislamu haki zao walizopewa na Mungu hatimaye kutafikia mwisho.                                                                                                  

3. Mamilioni ya wanawake wa Kiislamu duniani kote wanaishi mitaani, au wanalazimishwa kuwa ombaomba au kuuza miili yao ili kupata chakula cha watoto wao. Wanahitaji serikali ambayo inawapa usalama wa kifedha na inaweza kuwaokoa kutokana na maafa haya yote. Katika ibara ya 152 ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah, imetajwa kuwa Khilafah itamdhaminia gharama za maisha kwa yule asiyekuwa na fedha, asiyekuwa na kazi wala jamaa anayewajibika na matunzo yake ya kifedha. Serikali inawajibika kuwahakikishia makaazi na kuwasimamia watu wasiojiweza na wenye ulemavu. Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa asilimia 70 ya watu masikini duniani kote ni wanawake. Je? Inawezekanaje kwamba mashirika kama vile Umoja wa Mataifa hayawezi kupata suluhu kwa wanawake masikini duniani kote. Je? Yanaweza kuwasaidia wanawake wa Afghanistan na kwengineko katika hali mbaya ya kiuchumi?

4. Wanawake wa Kiislamu pia wanahitaji huduma bora za matibabu. Wanateseka na kufa kwa ajili ya magonjwa yanayoweza kuzuilika au kutibika na ukosefu wa dawa, lakini hakuna serikali ambayo inaweza kutatua shida zao za kiafya. Ulimwengu na mashirika ya misaada wanaona tatizo hili lakini hawawezi kulitatua. Mara nyingi huwatumia tu dawa zilizo kwisha muda wake na zilizopitwa na wakati ili kuonyesha huruma yao. Lakini wanawake katika nchi za Kiislamu wanahitaji serikali inayowapa huduma za afya bure za kitaalamu na za kibingwa na za hali ya juu, serikali ambayo inajali kikweli hali ya afya za kina mama na mabinti wa Ummah. Ibara ya 160 katika Rasimu ya Katiba ya Dola Khilafah inataja kuwa serikali inatoa huduma za Afya bila malipo kwa wote. Hili litakuwa ni jukumu la dola ya Khilafah na sio chaguo wala upendeleo kwa wanawake wake. 

 5. Je, UN na mashirika mengine yataweza kuwapatia wanawake na wasichana wote wa Afganistan na kwingineko elimu bora? Takwimu zinatuonyesha vinginevyo na kwamba kwa miaka mingi wameshindwa vibaya katika eneo hili. Khilafah pekee ndiyo inayoweza kuhifadhi haki hii kwa wanawake wa ardhi ya Kiislamu kwa sababu katika Khilafah, elimu ni moja ya haki za kimsingi ambazo dola inawajibika kutoa kwa kila raia wake - wanawake na wanaume. Ibara ya 173 ya Rasimu ya Katiba ya Khilafah inaeleza kwamba ni wajibu wa dola kumfundisha kila mtu mwanamume au mwanamke mambo yale muhimu kwa maisha ya kawaida. Hili liwe faradhi na litolewe kwa uhuru katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari. Serikali inapaswa kwa uwezo wake wote, kutoa fursa kwa kila mtu kuendelea na elimu ya juu bila malipo.

6. Kwa kifupi, ni wazi kwamba Umoja wa Mataifa, WHO na mashirika mengine ya kibinadamu lazima zijifinike barakoa zao na kujifanya wanataka kuwasaidia wanawake na wasichana wa Afghanistan na nchi nyingine za Kiislamu kwa kutoa vyakula, huduma za Afya, Elimu, fursa za maisha na ulinzi kwa sababu wao hawana uwezo wa kufanya hivyo na dunia nzima imekuwa shahidi kwa kushindwa kwao nchini Afghanistan, ardhi ya Kiislamu na dunia nzima katika kupata maisha ya heshima na salama kwa wanawake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Taharir na

Amanah Abed

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Taharir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu