Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Dhoruba Inayokuja: Kutoka kwa Uingereza Katika EU

Uingereza imetoka rasmi katika Muungano wa Ulaya katika siku ya mwisho ya Januari lakini utokaji umezusha changamoto nyingine nyingi, ambazo zitaharakisha kuvunjika kwa Umoja wa Ulaya. Kwa sasa kuna kipindi cha mpito ambapo Uingereza na EU zitakuwa zikijadiliana mipangilio ya ziada, hata hivyo, masuala kadhaa yanajitokeza kuhusiana na mpango mpya wa biashara baina ya Uingereza na EU. Uingereza bado inapendelea kuendeleza mpango huru pamoja na Muungano wa Ulaya na kujionyesha kwa madaha uwazi wake mpya kwa ulimwengu hasa kwa hivi sasa ambapo ina sauti juu ya kanuni na viwango.

Msimamo wa nchi juu ya muungano umejengwa juu ya misingi minne. 1) Uingereza muda wote imekataa lengo la muungano wa kisiasa ndani ya EU. 2) Uingereza inaunga mkono biashara huru tu pamoja na EU. 3) Uingereza inapendelea sera za kigeni na usalama nje ya mpangilio wa Ulaya. 4) Uingereza mara chache haijapatiliza ushawishi wake ndani ya EU. Hata baada ya Uingereza kutoka rasmi, lakini bado inataka kuendeleza makubaliano huru, hii inaonyesha namna Uingereza inavyojali ustawi wake binafsi kwa kuwa maslahi na madhara ndio vigezo vikuu vya utowaji wa maamuzi. Na kwa kuwa Uingereza muda wote imekuwa ni yenye kuuchukia Muungano wa Ulaya, Donald Trump ametumia hisia hizi za husuda za Uingereza kuuyumbisha Muungano wa Ulaya na hadi sasa, zinafanya kazi.

Kutoka kwa Uingereza kumesababisha tatizo kwa bajeti ya EU, kwa kutoka kwake kumesababisha mzigo kuhamia juu ya nchi nyingine ndani ya Muungano wa Ulaya. Kutoka kwa Uingereza kumeacha pengo la kifedha kuzibwa kwa kiasi cha Uro bilioni 12. Nchi nyingi za Mashariki na Kusini ya Ulaya hazitaki kuongeza michango yao, hivyo, mzigo wa kujaza pengo hili la kifedha limeelemea juu ya nchi tajiri jirani ndani ya EU. Kutoka kwa Uingereza kumewacha fursa ya ushindani kwa Ufaransa na Ujerumani kuibuka ndani ya EU, ambapo Ujerumani inataka kuweka kiwango cha mchango kufikia asilimia 1 ya ziada wakati Emmanuel Macron anataka kumwaga fedha kwa kujionyesha.

Sababu ya kuwa mataifa ya EU hayataki mzigo wa uingizaji fedha ni kwa sababu nchi zao bado hazijapata afueni kutokana na mgogoro wa kiuchumi wa 2008, ambapo Uro (sarafu ya nchi za Ulaya) imezuia mataifa mengi ya Kusini na Mashariki ya Ulaya kufikia kuwa na afueni, kwa hivyo, tayari zimeshakuwa na mzigo wa kitaifa zilizojifunga nao. Kutokana na kuwa na sarafu ya pamoja, nchi zote ndani ya sarafu ya pamoja zimeondoa umiliki juu ya viwango vya riba. Uhakika ni kuwa kila nchi ina malengo yake ya kisiasa ndani ya EU na hali ya kiuchumi kwa kila nchi unatofautiana kwa kiasi kikubwa, na sarafu ya pamoja ya Uro haisaidii katika kutatua masuala haya yaliyotofautiana. Hii ndio sababu kwa nini nchi kama Uhispania, Ugiriki, Ureno, Italia, na nyingine nyingi zimebaki kuwa dhaifu. Kwa hakika, umoja wa sarafu ya Uro hatimaye umeinufaisha Ujerumani. Ujerumani hadi leo imetawala Ulaya bila kutumia risasi hata moja kutokana na sarafu ya Uro. Ambapo nyingi ya bidhaa zinazosafirishwa ndani ya EU zinatokea Ujerumani. Ujerumani ndio nchi iliyo na dhamira zaidi kudhibiti hali bora ya EU na sarafu ya pamoja ya Uro kwani inataka kubakisha nafasi yake ya kuwa ni kituo cha nguvu ya kiuchumi ndani ya bara.

Ujerumani imekuwa ni mchangiaji mkubwa zaidi wa EU kwa kiwango kinachofikia asilimia 20.78. Ya pili ni Ufaransa asilimia 15.58 na mchango wa Uingereza haupo tena, Italia hivi sasa inalipa 11.78 kuifanya ni mchangiaji wa tatu mkubwa, kwa hivyo Italia inahitaji nafasi inayostahiki kwani haikuamiliwa kwa haki ndani ya EU. Hili limezusha tumbo joto kwa Ujerumani, kwani ikiwa inataka kubakisha nguvu zake ndani ya EU inahitaji kuongeza mchango wa matumizi yake, ambapo ni vigumu kwani nchi yake iko katika ukingo wa mdororo wa uchumi, unaoweza kuenea kote katika eneo la Muungano wa Ulaya kwa kuathiri Uhispania, Ufaransa, Uholanzi na nchi nyingine nyingi. Kujitoa kwa Uingereza kumesababisha kutokea mbadiliko ndani ya uzani wa nguvu katika Ulaya hivi sasa. Hivyo, mashindano ya Ufaransa na Ujerumani yanaweza kuharakisha hali ya kutaka ubwana ndani ya bara.

Ufaransa muda wote ikitaka kurudisha nguvu kupitia Ulaya kurejesha nafasi yake ya ubeberu mkongwe.  Ujerumani kwa upande mwingine inataka kujikomboa kupitia Ulaya ili kufuta damu iliyopita, na wakati huo huo kujenga dhima mpya ndani ya Ulaya. Hivyo, EU ni muhimu sana kwa Ufaransa na Ujerumani kutaka na kushikilia malengo yao. Vile vile, kwa usalama wa Ujerumani na Marekani ni muhimu ili kupunguza wasiwasi miongoni mwa mataifa katika bara, kwani Ujerumani haiwezi kukuza nguvu za kijeshi kwa sasa na kuendelea kutokana na ukatili wake hapo nyuma kwa kuwa usalama wa Ujerumani na Amerika ni muhimu. Ufaransa kwa upande mwingine, linapokuja suala la usalama inabakia kuwa kaidi na kusita kutegemea usalama wa Amerika. Hii ndio sababu ya kwa nini de Gaulle alijiondoa katika muundo wa uunganishaji wa kijeshi wa NATO mwaka 1967, ambapo Ufaransa baadaye ilirejea 2009. Tamko la Macron la kifo cha NATO kinaonyesha uwazi thabiti kwa Ufaransa, ambao upo hadi sasa.

Tokea Donald Trump kuingia White House, Amerika imekuwa ikisaidia kujitoa kwa Uingereza katika EU ambapo imeleta hali ya kutokuwepo utulivu na kupinga harakati za EU ndani ya bara. Donald Trump amemtumia Steve Bannon kuleta siasa kali kote Ulaya kutengeneza njia kwa utaifa na kujenga msingi kwa siasa za ummah za mrengo wa kulia. Trump ameibambikiza EU ushuru na ilhali macho yake yanamkodolea Angela Merkle wa Ujerumani. Rais wa sasa amesababisha hisia zaidi dhidi ya Amerika kwa Ulaya kuliko Rais mwingine yeyote katika historia. Wakati huo huo, Trump amepata uungwaji mkono mkubwa Ulaya-lakini kutoka kwa makundi ya wenye mrengo wa kulia. Trump ni mwenye fikra za kibiashara, ambapo hutaka kuigawa Ulaya na kuzuia ukuaji wa kiuchumi wa Ujerumani, na pia jitihada za mbeleni za Ufaransa za kuendelea daima katika kukuza uhuru wake wa kijeshi kwa Amerika. Trump anataka kuvunja mtegemeano ndani ya EU ili kuimaliza, wakati huo huo akiisihi Ulaya kuongeza “kibarua kigumu” ndani ya Ushirikiano wa Kaskazini (NATO).

Moja ya sababu ya Trump kuvunja makubaliano ya JCPOA mwanzoni, ilikuwa ni kuharibu biashara ya Ulaya pamoja na Iran. Trump hivi sasa ametishia ushuru wa asilimia 25 kwa Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani kama hazitotekeleza vita vya kidiplomasia dhidi ya Iran. Aliwaagiza washirika wanaoiunga mkono Amerika Mashariki ya Kati kumsaidia Haftar (anaeungwa mkono na Amerika) kwa ajili ya kuidhoofisha Ulaya katika Tripoli. Amerika inapendelea Ulaya itakayo beba majukumu zaidi wakati huo huo kuzuia fursa yoyote kwa Ulaya kuwa huru na utegemezi wa kijeshi wa Amerika. Ni ukweli kabisa kuwa Amerika haina rafiki yeyote, hata pia Uingereza. Hii ni kwa sababu mtazamo wa Amerika kwa ulimwengu ni ule wa nadharia ya Hobbesian kwa maumbile yake. Japokuwa Uingereza inajaribu kukazia mshikamano wake na Amerika baada ya kutoka EU, hata hivyo, Amerika kwa upande mwingine haikusudii hilo. Hii ni kwa sababu Amerika inaelewa mvutano wa Uingereza na Marekani uliopo tokea 1941. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwa Amerika kuchukuwa hatua kali dhidi ya Uingereza katika wakati ujao kwak uwa Uingereza imeshavunja mahusiano yake na EU, kuiwacha Amerika kuwa ni tegemeo lake pekee.

Majaribio yote ya Ulaya yameshindwa, ambapo Ulaya imejaribu kuwa pale isipokuwepo. Dhoruba inayokuja inaweza kuwa na athari mbaya kwa bara la Ulaya kutokana na mbadiliko wa sasa katika uzani wa nguvu. Kwa upande wa Amerika, inataka kutwaa kiasi kikubwa zaidi cha ushawishi ndani ya Ulaya, na pia kuidhoofisha kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya manufaa yake binafsi. Wakati Trump anataka kukuza ustawi wa Amerika huku akizuia wa wengine. Na hatimaye kudhibiti cheo chake ndani ya bara la Eurasia, kwa kuwafanya wengine kubeba mzigo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammed Mustafa

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:33

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu