Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mgogoro wa Kiuchumi wa Lebanon

Mgogoro wa sasa wa kiuchumi nchini Lebanon umefichua ulaji rushwa wa wanasiasa wenye kudharauliwa, mfumko wa juu wa bei za bidhaa, na unyonyaji wa wageni mabeberu ulioenea. Mbali ya ufichuaji wa wazi wa mfumo wa sasa, dola za kigeni na wawakilishi wao wanajaribu kwa uwezo wao wote kuielekeza nchi hii katika mageuzi yale yale ya kisiasa na kiuchumi, ambayo yameibomoa nchi mwanzoni. Ni muhimu kuchunguza namna ambavyo Lebanon ilijikuta ikiingia kwenye mgogoro huu na ni kitu gani Lebanon inahitaji kufanya ili kuielezea hali yake ya kushinda moja kwa moja.

Muundo wa benki wa Lebanon umejengwa juu ya uwekezaji wa kigeni usiodhibitiwa kuvutia uingiaji wa dola za Marekani nchini; hizi baadaye zinatumika kufanyia biashara katika soko la kimataifa. Kuna namna nyingi ambapo Lebanon huweza kufanikisha hayo. Ima kwa kupitia mikopo ya fedha kutoka Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), kuvutia uwekezaji wa dola kutoka nje au utumaji wa fedha kwenye benki za Lebanon kutoka kwa jamii za wazawa walioko nje. Lebanon pia hupata dola kupitia kusafirisha bidhaa nje; hata hivyo, uagizaji wake wa bidhaa umeyazidi mauzo yake ya nje. Kwa nchi dhaifu inayoendelea kama Lebanon kiwango kikubwa cha bidhaa zinazoingizwa huzalisha nakisi ya biashara inayoathiri uzalishaji wa kazi na kuongezeka kwa uchumi. Baada ya Vita vya Lebanon mwaka 2006, nchi ilianza kukopa kiwango kikubwa cha dolari za marekani kutoka IMF kwa kuagiza bidhaa muhimu kwa ajili ya hatua za ujenzi ili kusaidia kuijenga upya nchi. Kwa bahati mbaya, katika kipindi hiki kilichofuatiwa na Mgogoro wa Kiuchumi wa 2008, sarafu ya dola ilishuka thamani na kiwango cha riba kilipungua kwa kasi na kuifanya mikopo kuwa ya kuvutia.

Lebanon haina viwanda vya maana sana na ina bidhaa chache za kuuza nje (vito na madini ya thamani ni miongoni mwa bidhaa kubwa inazosafirisha). Muundo wa sarafu inayoegemezewa thamani ya sarafu nyengine ambapo nchi huweka kiwango maalum cha ubadilishanaji wa sarafu yake kwa sarafu ya nchi ya kigeni au mkusanyiko wa sarafu tofauti, huleta vizingiti vingi. Hii ni kwa sababu wakati sarafu inapoegemezewa dolari ya Marekani huwa inapungua thamani na kupanda kutegemeana na sarafu ya dolari. Hata hivyo, wakati sarafu inapoanguka thamani yake chini ya kiwango ilichoegemezewa, nchi inahitajika kuwa na Dhamana ya Hazina ya Marekani ya kutosha ili iuzwe na kuongeza thamani ya sarafu yake ili kuirejesha thamani yake ilioegemezewa. Hii hutokea kwa benki kuu ya nchi (Banque du Liban) kuuza Dhamana ya Hazina ya Marekani, ambayo inasababisha thamani dolari ya Marekani kushuka. Wakati Benki Kuu inapokea dolari kupitia uuzaji wa Dhamana ya Hazina ya Marekani, benki kuu ya nchi inaanza kununua sarafu za ndani kuongeza thamani yake. Njia hii huwa ni tatizo kwa kuwa nchi inayohitaji kubakisha uegemezaji huhitaji dola nyingi, ambazo kwa kawaida hupatikana kupitia mauzo ya nje. Lebanon kwa upande mwengine, haina dolari za kutosha kwani inaagizia zaidi ya inavyouza. Kwa hiyo, huwa ni vigumu kwa Lebanon kudhibiti utegemezaji wake kwa dola. Licha ya hayo, thamani ya dola huwa inayumba mfululizo kutokana na kuwa kwake ni sarafu ya akiba ya dunia.

Kutokana na uhaba wa dolari, nchi ilihitaji kuwa na sarafu za kutosha za ndani ili iweze kuendelea kununua dolari za Marekani, ambazo nchi inahitaji kwa haraka kwa ajili ya kuagiza bidhaa nje. Benki Kuu ya Lebanon ilianza kuchapisha fedha za ndani kwa wingi ili kununua dola za Marekani kwa kuwa Pauni ya Lebanon ni dhaifu sana kulinganisha na dolari. Matokeo yake, kuendelea kuchapa sarafu za ndani kumepelekea mfumko wa juu wa bei. Hivi sasa, watu wa kawaida hawawezi hata kupata mafuta katika vituo vya gesi kwa kuwa Pauni ya Lebanon imeshuka thamani kwa kiasi kikubwa ambapo manunuzi ya ndani yamekuwa ghali mno. Hivyo, umma umeanza kukimbilia kununua noti za fedha za nje kwani ndio zenye uwezo wa kununua bidhaa za ndani kwa ajili ya matumizi. Foleni zimeanza kwa haraka nje ya vibanda vya kubadilisha fedha nchini kote kununua dolari za Marekani bila mafanikio kwani dolari zimekuwa chache.

Kwa upande wa mikopo ya kigeni inayokopwa kutoka IMF inaiacha Lebanon kukaukiwa na dolari kwa kuwa fedha inayokopwa inatumiwa kwenye miradi ya ujenzi, utalii, na mali isio hamishika. Kwa hivyo, kuilipa IMF pamoja na riba maradufu kila siku huwa ni suala gumu kwani haitoweza kulipa deni halisi la mkopo – haikuwa ni chengine isipokuwa ni mtego wa madeni ambao unazuia mapato ya mbeleni.

Zaidi ya hayo, kutokana na kukosekana kwa mauzo ya nje ya kutosha, Lebanon haiwezi kuzalisha kiasi cha kutosha cha dolari za kulipa madeni ya IMF au kuzihifadhi kwenye hazina yake kwa ajili ya miamala ya kimataifa. Hivyo, Lebanon inalazimika kuregelea tena IMF kwa ajili ya mikopo zaidi, ambayo yanafungamanishwa na minyororo inayojulikana kama ni marekebisho ya kimuundo. Hali hiyo imesababisha hasira kubwa na mfadhaiko miongoni mwa watu wa Lebanon kwa kuwa nchi imelenga zaidi katika kuwalipa wadeni wake wa nje, na hivyo kupuuza uingizaji wa fedha zinazohitajika zaidi kwa matumizi ya ummah, kama sekta ya umeme ambayo imekumbwa na mbinyo mkubwa katika miaka ya karibuni kutokana na uingiaji wa wakimbizi wa Syria wanaoingia nchini.

Kuhusiana na uhifadhi wa fedha za nje, benki nchini Lebanon zimeanza kukopesha akiba zao za dolari kwa Benki Kuu ya Lebanon kwa lengo la kupata riba kubwa. Lakini suala linabakia, kwa kuwa hakuna dolari za kutosha za kuzilipa benki za biashara nchini Lebanon, au wakopeshaji wa kigeni au kwa manunuzi ya bidhaa za nje. Benki Kuu haiwezi kuhimili kuchapisha fedha kununua dolari za Marekani za kutosha kuzilipa benki za biashara nchini. Hivyo, muendelezo wa hatua kwa hatua na dolari kwa dolari, utambulisho tofauti ndani ya Lebanon, benki kuu, benki za kibiashara na sekta binafsi na za umma zimesambaratika kutokana na uhaba wa dolari na mzunguko wa deni, ambapo hatimaye inakuwa ni mdaiwa wa Amerika.

Gavana wa Benki Kuu ya Lebanon Toufic Salame, kwa maajabu amesisitiza juu ya kubakisha uegemezi wa dolari na kuonyesha upinzani wa kuiondoa Pauni ya Lebanon moja kwa moja kutoka katika muundo wa uegemezi wa dolari. Ukweli wa mambo ni kuwa ima Lebanon ibakishe uegemezi wake au iachane nao ambapo hilo halielekei – matatizo ya uchumi wa nchi yataendelea kuwepo kwani nchi itaendelea kuwaelekea mabeberu wa kigeni kwa usimamizi na urekebishaji wa kiuchumi. Na sababu ya Riad Salame kusisitiza juu ya kubakisha muundo wa uegemezi wa dolari ni kwamba yeye ni “mdunguaji mahiri” wa uchumi wa Amerika. Mwanzoni, Salame alifanya kazi kwenye kampuni ya Marekani ya kusimamia mali ya Merrill Lynch kabla ya kuwa gavana wa benki kuu ya Lebanon (Banque du Liban), na kwa wakati huo huo pia ni mwanachama wa bodi ya magavana wa IMF. Hivyo, itashangaza sana kuwa sera zake za uchumi wa jumla katika nchi usiwiane na maslahi ya Amerika.

Hali ilianza kubadilika zaidi wakati vikwazo vya Amerika vilipoanza kufanya kazi kwenye benki za Lebanon ambazo zinadhaniwa kushirikiana na Hizbullah. Vikwazo hivi ni sehemu ya kampeni ya shinikizo kubwa zaidi la Amerika, ambalo limeanza baada ya Trump kuingia Ikulu. Vikwazo vikali vya Amerika pia vilianza kuchochea athari ya hali ngumu zaidi ya uchumi wa Lebanon iliyo kuwepo kabla kwa sababu wawekezaji wa kigeni wameanza kupoteza uaminifu wa kuwekeza katika mabenki ya Lebanon na kupelekea ugumu kwa nchi kupata dolari za kutosha za kuagiza bidhaa kutoka nje. Hii imepelekea familia nyingi kutoweza kukidhi mahitaji yao ya msingi kwa sababu mahitaji ya bidhaa kutoka nje ni kiasi cha asilimia 85 ya chakula na bidhaa nyengine za matumizi. COVID-19 imeongeza tena kifo cha mfumo wa jamii wa kiuchumi wa Lebanon katika kiwango kipya kabisa. Marufuku ya matembezi (lockdown) ya serikali imepelekea kuzorota kwa ghafla kwa mzunguko wa fedha unaohitajika zaidi ndani ya uchumi ukipoteza uaminifu kwa walaji wa ndani.

Kwa upande mwengine, ulimbikizaji wa mali wa tabaka lenye utajiri mkubwa zaidi Lebanon likijumuisha wanasiasa mafisadi wanaosomba fedha kutoka kwenye mikopo iliojazana na hazina ya kigeni katika benki za ndani. Unafiki wa mataifa ya kigeni ya Wamagharibi umefichuliwa wakati yalipotaka uwazi kuhusiana na shughuli za serikali na mageuzi ya kimuundo. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya serikali imebaki kuwa chini ya udhibiti wa Amerika na iliobaki ikiwa chini ya mazingira ya ushawishi wa Ufaransa. Ukweli ni kuwa, taasisi za kibeberu za Amerika ambazo ni IMF na Benki ya Dunia, zimechangia moja kwa moja katika nafasi ya tabaka la matajiri na mafisadi ya orodha ya matajiri wakubwa wa Lebanon kwa kuimarisha nguvu za kikundi cha wanasiasa mafisadi ambao Amerika baadaye huwatumia kulinda maslahi yao. Wakati yote haya yakijiri wananchi wengine waliobaki wanaendelea kubakia katika shida. Mbali ya kuongezeka kwa nguvu ya wanasiasa mafisadi na wengineo wenye ushawishi kama akina Riad Toufic Salame, Amerika imewabana kwa kuifanya nchi ihangaike kupitia ugumu wa maisha, ambayo inainufaisha Amerika kwa kuendeleza udhibiti wake sio tu juu ya nchi lakini pia juu ya wanasiasa tegemezi ambao utajiri wao na nguvu zao zimebakia chini ya mikono ya Amerika. Wakati Amerika ilipoweka vikwazo vyake kwa benki za Lebanon zinazodaiwa kuwa na mahusiano na Hizbullah, Banki ya  Lebanese Canadian Bank na benki ya Lebanon’s Jammal Trust Bank, hazikupata upinzani wowote kutoka maafisa wa serikali, ambapo inaonyesha kiwango cha udhibiti na ushawishi ilionao Amerika kwa Lebanon ambapo Amerika inaweza kufanya ilitakalo bila ya upinzani wowote wa maana katika maslahi yake. Dai la kutaka uwazi halifikiwi kwani mipango ya Amerika ndio sababu hasa ya mfumo wa ufisadi uliopo leo Lebanon.

Suluhisho pekee kwa mgogoro wa Lebanon ni kusimamisha dola ya Khilafah, ambayo itaondoa kutoka Lebanon uwakilishi wa Wamagharibi na mipango ya kibeberu na kuiunganisha na ardhi nyengine jirani za Kiislamu. Kama Lebanon itaunganishwa tena na Syria na hatimaye, Syria kuunganishwa na Misri, umbo la Kiyahudi halitoweza kudumu zaidi ya wiki moja. Kwa kuwa kwake kitu kimoja kisichogawika, ardhi za Ash-Sham zitaweza kuunganisha rasilimali zao, na kuondosha utegemezi wao kwa mataifa ya kigeni, na sio kama hali ilivyo sasa ya mfumo wa dola za kitaifa unaozigawa ardhi za Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha katika Sura Anfal:

(وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ)

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamuwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” [TMQ Anfal:60]

Wakati huo huo, kusimamishwa kwa Khilafah kutabadilisha sarafu zinazopewa nguvu na tawala kwa viwango vya dhahabu na fedha, kuzuia kuyumba na kudhibiti thamani asili ya sarafu.

Khilafah pia itaziweka mali kuwa za binafsi, za umma, na za serikali. Sheria kama hizi za mali chini ya dola ya Khilafah itazuia ubinafsishaji wa kiwango kikubwa cha ardhi mbali mbali na rasilimali nyingi. Hatimaye, Dola itaweza kudhibiti aina tofauti ya mali na hivyo utajiri kuweza kugawanywa kote katika ardhi za Waislamu kinyume na (hali iliyopo) kuhodhiwa na kukusanyika ndani ya eneo moja. Mtume (saw) ametuelezea katika hadithi kuwa “Waislamu ni washirika katika (vitu) vitatu, maji, malisho na moto” [Sunan AbuDawud].

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 (وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُ)

“Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa walinzi wake, bali walinzi wake hawakuwa ila wacha Mungu tu. Lakini wengi katika wao hawajui”. [TMQ Al-Anfal:34].

Khilafah pia itaweka uchumi wa walaji wa ndani, ambapo hautategemea juu ya mauzo ya nje au kuagiza kutoka nje. Kwa kuwa mfumo wa biashara ya kimataifa umeegemea juu ya ubwana wa Amerika kwa nchi nyengine, kwa hiyo, ushiriki ndani ya mfumo wa kimataifa utapelekea kuwapa makafiri mamlaka juu ya waumini. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَٰؤُلَاءِ شَهِيدًا)

“Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa?” [TMQ An-Nisa:41].

Mwenyezi Mungu (swt) amemteremshia Mtume wetu Muhammad (saw) mfumo mzima wa maisha uliokamilika ambapo Waislamu hawatohitaji msaada kutoka kwa makafiri juu ya namna ya kuendesha mambo ya Waislamu. Hivyo, ili Waislamu waweze kushinda na kuondokana na pingu za udhalilifu wa Wamagharibi, vijana wa Ummah lazima watamani na kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha nidhamu ya Khilafah na wakati huo huo kuzuia mageuzi ya udanganyifu ya kikafiri kuingia katika ardhi zetu. Kwa kuhitimisha, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [TMQ Al Anfal: 24].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammed Mustafa

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 31 Agosti 2020 16:29

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu