Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ushuhuda wa Abdullah Haider Kuhusu Naveed Butt
#KnowNaveedButt
#FreeNaveedButt

(Imetafsiriwa)

Kwa kuwa ushuhuda wa Waislamu wanne wa wema wa Muislamu unatosha kumuingiza peponi, Naveed Butt ana ushuhuda kama huo kutoka kwa maelfu ambao wameingiliana naye kibinafsi.

Ni kuijulisha familia yake kwamba dua yetu ya dhati iko pamoja naye na wao na kwamba Mwenyezi Mungu hivi karibuni atawalipa ujira mkubwa kwa kujitolea kwao.

Ni kuwafahamisha pia waovu waliomteka nyara, kwamba Naveed Butt ni shahidi wa maovu yao, vilevile sisi na pia mamilioni ya watu katika Ummah huu. Naveed Butt ananikumbusha sehemu hii ya Ayah ya 35 kutoka Surah An-Nur

(يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ نُّورٌ عَلَى نُورٍ)

Yanakaribia mafuta kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa – Nuru juu ya Nuru.” [An-Nur: 35]

Nilimjua Naveed alipokuwa bado akichunguza mashirika na harakati kadhaa za Kiislamu kama mwanafunzi. Alipoipata Hizb ut Tahrir, nilimuona akiushika mwangaza kama Ayah hiyo ya juu inavyo elezea. Huu ndio moyo wa kiongozi wa kweli, wa kupambanua Haki, kuikubali kwa ujasiri na kusonga mbele nayo. Kwa kuongezea, Naveed alikuwa na ubora wa uelewa kuwaelewa vizuri watu aliokuwa akiingiliana nao na akilenga kubeba fikra zake ambapo ilimfanya kuwa mlinganizi aliyefanikiwa mno.

Nakumbuka mazungumzo naye ambapo tulikuwa tukijadili faida za kuhifadhi Quran kwa kadiri inavyowezekana kwa sababu itakuwa mwandani wetu, ikiwa tungefungwa gerezani katika wito wa kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Nami nilimuona akihifadhi Quran kila wakati akiwa na mtazamo huo. Kwa hivyo najua kwamba hata kama mwili wake labda uko kifungoni na katika mahali pa giza, moyo wake ungali unang'aa kwa Nuru ya Mwenyezi Mungu.

Wale waliomfunga hakika ni lazima wanamwogopa kwa sababu kwa kuzoea kuwavunja wafungwa sugu, hunaona akisi ya uovu wao wenyewe pindi wanapokabiliwa na ujasiri na ushupavu wa haki wa haiba za watu kama hawa ambao nyoyo zao zinaangazwa kwa nuru ya Mwenyezi Mungu (swt).

Pia namkumbuka waziwazi akiongea kuhusu mafunzo tunayoweza kuchukua kutoka kwa kifungo cha Yusuf (as), kwamba nyoyo zetu zinapaswa kuwa thabiti na kamwe msikate tamaa na faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

)يَا بَنِيَّ اذْهَبُواْ فَتَحَسَّسُواْ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلاَ تَيْأَسُواْ مِن رَّوْحِ اللّهِ إِنَّهُ لاَ يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللّهِ إِلاَّ الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ)

Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf: 87]

Hata kama nimekuwa nikiijua Ayah hii, yeye ndiye aliye ikitisha moyoni mwangu.

Siwezi kuongeza zaidi yay ale ambayo Ayah hii inayazungumzia kwa familia yake na kwa wabebaji ulinganizi wote wanaomtamani rohoni.

Allahumma Ameen

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Haider

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu