Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Usalama wa Wanawake ni Sarabi Ndani ya Mji Mkuu wa India ya Kiliberali

(Imetafsiriwa)

Hasira za watu zinaongezeka siku hadi siku kutokana na mauaji ya Sabiya Saifi aliyejitolea kwa ajili ya Ulinzi wa Raia. Madai ya haki kwa Sabiya yanaongezeka sio tu jijini Delhi, bali hadi UP [Uttar Pradesh], Uttarakhand, Bihar, Maharashtra na majimbo mengine ambapo maandamano ya mishumaa yanafanyika. [Gazeti la Siasat daily, 7 Septemba 2021]

Tukio hili la kuumiza moyo la mauaji ya kikatili ya msichana mdogo wa Kiislamu kwa kuchomwa visu karibia mara 50; titi lake kukatwa pamoja na vidonda kadhaa mwili mzima ikiwa ni pamoja na sehemu za siri na kutupwa kwenye vichaka jijini Delhi ilisababisha wimbi la mshituko kote nchini, vyombo vingi vya habari vilishindwa kutangaza taarifa yoyote kuhusu mauaji haya ya kikatili. Isipokuwa baada ya kuvuma kwa hashtagi katika akaunti za mitandao ya kijamii kwa muda wa wiki isemayo #JusticeForRabia (haki kwa Rabia), vyombo vya habari vichache vilichapisha habari kuhusiana na suala hili. Ni wazi kabisa inaonyesha majadiliano ya kudhibiti tukio hili yanayofanywa na mashirika ya habari ya kitaifa yanayofanya kazi ndani ya nchi kubwa ya kidemokrasia duniani. Wazazi na kaka wa marehemu walisema walikabiliwa na changamoto kadhaa na ugumu kabla ya kuweza kufungua faili la malalamiko. Kumekuwa na maandamano machache yanayodai uchunguzi ufanywe na CHOMBO KIKUU CHA UPELELEZI, huku polisi wa Delhi wakijaribu kuifunga kesi kwa maneno ya uwongo.  Hii inaonyesha kiwango cha ufisadi ndani ya idara ya usalama na thamani iliyotolewa kwa usalama wa wanawake ndani ya nchi yao wenyewe. Hata hivyo, vyombo vya habari vya ndani vilivyozoeleka vilikuwa na wasiwasi sana kuhusu siku zijazo juu ya haki za wanawake na usalama wao nchini Afghanistan baada ya Taliban kuichukua Kabul. Ni wazi matukio haya yanaonyesha unafiki wa vyombo vya habari juu ya uhalisi wa kweli wa usalama wa wanawake na ‘uwezeshaji’ ndani ya nchi kubwa ya kidemokrasia duniani ambayo inaunga mkono uhuru wa Kimagharibi.

Hii sio mara ya kwanza uhalifu wa aina hii dhidi ya wanawake kuripotiwa nchini India; matukio kadhaa kama kesi ya ubakaji ya Nirbhaya (2012), kesi ya ubakaji ya Unnao (2017), kesi ya ubakaji ya Kathaua (2018) na kesi ya ubakaji na mauaji ya Hyderabad (2019) yanafichua uhalisia mbaya wa uhalifu wa kinyama wa kijinsia dhidi ya wanawake nchini. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Thomas Reuters mwaka 2018 uliiweka India kama nchi hatari zaidi kwa wanawake. Kwa mujibu wa Afisi ya Kumbukumbu za Uhalifu wa Kitaifa (NCRB), India ilirekodi kesi za ubakaji 88 kila siku ndani ya mwaka 2019. Ripoti ya NCRB inaonyesha kuwa mazingira makubwa ya ubakaji wa msichana au mwanamke yameongezeka kufikia asilimia 44 kwa miaka 10 iliyopita. Kuhusu Delhi, sio tu ni mji mkuu wa kisiasa lakini pia ni mji mkuu wa ubakaji ambao unarekodi ya idadi kubwa zaidi za ubakaji kuliko miji mingine nchini India; Katikati ya Januari 1 na 15 Juni 2021, polisi wa mji huo walisajili kesi 833 za ubakaji na 1,022 za unyanyasaji, juu zaidi kutoka kesi 580 za ubakaji na 735 za unyanyasaji zilizofunguliwa ndani ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Tokea kuvunjwa kwa Khilafah, ulimwengu umekosa utawala wa marejeo, jamii ya marejeo, mfumo wa marejeo kwa wanadamu; Kila mfumo uliotengenezwa na mwanadamu umekuwa ukiwakandamiza wanadamu na wanawake ndani ya jamii zao; watu weusi wanaonewa kidhati ndani ya mataifa ya Magharibi; uwonevu kwa Waislamu wa Uyghur ni sera maalumu iliyowekwa na China; vivyo hivyo, kuna mfumo maalum wa kugawa jamii ya India, ambapo kama mwathirika ni Muislamu au ni wa jamii ya Dalit [tabaka duni la kibaniani], basi vyombo vya habari havitachukulia uzito na muda mwengine wanashindwa kutangaza habari hio kwa ulimwengu, na taasisi za serikali fisidifu zinashindwa kuwaadhibu wahusika kwa mwenendo kama huo. Hata hivyo, kama mwathirika ni wa ‘tabaka la juu’ la jamii hiyo, hapo ndipo vyombo vya habari, polisi na mahakama vinafanya kazi kwa haraka mpaka uamuzi unapitishwa na mhalifu anaadhibiwa.

Dunia haitoweza kufikiria kuhusu jamii yoyote ambayo ilikuwa ni ya mfano katika kusimamisha haki isipokuwa jamii ya Kiislamu. Mfumo wake wa utawala ulisimamisha haki kati ya matabaka ya watu tofauti tofauti kwa kutekeleza Sheria na kuadhibu wahusika wa uhalifu bila ya kujali dini, rangi au kabila. Msingi wake wa kiroho wa kujisalimisha kwa Muumba uliifanya jamii hii iwe ya tofauti na ya kushangaza kuliko ustaarabu wowote katika historia ya binadamu.

Amri ya Mungu ya kusimama imara kwenye upande wa haki imewekwa wazi katika aya ya Qur’an ambapo Mwenyezi Mungu (SWT) asema;

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلَّا تَعْدِلُوا اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ)

"Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda" [Surat Al-Maida: 8]

Hili pia limesisitizwa katika Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama ilivyoripotiwa katika Bukhari. Mtume (saw) amesema:

«إِنَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَانَ إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ، وَإِذَا سَرَقَ الضَّعِيفُ قَطَعُوهُ، لَوْ كَانَتْ فَاطِمَةُ لَقَطَعْتُ يَدَهَا‏»

“Hakika Bani Israel walikuwa anapoiba mtukufu miongoni mwao humsamehe, na pindi anapoiba dhaifu humkata mkono. Lau ingekuwa ni Fatima (yaani binti ya Mtume) ameiba ningemkata mkono.” [Sahih al-Bukhari]

Ama kuhusu usalama wa wanawake, ulimwengu wa kiliberali wa Kimagharibi hauwezi kutatua mgogoro huu mkubwa. Tunaona uhalifu wa kutisha dhidi ya wanawake unaokithiri ndani ya nchi huria za Kimagharibi na takwimu zinazofanana zina akisi ndani ya nchi hizo zinazofuata nyayo za mfumo wa Kimagharibi. Katika zama za enzi za kati, karibia kila tamaduni isipokuwa Uislamu ziliwakandamiza wanawake kwa namna tofauti na watu wa wakati huo walitambua ukandamizaji huo; hata hivyo, usekula huria na kauli mbiu zao za kuvutia, kama uhuru wa kibinafsi, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake uliathiri usalama wa kweli na heshima kwa wanawake ndani ya jamii hizi. Lakini bado watu wanadanganyika na kauli mbiu hizi na wanashindwa kutambua athari mbaya iliyoletwa na kanuni hizi moja kwa moja. Uislamu pekee ndio unaoweza kuhakikisha usalama wa mwanamke ambao utadumisha heshima yake na kuwaadhibu wahusika wa uhalifu bila ya kulegeza msimamo maadili ya Kiislamu yaliyowekwa na Muumba wa Ulimwengu.

(وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ * بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ)

"Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, Kwa kosa gani aliuliwa?" [At-Takwir, Aya ya 8-9]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut tahrir na

Faizul ibn Ahmed

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu