Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Suala la Dkt Aafia Siddiqui ambalo lingali Halijatatuliwa

(Imetafsiriwa)

Kesi ya Kushtua ya Dkt Aafia Siddiqui Muislamu anayejiheshimu na Mwanasayansi wa neva (Neuroscientist) ambaye amekuwa nembo ya ‘Vita vya Ugaidi’ vya Amerika ni mmoja miongoni mwa mifano mingi ya kutisha ya ubaguzi wa Amerika katika miaka ya hivi karibuni.

Mwaka 2003, Aafia alitekwa nyara na huduma ya usalama ya Pakistan, ISI, chini ya serikali ya Musharraf, na kukabidhiwa kwa mamlaka za Amerika ili awekwe ndani ya gereza la ovu la Bagram.

Watoto wake wadogo watatu walipotea kwa miaka mingi, inadaiwa walifungwa pia, lakini habari kumhusu mtoto wake aliyemzaa kipindi hicho (kabla ya kutekwa) mpaka leo hazijulikani.

Aafia kuhusishwa kwa tukio la Septemba 11 ilitosha kuidhinisha ukatili na dhuluma aliyoteseka kwayo tangu kipindi hicho, na ilikuwa ni Yvonne Ridley mwandishi mchunguzi wa habari wa Uingereza aliyefichua ukweli kuhusu mahali alipo Aafia, akimwita “mwanamke aliyedhulumiwa zaidi duniani”. Aligundua kuwa Aafia, mfungwa namba 650, alijulikana kama mwanamke mwenye rangi ya kijivu wa Bagram kutokana na vilio vyake kutokana na mateso ya muda mrefu ya miaka mitano na kubakwa mara kwa mara yalishamiri kwenye korido za jela ya kijeshi alikoshikiliwa ndani yake kwa miaka mingi.

Kana kwamba hii haikutosha baada ya miaka mingi ndani ya Bagram, Aafia alikabiliwa na kesi nchini Amerika kwa mashtaka tatanishi–mwanamke huyu mdogo mwenye kilogramu 44 inadaiwa alichukua silaha dhidi ya walinzi wa gereza kwa nia ya kutoroka! – Hakuna ushahidi uliohusishwa wa kuwa mtendaji wa ngazi za juu wa Al Qaida kama madai yalivyooneka. Kesi yenyewe imeleta lawama kimataifa, wimbi la hisia na ukosoaji wa vita vya Amerika dhidi ya ugaidi.

Lakini bila la kushangaza dada yetu Aafia alihukumiwa miaka 86 ya kufungwa ndani ya gereza la kiwango cha juu, FMC Carswell lililopo Fort Worth, Texas. Kuifanya iwe wazi kabisa kwa watoa maoni wote kwamba licha ya ushahidi wenye mashaka, na hukumu isiyo ya sawa ambayo haikuendana na kosa lililodaiwa – pamoja na mateso ya dhahiri na unyanyasaji ambao tayari alishateseka, Amerika ilikuwa na nia ya kufanya mfano kwa Aafia ili kuwanyamazisha raia wao wa Kiislamu. Hivyo kulinda ajenda yao dhidi ya sauti yoyote ya ukweli kuhusu vita vyao vibaya vya kimabavu ambavyo majeshi ya Amerika yalivisababisha juu ya watu wote wa Iraq na Afghanistan.

Mipango potofu ya Raisi Bush na serikali yake korofi iliendelezwa na serikali zilizofuata. Hivi ‘vita vya muda mrefu’ vyenye nia ya kugandamiza mwamko wa Uislamu na Waislamu ulimwenguni vilihakikisha kuwa kesi ya Aafia iliendelea kwa kiasi kikubwa bila ya kutajwa ndani ya Amerika. Ngome ya misaada ya Uingereza na Jfac wamehakikisha kuwa Aafia amekuwa akipata mawakili ambao wanapokea ufadhili kwa kesi yake wakati huu wote, kudumisha mawasiliano na familia yake, na siku zote kuwa mstari wa mbele katika kunyanyua mwamko ulimwenguni na wasiwasi juu ya Aafia.

Hata hivyo licha ya juhudi za dhati hata kwa watu wanaofahamika na watoa misaada na mashirika mashuhuri, Aafia anaendelea kutaabika ndani ya gereza la Texas. Amewekwa ndani ya kifungo cha faragha kwa miaka kwa wakati mmoja, akipigwa na kuteswa mpaka kukaribia wendawazimu; pia alishambuliwa kikatili mwezi uliopita na mahabusu mwenzake ambaye alivunja kikombe cha kahawa ya moto kwenye uso wake, “karibia kumpofusha” kama yeye mwenyewe alivyosema, na “kushindwa kutembea” kwa hivyo “ilibidi kutolewa kwa kiti cha magurudumu”.

Dkt Aafia Siddiqui ni mwenye kuheshimiwa zaidi katika wanawake wa Kiislamu. Mama aliyejitolea na mbebaji daawa mtukufu alifaulu katika kazi yake na alikuwa ni mhamasishaji kwa wote waliomjua. Alikuwa mfano bora katika majukumu na wajibu mwingi wa Muislamu mchamungu; lakini licha ya heshima kubwa na thamani ya Uislamu iliyowekwa kwa kila mwanamke, mwanamke huyu wa kipekee ametelekezwa kabisa na viongozi Waislamu ambao hawajawahi hata kujadili masharti ya kuachiliwa kwake achilia mbali kudai kuachiliwa kwake.

Watawala wa Waislamu na haswa serikali ya Pakistan wana nguvu ya kidiplomasia ya kutishia kuondoa msaada wa kisiasa na kijeshi wanaoupatia Amerika kupitia kanda yote ya AfPak.

Ni baada ya yote, ni haki ya kila nchi kudai kuachiliwa kwa wafungwa wake kupitia hatua kama hiyo kama sio kwa diplomasia. Kuhakikisha kuachiliwa kwa wafungwa ni sheria ya ulimwengu, ni kawaida na haki ambayo imekuwepo katika hadhara zote. Kitu kimoja kinachodumisha uhalali wa kweli wa uongozi wowote ni hatua unazochukua ili kulinda watu wake wenyewe.

Sasa kwa nini serikali za Waislamu zimekuwa dhaifu mbele ya uso wa Magharibi? Lini uoga na hofu yao kwa Magharibi itabadilishwa na kuwa na uoga na hofu kwa Mwenyezi Mungu (swt)?

Abu Bakr As-Siddiq (ra) ameripotia,

«إنّ النَّاسَ إِذا رَأوا الظّالِمَ فلَمْ يأْخذُوا على يَدَيْهِ أوْشَكَ أنْ يَعُمَّهُمُ الله بِعِقابٍ منهُ»

“Pindi watu watakapomuona dhalimu (akidhulumu) kisha wasimzuie mikono yake kudhulumu Mwenyezi Mungu atakaribia kuwachanganya wote katika adhabu yake.” [Abu Dawuud na Tirmidhi]

Kwa kuzingatia hili, wafungwa wa Kiislamu na wanaume wote na wanawake wanaokabiliwa na ukandamizaji na uonevu, kwa uvumilivu wanasubiri kurejea kwa mamlaka ya kweli ya Kiislamu. Khilafah kwa njia ya Utume itaupa kipaumbele Ummah wa Kiislamu kulingana na maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu (swt) Qur’an – na kuwa uongozi ulio na ari na ujasiri wa kutosha kukabiliana na uovu na ulafi wa mwanadamu ambayo inamsukuma kurudia rudia udhalimu mkubwa.

Shariah anaamrisha kuwa majeshi ya Kiislamu yana jukumu la kuonyesha nguvu zake kwa madhalimu, kwa ajili ya kuwaweka huru wafungwa wetu na kutekeleza kile kinachohitajika ili kufanya neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu kabisa, kama Yeye (swt) anavyosema ndani ya Qur’an

(وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا)

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako!’” Surah An-Nisaa :75].

Kwa hivyo huu lazima uwe wito wa Ummah huu mtukufu wa kiulimwengu, wenye kujikariri ndani ya makasri na ngazi za utawala. Wito kwa, na kusadikishwa kwa Khilafah – muundo asili na takatifu utawala wa Kiislamu ambao unatimiza jukumu letu la pamoja la kumtii Mwenyezi Mungu (swt) kuhusiana na suala la Uislamu, na kuisimamisha tena Dini hii imara ndani ya ardhi za Waislamu, na kurudisha heshima ya roho nyingi sana zisizo na hatia, heshima iliyonyakuliwa na madhalimu wa kibeberu na mfumo wao kinyama wa Kibepari ya maslahi ya kibinafsi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Maleeha Fahimuddin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu