Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dola ya Tashwishi ya Kirasilimali Ikivalia Vazi la Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Wakati Ummah ukielekea katika ufahamu wake jumla wa kutoshindikana kurejea kwa Khilafah, tunaona baadhi ya watu wakimtafuta mkombozi kutoka kwa pote la viongozi walio mamlakani, ambaye anafaa zaidi kwa jukumu hili, na wanapendelea Raisi wa Uturuki Erdogan kuwa ndiye mwenye kufaa kwa jukumu hili. Hivyo, wanakubalisha matendo yake yote na kujaribu kuyakuza. Wanafikiri kuwa anatenda kisiri kwa ajili ya kuurejesha Uislamu madarakani, na kurejesha utekelezaji wa Sheria za Mwenyezi Mungu (swt)!

Bali kwa ushujaa wa mbwa mwitu na ujanja wa mbweha, Erdogan anajitahidi kuwalaghai baadhi kwa njia zisizo za moja kwa moja kuwa utekelezaji wa Uislamu unaweza kufanyika hatua kwa hatua, ili kuepuka hasira za dunia zinazopinga kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu, na kuepuka uvamizi wa ghafla. Tunaona waungaji mkono wa muelekeo wa Erdogan wakihalalisha utekelezaji wake wa sheria safi za kisekula kuwa ni aina ya udanganyifu kwa Wamagharibi, na kuwa matendo yote anayotenda yanaonyeshwa na serikali yake kuwa anafanya kazi kisiri kuurejesha Uislamu madarakani.

Haya ndiyo yale aliyoyataja mwandishi wa Jordan, Daoud Omar Daoud katika makala kwenye “Al-Quds Al-Arabi” yenye kichwa: “Vita vya Majaliwa na Kurejeshwa kwa Maisha ya Kiislamu,” ambapo alijaribu kuhusisha fikra za Erbakan na ushawishi wake kwa fikra za Hizb ut Tahrir, kama alivyodai. Fikra za Sheikh Taqiuddin An-Nabahani, muasisi wa Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu amrehemu, zimetokana na Quran na Sunnah, na kila anayesoma anaathirika nazo kwa sababu ni mtazamo wenye chimbuko la ki-Wahyi unaowakilisha kitulizo kwa majeraha ya Ummah huu na dunia. Hakuna shaka juu ya hilo. Hata hivyo, kubeba fikra ni vigumu kwa sababu madhalimu wote wa dunia wanataka kuzuia utawala wake, na kuibua vita kusitisha utawala wake ukiwa ni muundo wa utekelezaji. Hii ni kwa sababu fikra hizi za Hizb ut Tahrir ni za kipekee katika utekelezaji wa Uislamu zikiwa ni fikra na twariqa (njia), itawaondoa kutoka mizizi yao mara baada ya kuiweka kwenye medani ya kimataifa, inayojumuishwa ndani ya Dola hii kubwa ya Kiislamu ambayo inatumia hukumu za Shariah.

Japokuwa mwandishi ameeleza wazi kuwa Erbakan alitaka kuanzisha muungano wa Kiislamu, shirika la Umoja wa Mataifa kwa Waislamu, uanzishwaji wa muungano wa kijeshi wa Kiislamu kama wa NATO, utoaji wa dinar ya Kiislamu kuzuia Wamagharibi kutupora, kuanzisha soko la uchumi la pamoja, na kuondoa ushuru, hati za kusafiria na viza baina ya nchi za Kiislamu, yote hayo ni majaribio ya kuunganisha nchi za Waislamu katika umbo maalum katika muundo wa nchi za kirasilimali, kana kwamba hatuna mfumo wa kipekee wa Kiislamu ambao ni tofauti katika muundo wake na mfumo wowote wa kisiasa, ni mfumo wa Khilafah ambao Sheikh Taqiuddin, Mwenyezi Mungu amrehemu, ameuchambua kwa vizuri kwa dalili za kiSharia katika kitabu, Nidhamu ya Utawala. Erbakan alitaka kuunda dola ya Kiislamu iliochanganyika na usekula, ambapo atatumia baadhi ya hukumu za ki Sharia huku akihifadhi muundo wa dola ya kirasilimali. Hata hivyo, usimamishaji wa dola ya Kiislamu una njia ilio wazi katika fikra za Sheikh Taqiudin An-Nabahani, muanzilishi wa Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu amrehemu.

Lengo la Erbakan katika majaribio yake ni kuiburuza nchi ikubali usekula unaozunguka ndani ya mzingo wa Ulaya. Uwepo wa Waislamu hawa walioundwa kushiriki katika mfumo huo na kukubali usekula usiopendelea upande wowote na kukubali mchakato wa kidemokrasia, lakini wakati hatari ya ushawishi wa Amerika ilipomjia au kupitia kati yake au kupitia kumtega, kwa sababu Amerika imeunga mkono hatua zake ndefu katika Cyprus, jeshi la Uturuki, katika kujidhalilisha kwa Ulaya, ilikuwa ni hofu kwa tabia ya Erbakan kwa Amerika na mara moja aliivunja serikali yake, ambayo haikudumu kwa zaidi ya miezi 13, na kulazimika kujiuzulu. Hatua hii ilizingatiwa ni moja ya hatua za kushindwa kwa Amerika kuiweka Uturuki kwenye mikono yake, na sio, kama baadhi wanavyodai kuwa aliivunja kutokana na hamu yake ya kutekeleza Uislamu.

Kuja kwa Erdogan madarakani, kuliiwezesha Amerika kuinyakua Uturuki kutoka kwenye makucha ya Uingereza kupitia mapambano makali ya kisiasa, ya mwishoni kabisa ni mapinduzi ya karibuni yaliowezesha kuondoa uwepo wote wa Ulaya katika Uturuki. Lakini kuna vitu katika medani za kimataifa ambavyo vimebadilisha baina ya kipindi cha Erbakan na cha Erdogan. Mwanzoni, Amerika ilitaka kuwavuta maSunni upande wake na kuwaondosha kutoka ndani ya guo la Uingereza, na kwa hivi sasa haya yamepatikana, baada ya kumiliki nchi nyingi za Waislamu, hasa Saudi Arabia, kumaliza Uwahabi, na kubadilisha utiifu wa watawala wa Saudi Arabia kunyenyekea sera ya Amerika, na haya hayakufichikana kwa yeyote hivi leo. 

Kama tutachukua kile alichokisema muandishi (japo kinaweza kuwa na sehemu ya uhalali) bila kuleta madhara yoyote, basi kuna uwezekano aina tatu ambao hauna wa nne:

1-Kuwa kile kinachosemwa kuhusu raisi wa Uturuki kufanya kazi ya kurejesha Khilafah na kurejesha tena maisha ya Kiislamu ni kweli. Hili liko mbali na ukweli. Alikuwa waziri mkuu tokea mwaka 2003, na baada ya kuigeuza serikali kuwa ya mfumo wa kiuraisi, aliendelea kutawala kama raisi wa jamhuri tokea 2014. Tunaona kuwa mafanikio yote aliyoyafanya katika Jamhuri ya Uturuki yamefanikishwa kwa usekula na alitamka kwa majigambo na kinywa kipana kwenye mahojiano yake. Na hili ndilo alilolisema katika Kituo cha Al-Arabiya kwenye mahojiano naye miaka minne iliyopita wakati mtangazaji alipomuuliza kuwa wengi wanapata shida kuchanganya Uislamu na usekula, alijibu:

“Ninapata shida ya kuelezea ufahamu wa ulimwengu wa Kiislamu katika kuunganisha Uislamu na usekula, tokea tuanzishe chama chetu na kuufafanua usekula, na tumeelezea mahusiano ya Uislamu na muunganisho wake na ugaidi, hivyo tumetafautisha baina ya kuwa Waislamu kama watu binafsi na mfumo wa kisekula. Mimi ni Muislamu ninayetawala Uturuki kwa mfumo wa kisekula, ambapo humaanisha kuvumiliana kwa serikali. Na serikali inasimama kwa kiwango sawa kwa dini zote na madhehebu. Je hii ni kinyume na Uislamu?” Mwisho wa nukuu.

Amelielezea hili kwa uwazi kuwa anatawala kwa mfumo safi wa kisekula na hana nia ya kutekeleza mfumo mwengine japo kuwa yeye ni Muislamu!

Kwa upande mwengine, imepita miaka zaidi ya saba tokea aliposhika nafasi ya Uraisi wa Jamhuri, na kila mwaka tunamuona akiwa mbali zaidi na Uislamu kuliko mwaka wa kabla yake! Katika upande wa kisiasa, tunaona ndege za kivita zikipaa kutokea ardhi yake zikiua Waislamu nchini Syria, Libya na Iraq, na yeye ndiye aliyejenga ukuta mpakani na kuitenganisha na Syria na kumuuwa kila anayejaribu kuuvuka kutoka kwenye majirani zake Waislamu, akitekeleza maagizo ya Amerika kupambana na Uislamu na Waislamu bila kificho, bali ameyaeleza hayo wazi. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu wanaunga mkono kile anachokifanya pamoja na kuthibitisha.

Ama kwa upande wa uchumi, tunafahamu namna alivyopiga pigo la mwisho kupata mafanikio ya kisiasa kabla ya uchaguzi kuwapiga wapinzani wake, hata kama haya yamefanywa kwa kuwapa shida watu na kuwashindisha na njaa. Baada ya kufanya maboresho yenye muelekeo wa riba ya wazi, akiwaitia watu kuweka akiba fedha zao na kuchukua mikopo ya benki yenye riba, kwa mrejesho wa kuwahakikishia mapato kwa msingi wa riba, tukashuhudia bei za kila kitu zikipanda zaidi na zaidi. Malipo ya umeme, gesi na mafuta yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 50, na kupanda kwa vitu hivi kumepelekea kuongezeka kwa bei katika namna ya kutisha, yaani, amewapatia zawadi kwa mkono wa kulia na kupokea kutoka kwao mara mbili kwa mkono wa kushoto! Je hii ndio namna ya ushughulikiaji wa mambo ya watu?! Au ni mafanikio maalum katika matayarisho kwa ajili ya uchaguzi ujao wa 2023 kubakia madarakani huku Amerika ikimuunga mkono na kusimama nyuma yake.

Baada ya uchambuzi huu, tunaona kuwa uwezekano huu uko mbali na ukweli, bali Erdogan anacheza na hisia za hamu ya Ummah ya kurejea kwa Uislamu.

2- Yeye ni Muislamu anayetawala kwa usekula na hana nia ya kuwa Khalifah wa Waislamu, na hafanyi kazi ya kutekeleza sheria za Uislamu. Hapa vile vile, tunaona kama hii ndio hali, matendo yake anayojisifia nayo kwa Uislamu yanaweza kubadilika, kama kauli yake: “Nitaendelea na juhudi zangu kwenye riba hadi nimewatoa watu wangu kutoka kwenye janga hili kubwa,” na kauli yake: “Riba ni sababu, na athari yake ni upandaji wa gharama za maisha.” (Kauli za Erdogan 19/12/2021)

Hapa swali linazuka: Kwa nini tunashuhudia upotoshaji wa Wamagharibi wa taswira ya kila raisi anayedhaniwa kuwa Muislamu sana, na kumfukuza kutoka madarakani mara moja, bila kujali upande aliomtiifu kwake, na hili ndilo lililotokea kwa wengi hata kama walikuwa watiifu kwa mfumo wa kimataifa na kutekeleza maagizo ya Amerika na wengineo, na bado walienguliwa, lakini hatujashuhuia hilo kutokea kwa Raisi Recep Tayyip Erdogan?! Kwa nini?

Unamuona akipanda majukwaa ambayo kwa uwazi yanaunga mkono Uislamu, na anafanya baadhi ya harakati zinazoonyesha Uislamu, hata kama ni kwa uchache, lakini bado hatuoni Amerika ikifanyakazi ya kumuondoa, bali anapata msaada mmoja baada ya mwengine.

Japokuwa kama angechukua au kutekeleza hukumu kwa kile alichoteremsha Mwenyezi Mungu, Ummah wote ungelimfuata mara moja, kwa sababu ya hamu ya unyenyekevu ilionao kwa ajili ya kurejea kwa hukumu za Uislamu na siku za utukufu na heshima. Ummah unasimama upande wa yule anayetaka kutekeleza Shariah na kurejesha maisha ya Kiislamu. Utavitoa muhanga vyote vyenye thamani kwa ajili ya hili. Kama alifikiria na kuchukua hatua moja katika muelekeo huu, angeliona kwa macho yake mwenyewe mandhari kubwa ya Ummah huu mkarimu, lakini hatuoni hatua yoyote ya Amerika dhidi yake, bali tunaona msaada wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi na nafasi za kimataifa zinazoinyanyua hadhi ya Uturuki na kuisukuma kwenye nafasi ya nchi kubwa za kiuchumi.

3- Uwezekano wa mwisho, japokuwa natarajia liko nje ya mada, kwa sababu ya ujanja mkubwa unaofanywa dhidi ya Ummah huu. Wamagharibi wanajua kuwa Utawala wa Khilafah Rashidah, Mwenyezi Mungu ajaalie, ni wenye kuja, hivyo wanaleta mtu wa utawala aliye karibu na akili za watu ya kuwa anafaa kuwa Khalifah, lakini yeye yuko mbali na hilo; ambalo linaambatana na tabia za Erdogan, na hiyo ni kwa sababu ya kuficha, inaweza kuwa ni kilango cha salama wakati dola ya kweli ya Khilafah itaposimamishwa, hivyo yeye pia anatangaza kusimamishwa kwa Khilafah ya Kiislamu na kutekeleza Shariah, lakini kwa lengo la kuzuia Khilafah ya kweli na kuhamisha mazingatio, haya yanafahamika kwa watu na yalifanyiwa kazi kabla.

Khilafah ya kweli inaweza kuwa ni mpya katika matukio, na kwa kuwepo kwa nususi za wazi, ikiwemo Hadithi ya Mtume (saw): «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ، فَاقْتُلُوا الْآخَرَ مِنْهُمَا» "Watakapopewa bay’ah makhaifah wawili, basi muuweni wa mwisho wao."

Hata hivyo, kujiweka mbali kwa watu na Dini kwa miaka zaidi ya mia moja imewapelekea kuwa na udhaifu mkubwa wa kifikra na hawakuyatia mafundisho haya kwenye vitendo.

Shakhsiya ya Erdogan ni yenye kufaa kwa nafasi hii kwa sababu ya ujanja na udanganyifu wake, na wanamuamini sana, kwa kuwa anatekeleza kila kitu kwa usahihi kama anavyotakiwa, wana uhakika kwamba hatousimamisha Uislam hata akipata msukumo wa aina gani, kwa kuwa anafanya kazi ya kutekeleza usekula, anawaruhusu Waislamu kushusha pumzi  na kugeuza hisia zao juu ya suala la kuurejesha Uislamu kutawala. Uwepo wake unatengeneza kilango cha salama kwa namna mbili:

1-Kazi yake ya kuunganisha fikra ya usekula na Uislamu, anaoutangaza. Anazingatia Uturuki kuwa ni mfano wa kuigwa, ambayo imefanikiwa kuwa na usawa, haki, neema na maisha ya starehe.

2-Yupo tayari kucheza dori alizopangiwa kuuvunja Uislamu.

Enyi Waislamu: Ujanja wa Wamagharibi umezidi ubunifu wote, kwa hakika haupuuzi watu mashuhuri aina hiyo pindi wanapokuwa watiifu, kwa hiyo msidanganyike kwa wasifu wao, na kuweni katika wenye fikra angavu, na kuweni pamoja na wanaotaka kuitekeleza tena Shariah na kurejesha maisha ya Kiislamu. Wajibu huu una njia moja, kutoka kwenye fikra ya Kiislamu yenyewe, ambayo imechorwa na Mtume wetu Mtukufu na yeye (saw) ameonyesha njia safi ambayo tunahitajia kuifuata katika kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kuasisi dola ya kweli ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuahidi, na bishara njema tumeshapewa na Mtume wetu (saw) katika Hadithi tukufu: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume”. Basi fanyeni kazi pamoja na wafanyao na msiwe miongoni mwa wapotezaji wa fursa hii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Nabil Abdul Karim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu