Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Tik Tok ni Mtego ambao Yule tu Aliyeufanya Uislamu kuwa ndio Msingi wa Maisha Yake Anaweza Kuuepuka
(Imetafsiriwa)

Kuonekana kwa mapana kwa wanawake wa Kisudan kwenye Tik Tok kwa namna ya kuvutia macho, wakionyesha urembo wao, kucheza, kuyumbayumba na kuimba kwa njia inayoondoa sauti ya fitra (asili), hili linatokeaje kwa mwanamke wa Kiislamu na mlezi wake anaweza kuruhusu hilo?! Tumeona jinsi baba alivyo na wivu wa kinga hata katika nchi zisizoufahamu Uislamu. Mwanamume mmoja aliyekasirika alimpiga risasi mkewe mbele ya binti yao wakati wa mabishano kuhusu video zenye kuchochea ngono alizotuma kwenye mtandao wa video fupi wa “Tik Tok”, na inaaminika kuwa mume wake alijiua baada ya hapo wakati wa uchomaji nyama wa familia katika eneo la Nova Itamaraty, katika manispaa ya Brazil ya Punta Bora, inayopakana na Paraguay, Januari 24 iliyopita, kulingana na gazeti la Uingereza, Daily Star.

Kadhalika, mtu mmoja katika watu wa Sudan alimuua mkewe kwa sababu hiyo hiyo, kama alivyofanya mtu mwengine katika watu wa Palestina. Wivu wa kinga kwa wanaume wa Kiislamu ni wa asili. Hata hivyo, ili tusiangukie katika hali hiyo, hebu tujadili suala hilo kwa mtazamo wa kishariah.

Mwanamke wa Kiislamu amepata uangalifu mkubwa katika Dini ya Kiislamu ili kuhifadhi heshima yake na kuinua hadhi yake. Kujitolea kwa yale ambayo Shariah ilimlazimisha katika mavazi na mapambo yake ilikuwa tu kwa ajili ya kuzuia ufisadi unaotokana na kuonyesha mapambo yake. Tunapozichunguza sheria hizi kwa undani zaidi, hatutazipata zimefungika kwa wanawake, bali ni kinga kwao dhidi ya kutumbukia katika mzunguko wa upotovu na kusambaratika au kunyanyaswa na wengine, na kuzuia jamii kutumbukia katika uchafu.

Haya iliwekwa kwa mwanamke ili asikiuke matukufu ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuonyesha mapambo ya kupita kiasi au maneno machafu. Haikuwa haramu kwake kuchanganyika masokoni na wale ambao haruhusiwi kuchanganyika nao majumbani kama jamaa zake. Na pamoja na kumjali huko mwanamke, bado mambo yalifikia kiwango ambacho sasa anaingia kwenye nyumba za wanaume, wanawake na vijana wengine kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa bahati mbaya, hali ya wasichana kujionyesha kwenye mitandao ya kijamii imeenea sana bila udhibiti au sheria. Tunawaona wasichana wa Kiislamu wakiiga nchi za Magharibi kwa upofu, kwa hiyo tunaona wengine wakijipiga picha (selfie) wakifanya harakati za kushangaza na zenye kuchochea ngono kwa matamanio ya wanaume, wakipuuza vidhibiti vya Uislamu na hata kusahau mtazamo wa mujtamaa juu ya hilo. Au kurekodi video na aina ya uigizaji wa kukejeli ambao umeingizwa maneno machafu au miondoko ya densi, wakisahau kabisa kuwa video hii itatazamwa na mamilioni ya vijana, na kwa hivyo watapoteza heshima yao, na pia inasababisha aina ya ugomvi kati ya vijana na kubadilisha mtazamo wa wengine kuhusu sura halisi ya wasichana wa Kiislamu.

Kwa mfano, katika baadhi ya mitandao ya kijamii, hasa Tik Tok, Instagram na Snapchat, baadhi ya wasichana, hasa wa Kisudan, wamejizolea umaarufu kupitia sehemu za video ambazo wanaonekana kama wanamitindo, waigizaji wa kike au waimbaji kwa njia za kejeli katika muktadha wa burudani na shangwe, kulingana na imani yao. Wanaonekana uchi katika vyumba vyao vya faragha, wakiyumbayumba, na ikiwa mmoja wa wafuasi (aliye na wivu wa kinga) atatoa maoni juu ya adabu na tabia ya msichana wa Kiislamu na kukosoa mienendo na mtindo wake, na kusema kwamba anapaswa kuheshimu Dini yake na mila na tamaduni za jamii yake ya Kiislamu ya Kiarabu, hujibu akisema, "Huu ni uhuru wangu wa kibinafsi, na hakuna mtu anayeweza kuingilia kile ninachovaa au kufanya, na simruhusu mtu yeyote kuingilia faragha yangu!" Unawezaje kusema "faragha yako" ilhali wewe ndiye uliyechapisha video hiyo kwenye mitandao ya kijamii kuingia nyumba zote katika sehemu zote za dunia, kwa hivyo unazungumzia faragha gani?

Je, hivi ndivyo jinsi ya kuiga? Je, ni kwa njia hii hasi ndivyo tunavyotumia mitandao ya kijamii?

Kumbuka kwamba inajuzu kwa mwanamke kushiriki katika mitandao ya kijamii ya kielektroniki kama vile Facebook na Twitter, ikiwa atashikamana na hukmu za Shariah, akaandika yenye manufaa, na akajiepusha na sababu za fitna kwake na kupitia kwake, kama vile maneno yenye kuvutia, kicheko na mzaha na wanaume, na kuwa na mazungumzo ya faragha nao.

Mwanamke wa Kiislamu anachukuliwa kuwa jiwe la msingi la ujenzi wa jamii. Yeye ni mwalimu wa vizazi. Uislamu umeharamisha unyonyaji wake na umehifadhi usafi wake na utakatifu wake, na hata kumzunguka kwa ngome ya hukmu zinazomhakikishia maisha ya usafi na utakatifu. Tangu mwanzo Uislamu umewafanya wanawake kuwa ni heshima ambayo lazima ilindwe.

Enyi Walezi, kwa kuzingatia hali hizi, Uislamu haukumwacha mwanamke kuwa dhaifu huku mawimbi yakimpiga yakimpeleka popote yanapokwenda, kwa kuyatimia mahitaji na udhaifu wake. Uislamu ulimwekea mlinzi ambaye atamlinda na kumsaidia kufanya maamuzi ya busara mbali na matamanio na shauku, kumhifadhi, na kuihifadhi jamii kutokana na maovu na muozo, na ukawawekea wanawake majukumu yanayofinika sehemu za siri, ukaharamisha mchanganyiko isipokuwa kwa haja iliyokubaliwa na Shariah, ukaharamisha kakaa faragha, ukafaradhisha kuinamisha macho, ukaharamisha kuonyesha mapambo... na hukmu nyenginezo, basi je, mumesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuziacha hukmu hizi?

Serikali ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itamaliza njama hizi kwa kuondoa maovu yote haya.

Enyi wanawake wa Kiislamu: Tunawalingania kusimama pamoja nasi dhidi ya kafiri mkoloni na taasisi zake, vyama vyake na zana vibaraka ili kuzima shambulizi hili la kihalifu dhidi ya wanawake. Nyinyi ni wanawake wetu, mabinti zetu, na dada zetu, na tunasema kwamba lengo hasa la shambulizi hili ni kuwafikisha Waislamu katika hali ambayo zinaa na aina nyenginezo za maovu ni jambo la kawaida, chini ya ulinzi wa sheria kwa maovu haya. Mjadala wowote wa mambo ya wanawake wa Kiislamu nje ya Shariah takatifu unatia shaka. Hivyo, tumefikisha ujumbe, Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi wetu.

Kwa kutamatisha: Mwanamume na mwanamke wako sawa mbele ya majukumu ya Shariah, na kwamba wanawake wa Kiislamu leo wana wajibu wa kufanya kazi pamoja na wafanyikazi ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kama ilivyo wajibu kwa wanaume kutoka katika Umma wa Kiislamu. Dola ya Khilafah ina mfumo wa kijamii wa Kiislamu kama muundo ambamo heshima ya mwanamke inaweza kuhifadhiwa kivitendo.

Kwanza: Kupitia utabikishaji upya wa Uislamu, mwanamke sio bidhaa inayotolewa ili kuwaridhisha wanaume, bali anatakiwa kudumisha uhusiano safi kati ya jinsia zote unaohakikisha maingiliano yao kwa njia salama mbali na upotovu wa kingono. Hii humakinihsa ushirikiano mzuri na wenye manufaa kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote za maisha.

Pili: Kupitia kutengeneza mazingira matakatifu na safi ambamo matamanio ya kijinsia yanashibishwa kupitia njia inayoleta kheri kwa mujtamaa badala ya madhara. Haya yote husaidia kudumisha mazingira ya heshima kubwa kwa wanawake, na kupunguza unyanyasaji na uhalifu.

Kwa miongo mingi, wanawake katika nchi zote za Kiislamu wameteseka kutokana na ukandamizaji, umaskini na udhalilishaji chini ya tawala fisadi za kidhalimu na mfumo mbovu wa kiuchumi. Serikali za Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini zimefumbia macho ukiukwaji unaofanywa dhidi ya wanawake na kuwanyima haki zao za kimsingi.

Tawala zote, ziwe za kifalme au za kijamhuri, za kidemokrasia au za kidikteta, zimefeli katika kipindi cha miongo minane iliyopita kuhakikisha maisha ya staha na heshima kwa wanawake, jambo ambalo linaangazia haja ya dharura ya kuwa na ruwaza tofauti ya kisiasa yenye uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli katika eneo hilo yenye kudhamini mustakabali wenye heshima, uadilifu na ustawi kwa wanawake na wanaume wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Tunawalingania wanawake wote wanaoamini katika kuleta mabadiliko ya kweli yenye kuchangia kuboresha maisha ya wanawake, wajiunge nasi katika Hizb ut Tahrir, inayowasilisha mfano inayong’aa kupitia Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya utume, ambayo kwayo heshima, usalama na uadilifu hupatikana kwa kina mama na mabinti katika nchi za Kiislamu, ambayo itasimama kama kinara wa kuhifadhi na kupata haki za wanawake duniani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Reem Jaafar – Wilayah Sudan

#بالخلافة_نقتلع_نفوذ_الكافر

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu