Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Lugha ya Kiarabu ni Kiungo Muhimu na Msingi cha Uislamu
(Imetafsiriwa)

Qur'ani Tukufu ni Kitabu cha Mola wetu Mlezi aliyekiteremsha kwa lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu (swt) amewapa furaha wanadamu wote, kupitia kushikamana na mwongozo Wake na kufuata Njia Yake. Yeye (swt) ametahadharisha kila aina ya dhiki kwa yule inayemsibu na kujiepusha na njia hiyo. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنتُفَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى *‏ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى * بَصِيراً

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: ‘Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?’” [20:123-125].

Kanuni za lugha ya Kiarabu zimedhibitiwa na vitabu vya Nahw (Nahau) na Swarf (Mofolojia). Haya ni mambo mawili ya lazima, ambayo moja halitenganishwi na jengine. Lau si kanuni za lugha ya Kiarabu, Quran Tukufu isingeweza kueleweka. Lau si Quran Tukufu, lugha ya Kiarabu isingehifadhiwa. Kwa hivyo, lugha ya Kiarabu ni kiungo muhimu na msingi cha Uislamu. Ulinganizi wa Kiislamu hauwezi kuwasilishwa bila lugha ya Kiarabu. Uislamu hauwezi kueleweka kwa mujibu wa vyanzo, kwa kuvua hukmu, kutoka katika maandiko matakatifu ya Quran Tukufu na Sunnah safi za Mtume, bila lugha ya Kiarabu. Hivyo basi kuwahimiza Waislamu katika lugha ya Kiarabu kuna athari kubwa sana, ilhali kuitunza lugha hiyo ni muhimu sana.

Pindi mababu zetu, Maswahaba wa Mtume (saw) walipobeba ulinganizi wa Uislamu, wenye sifa yake ya kuwa ni ujumbe wa uongofu, nuru na baraka kwa walimwengu, waliubeba kwa nguzo tatu: Quran Tukufu, Sunnah safi ya Mtume na lugha ya Kiarabu.

Kwa hiyo, watangulizi wetu wema walihimiza kuwafundisha watoto wao na watu kuhusu Uislamu, kwa nguzo hizi tatu. Walikuwa wakijifunza Kiarabu, kama walivyokuwa wakijifunza Qur’an Tukufu na Hadithi Tukufu za Mtume.

Maadui wa Uislamu walitambua kwamba siri ya nguvu ya Waislamu iko kwenye imani yao ya itikadi ya Uislamu, na kujitolea kwao kutabikisha hukmu za Shariah zinazochipuza kutokamana na itikadi hiyo. Ni itikadi ya Upweke wa Mwenyezi Mungu (swt), katika kumtumikia Yeye Peke Yake, ambayo ilikuja kwa Waislamu, kupitia Quran Tukufu.

Maadui wa Uislamu walitambua hilo. Walikiri kwamba hawawezi kuidhoofisha Dola ya Kiislamu, maadamu Uislamu unabaki kuwa na nguvu miongoni mwa nafsi za Waislamu, kiasi kwamba ufahamu wake unabaki kuwa imara na utabikishaji wake uko imara. Hivyo maadui hawa wakakimbilia kutafuta njia za kudhoofisha ufahamu wa Waislamu kuhusu Uislamu, na kudhoofisha utabikishaji wao wa hukmu za Kiislamu.

Waliilenga lugha ya Kiarabu kwani ndiyo lugha ya Uislamu. Walijaribu kuitenganisha lugha ya Kiarabu na Uislamu. Hivyo, waliwasaidia wale ambao hawakuijua lugha ya Kiarabu, maadili yake na sifa zake, kuchukua mamlaka katika Ardhi za Kiislamu. Matokeo yake, umuhimu wa lugha ya Kiarabu ulipuuzwa, hivyo hatimaye Ijtihad ikakoma. Wale ambao hawajui hukmu na ujuzi wa lugha hii, hawawezi kuvua hukmu za Shariah. Kwa hiyo lugha ya Kiarabu ikatenganishwa na Uislamu. Dola ya Kiislamu ilichanganyikiwa juu ya kuzielewa hukmu za Shariah. Natija yake, ilichanganyikiwa juu ya utabikishaji wake. Hili lilikuwa na athari kubwa kwa dola, liliidhoofisha na kudhoofisha ufahamu wake wa matukio mapya. Kinachozua tatizo chenyewe, hakiwezi kulitatua, wala kulitatua kwa njia ifaayo. Hii ilisababisha kuongezeka kwa matatizo ndani ya dola hiyo, ambayo hatimaye ilisababisha dola kupoteza mashiko. Kutokana na haya, maadui wa Uislamu waliweza kudhoofisha uti wa mgongo wa Uislamu, ingawa ni kwa muda tu ... kwani Mwenyezi Mungu (swt) anakataa isipokuwa kuikamilisha Nuru yake, na Mwenyezi Mungu (swt) ni Muweza wa mambo yote, ingawa watu wengi hawajui hili.  

Pindi lugha ya Kiarabu ilipopuuzwa, Mujtahidina wakawa wachache sana miongoni mwa Ummah. Hatimaye vizazi vilishindwa kuelewa maana ya aya za Quran. Makafiri wa kikoloni wakafanikiwa, kwa bahati mbaya, katika kutuweka mbali na Dini yetu. Walifanikiwa kututawala. Hii ni hali ambayo haifichiki kwa mtu yeyote.

Hili lilitokea kwa kukosekana utawala wa Kiislamu, chini ya kivuli cha utawala dhalimu, katika zama za watawala Ruwaibida (wajinga). Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aturudishe kwenye Dini yetu. Tunamuomba atuongoze kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia, na atusaidie sisi Mashababu wa Hizb ut Tahrir kukamilisha mradi wetu mkubwa wa hadhara, mradi wa kusimamisha Khilafah Rashida ya Kiislamu ya Pili kwa Njia ya Utume. Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, tumetayarisha, tumeihifadhi na kuisafisha katiba ya dola, inayoshughulikia matatizo yote ya wanadamu, kwa mujibu wa kanuni tukufu za Shariah ya Uislamu, ikiwemo mfumo wote wa utawala, pamoja na masuala yote ya maisha ndani ya nyanja za kijamii, kiuchumi, masuala ya ndani na nje ya kigeni. Pia tumeandaa mtaala wa kipekee kwa vizazi vijavyo, kwa neema na rehema za Mwenyezi Mungu, mtaala wa kipekee wa kielimu na kithaqafa.

Dola hii inayoongoza itakuwa na hamu juu ya elimu na itawaheshimu Maulamaa. Itaregesha nafasi na hadhi kwa Maulamaa na walimu ndani ya jamii.

Hali hii changa, inayojua thamani, umuhimu na hadhi ya lugha ya Kiarabu, itaitilia maanani zaidi. Itakifanya Kiarabu kuwa lugha rasmi. Itawalazimu Waislamu wote kutoka wilayah mbalimbali kujifunza lugha hii kuanzia madarasa ya kwanza, kuanzia chekechea hadi shule ya msingi, kati na sekondari, kisha hadi vyuo vikuu. Italazimisha mtindo wa kuzungumza na mawasiliano, kadiri iwezekanavyo, katika Kiarabu cha kiasili (Fus’ha), kwenye vyombo vya habari, shuleni na vyuo vikuu, na kila mahali.

Ni dola ambayo alfajiri yake imedhihiri, na kuzuka kwake ni suala la wakati tu. Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, dola hii ya Uislamu itakuwa ndio dola inayoongoza duniani. Ewe Mwenyezi Mungu! Tufanye tuwe wanajeshi wake, wenye kuishuhudia na mashahidi wake. Hakika, utukufu ni wako Wewe pekee, na wewe ndiye muweza wa hayo. Utukufu wote ni Wako, Mwenye kusikia yote, Aliye Karibu zaidi na Mwenye kujibu dua.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً]

“na watasema: ‘Lini hayo?’ Sema: A'saa yakawa karibu!’” [17:51]

 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad An-Nadi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu