Jumapili, 02 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo Katili Nchini India Waongeza Chumvi Mauaji ili Kuidhinisha Mashini yake ya Uovu Inayoyumbayumba?

(Imetafsiriwa)

Huku India ikipitia baadhi ya maonyesho muhimu ya uchaguzi katika majimbo yake tofauti tofauti kama Himachal Pradesh, Gujarat na uchaguzi mkuu wa ndani lakini wenye hisa nyingi kwa Mashirika ya Manispaa ya Delhi, inakuwa chanzo cha masuala machafu, yenye uvundo na ugomvi ambayo ni sarafu za uchaguzi zenye uwezo wa kununua tena kura ili kusaidia kuunga mkono mfumo uliofeli. Mojawapo ya suala linalofaa zaidi na la kuchuma mapato kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi ni kesi ya mauaji huko Delhi ambapo mshtakiwa Aftab Ameen Poonawala 'alimnyonga', 'kikatili', 'kwa chuki' na 'kishetani' mwenza wake Shraddha Walker na kisha akakatakata mwili wake vipande 35, akavihifadhi kwenye jokofu jipya na kuendelea kutawanya vipande hivyo msituni kwa siku 18.

Ingawa aina kama hizi za kesi katika nchi kama India sio nadra na za kipekee lakini zinaonekana kwa sababu zinazojulikana, zilisisitizwa kwa njia ya hali ya juu kwamba tangu siku 10-11 kabla ya kuripotiwa kwa mara ya kwanza hadi siku ambayo nakala hii inaandikwa, karibu njia zote za habari, magazeti na vipindi vya runinga vya wakati wa watazamaji wengi na vichwa vya habari hujaa huku maelezo madogo na mazuri zaidi ya kesi hii yakisasishwa ndani ya kila saa 2-3. Matokeo mapya na mienendo ya hivi punde katika kisa hicho yanaendelea kuingizwa katika hali ambayo tayari ni ngumu kuarifu.

Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, mhalifu ni 'Aftab' na mwathiriwa ni 'Shraddha' ambayo hufanya mchanganyiko muafaka wa kupika kitoweo kitamu na cha kupendeza cha jamii ambacho kinapaswa kutolewa kwa umma ambao daima umekuwa ukitoa zawadi kwa BJP na mrengo wa kulia angalau katika uchaguzi. Neno la mrengo wa kulia la 'Jihad ya upendo' tayari linazunguka kwa umma na mitandao ya kijamii. Waziri Mkuu wa Assam Himanto Biswa Sarma alipokuwa akifanya kampeni huko Gujarat kwa ajili ya uchaguzi ujao tayari amefungua uwanja kwa kutamka kwamba "Ikiwa nchi haitamchagua kiongozi mwenye nguvu kama Narendra Modi mnamo 2024, mnyama kama Aftab ambaye aliukakata mwili wa mwenzi wake vipande vipande na pia alikuwa mtekelezaji wa jihad ya upendo, ataibuka katika kila mji wa nchi hii.”

Kinaya ni kwamba Himant Biswa Sarma ni Waziri Mkuu wa Jimbo (Assam) ambalo ni kati ya majimbo 5 ya juu ambapo kesi za unyanyasaji wa kinyumbani sio tu zimekithiri lakini pia zinahalalishwa na kufanywa kuwa jambo la kawaida.

Zaidi ya hayo, mtu anayemuua mtu mwengine anachukua athari kubwa zaidi hata kumwaga dhamana kwa jamii na dini yake lakini hujuma mbaya na iliyoratibiwa ya Daraja la Morbi lililokarabatiwa hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu 150 wengi wao wakiwa wanawake na watoto inapigiwa debe kama ajali tu ambayo hutokea kwa sababu ya ulegevu wa baadhi ya watu bila uwajibikaji wowote wa utawala na taasisi. Kwa upande mwingine, ripoti zinaonyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya watatu anakabiliwa na ukatili wa mpenzi wa karibu nchini India na kila saa moja kifo kinachohusiana na mahari kinaripotiwa kote nchini lakini hakuna mtu anayeangalia masuala haya halisi ambayo athari, makovu na kiwewe chake kimesambaa, kuenea na kudhoofisha jamii yenye afya. Uhalifu dhidi ya wanawake wa rika zote kutoka kwa watoto wachanga hadi wakubwa umekithiri wakati wote katika nchi kama India lakini ni machache tu ambao husisitizwa kimakusudi na kuongezwa chumvi kwa maslahi yao binafsi.

Lakini tukichunguza jinsi kesi hii inavyotendewa katika vyombo vya habari na nyanja za kisiasa, tunaona kwamba askari wa mrengo wa kulia na washauri wao katika taasisi za kisiasa wamekuwa wakishughulikia tukio hili la unyanyasaji wa kikatili wa wapenzi peke yake, kwa sababu linajumuisha mwanamume Muislamu na mwanamke wa Kibaniani. Hata mbunge wa Aam Admi Party alijaribu kulitumia sana kumtuhumu kiongozi wa BJP aitwaye Shehzad Poonawala kuwa na uhusiano na Aftab Poonawala. Kwa hivyo, wazo ni kulitia chumvi suala hili ili kupata TRP za haraka au kupata gawio la uchaguzi, haijalishi, jinsi gani kipindi hiki kinavyoacha alama zake zisizofutika na mbaya kwenye fikra za watu.

Madhumuni mengine ya wazi ya kuangazia tukio hili ni kuuchafua Uislamu na Waislamu kwa kuwachagua kibaguzi watu ambao kwa bahati mbaya wana majina ya Kiislamu lakini ukweli ni kwamba wao ndio zao la mfumo huu wa kikafiri, mtupu na potovu ya Urasilimali huria ambao humwachilia mwanadamu kuwa mnyama mwenye miguu miwili kumwachilia kufuata matamanio yake ya kimwili na ya kimsingi hadi kufikia kiwango cha juu kabisa kupitia kujiinua kwa wingi wa uhuru ambao unahakikishwa na kulindwa na Mfumo ya Kiliberali wa Kirasilimali. Aftab Poonawala anaweza kuzaliwa katika familia ya Kiislamu yenye jina la Kiislamu lakini yeye ni mfano halisi wa jinsi mfumo unavyoweza kubadilisha na kuwayeyusha watu binafsi ili wajitengeneze katika umbo lake la kimfumo. Aftab anasimama dhidi ya kila kitu ambacho Uislamu unatupa na anasimamia kila kitu ambacho mfumo huu mbovu unamtarajia kuwa. Mtu ambaye alipendezwa na onyesho la uhalifu la Marekani la Dexter, akitumia zaidi programu ya kuchumbiana ya Bumble kupata marafiki wa kike wengi kadri apendavyo na kuwa nao kama wenza wao wa kuishi kinyumba kwa ufadhili wa kisheria wa mfumo na serikali inazungumza mengi juu ya mtu ambaye anatumia kikamilifu bidhaa zote zinazopatikana za mfumo huu inaonuka. Aftab anaweza kuwa Muislamu kwa jina lakini kwa hakika yeye ni bidhaa ilitengezwa ya mfumo wa Kiliberali wa Kisekula wa Kirasilimali ambao huwezesha watu kufuata matakwa na matamanio yao ya kisilika kwa uwezo wao kamili bila kusahau ukweli kwamba inaweza kumgeuza mwanadamu mwenye fikra na busara kuwa jini. Huku si kushindwa kwa mtu binafsi tu bali ni kazi ya makusudi ya mfumo mbovu ya Kirasilimali.

Katika mujtamaa ambao Uislamu unatawala kama mfumo kupitia njia ya dola, masuala haya hayapo au yapo kidogo mno kwani Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ulioamrishwa na Muumba Mwenyewe kwa ajili ya viumbe wake (wanadamu) ambao unaelekeza na kushibisha ghariza zake na mahitaji ya kimwili kupitia masuluhisho mingi kwa njia iliyosawazishwa ikifafanua kwa uwazi majukumu mahususi, haki na wajibu wa watu binafsi na jamii ya kwa jumla. Mstari wa kwanza wa utetezi ni Taqwa (ucha Mungu) na hisia ya uwajibikaji ambayo mtu anapaswa kukutana na Muumba wake Siku Moja na inabidi alipwe kwa matendo yake mema au mabaya yanayosababisha raha ya milele au adhabu ya milele.

Ghariza hizo huhudumiwa vyema na kushibishwa ipasavyo kwa namna ambayo inahakikisha sakina na utulivu wa nafsiya ya mwanadamu. Lau Aftab angekuwa ni mwanajamii ya Kiislamu inayotawaliwa na mfumo wake, ni lazima angelelewa kumwamini Muumba wake Mwenyezi Mungu kiakili, mwenye kuzingatia matendo yake kwani yatahesabiwa katika Siku isiyo na shaka, kwa kushibisha ghariza yake ya uzazi kupitia kumruhusu kuoa wanawake wanne kwa wakati mmoja na kuepuka njia haramu au mbadala mbaya ili kushibisha ghariza hii. Aftab hapo hangekuwa huru kuwa mtumwa wa nafsi yake bali mtumwa wa Mwenyezi Mungu kuwa huru kutokana na matatizo ya kiakili yaliyoachwa huru na jamii za kiliberali zenye kuendekeza ngono kupita kiasi, zinazochochea uhalifu. Angewajibishwa na kukomeshwa wakati huo huo alipoingia kwenye uhusiano wa Haramu na mpenzi wake ukiangalia kitendo hicho kibaya mapema na badala yake angeozeshwa na kuwa na watoto ambao wanaotenda kwa mshikano wa uhusiano wa kihisia kati ya wazazi badala ya kuishi kama wenzi bila ya majukumu na fungamano lolote.

Kuchagua kibaguzi keso moja pekee na kuiongeza chumvi kwa maudhui yake ni upande mwingine wa kishetani wa mfumo huu mbovu ili kuhamasisha mashini zake zinazo karibia kufa. Huku sio kutengua na kufeli kwa mtu mmoja au wawili bali ni matunda machungu ya mfumo unaoyumba na siku moja utaangamia.

(وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا)

“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!’” [Al Quran 17:81]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mujahid Abu Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu