Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ummah Unakua Kiidadi, na Haja ya Khilafah Kusimamisha Dini ni Kadhia Nyeti

(Imetafsiriwa)

Nimegundua ongezeko la video fupi zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, za watu wakitamka Shahada na kuwa Waislamu. Hilo lilinivutia. Liliniweka kwenye safari ya utafiti ili kujua ni watu wangapi, haswa katika ulimwengu wa Magharibi, wanaokuwa Waislamu. Ni vigumu kukusanya takwimu halisi, lakini Ramadhan 2023 ilishuhudia kusilimu kwa watu mashuhuri. Watu hao mashuhuri ni pamoja na Charvarius Ward, mchezaji mpira wa miguu wa NFL wa timu ya San Francisco 49ers, mwigizaji mwenye tuzo wa Nigeria Mercy Aigbe, rapa maarufu wa Uganda na kijana Prodigy Felista di superstar na mpiganaji wa UFC wa Australia Jack Matthews, na Amber Leibrock, mpiganaji wa kike wa MMA wa Marekani, kwa kutaja tu wachache. Mwana YouTube Obayd Fox alisilimu mnamo 2022, lakini akazuru Makka mwaka huu na kusambaza video yake kwetu sote kuiona. Mbali na watu maarufu, kuna wengine, kama maafisa wa polisi nchini Uingereza, na watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Magharibi, ambao video za Shahada na safari kwenda katika Uislamu zinasambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Mtiririko wa ripoti za vyombo vya habari kutoka nchi tofauti tofauti kama vile Marekani, Australia, Ufaransa, Uingereza, zinazojadili kuongezeka kwa kusilimu katika Uislamu katika nchi zao zinaonyesha kuwa hata bila idadi halisi, inaonekana kana kwamba vyombo vya habari katika nchi hizi vimekaa na kutazama. Kulingana na Crestresearch.uk, "Katika nchi za Ulaya, wanaosilimu kwa ujumla ni kati ya asilimia moja na tano ya idadi ya Waislamu, lakini nchini Marekani, takwimu hiyo inaongezeka hadi asilimia 25."

Kumekuwa na utafiti uliofanywa na mashirika kama vile Mradi wa Matarajio ya Kidini wa Pew-Templeton mnamo 2021, ambao ulisema kwamba mwisho wa karne hii, Waislamu watakuwa kundi kubwa la kidini. Mnamo 2023, tumezidi bilioni 2. Hii inahusishwa na kiwango cha juu cha uzazi miongoni mwa Waislamu, lakini tunaweza kuona kwamba wanaosilimu ni nyongeza ya baraka kwa idadi yetu. Ummah unaokua ni katika bishara njema za Mtume Mtukufu (saw). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

أَنَا أَكْثَرُ الأَنْبِيَاءِ تَبَعًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ يَقْرَعُ بَابَ الْجَنَّةِ››» “Mimi nitakuwa na wafuasi wengi kushinda mitume wote Siku ya Kiyama, na mimi nitakuwa wa kwanza kubisha mlango wa Pepo.” [Muslim] Hadithi za kusilimu ni za kufurahisha nyoyo. Huku Uislamu ukikataza usilimisha wa nguvu, ubebaji Dawah kwa Uislamu ni kitendo kinacholipwa ujira mwingi sana. Waliosilimu wengi hutaja kiigizo cha Muislamu mmoja, au jamii maalum ya Waislamu, ambayo ushawishi wake uliwapelekea kuukubali Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) ayalipe matendo haya mazuri. Sahl ibn Sa'd ameripoti: Mtume (saw) alimwambia Ali (ra),

«انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحَتِهِمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإِسْلاَمِ، وَأَخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ، فَوَاللَّهِ لأَنْ يَهْدِيَ اللَّهُ بِكَ رَجُلاً خَيْرٌ لَكَ مِنْ أَنْ يَكُونَ لَكَ حُمْرُ النَّعَمِ»

“Waendee kwa Subira na upole hadi uingie katika ardhi yao. Kisha, walinganie Uislamu, na uwaarifu yale yanayowalazimu, kwani, naapa kwa Mwenyezi Mungul, lau Mwenyezi Mungu atakuongozea mtu mmoja kwako ni bora kwako kuliko kumiliki ngamia wekundu.” [Bukhari]

Ukuaji wa Ummah unatuhamasisha sisi sote. Tunaona jinsi kusimama kwa ajili ya Haqq (ukweli) kunaweza kusababisha watu kujibadilisha kikamilifu na maisha yao. Hata Waislamu ambao wamezaliwa ndani ya Dini, lazima wafike mahali wanapokubali Deen yao kwa uangalifu na kwa ukinaifu. Sisi sote, wale waliozaliwa ndani ya Uislamu, na waliosilimu, lazima tuukatae usekula. Haiwezekani sisi kufuata sheria zote za Uislamu, chini ya mfumo wa kisekula, ambao hautabikishi Uislamu!

Jamii za kisekula zinamaanisha kuwa watu wanakuwa Waislamu licha ya kuona tu sehemu ya Dini. Hii ni kwa sababu Dini ni Haqq na inajibu maswali muhimu tuliyo nayo juu ya maisha. Wanaona kufeli kwa mfumo wa kisekula. Lakini, hebu na tulinganishe kiwango cha sasa cha watu kusilimu, na kiwango cha kusilimu wakati wa Dola ya Khilafah. Wakati huo, jamii nzima zilikuja ndani ya Dini, kwani watu waliweza kuona uzuri wa Uislamu kwa ukamilifu, ulioasisiwa ndani ya jamii na dola. Fungamano la kiroho kwa Mwenyezi Mungu (swt) liliimarishwa kila wakati na mazingira ndani ya Khilafah. Mazingira hayo yalizalishwa kupitia utabikishaji wa sheria za Kiislamu kwa ukamilifu. Sheria zilizotabikishwa zinazohusiana na kila nyanja ya maisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Dola ya Kiislamu iliiunda jamii ambayo haipo ulimwenguni leo. Ile ambayo ilitatua matatizo ya wanadamu kulingana na maumbile yao na kuleta amani na uadilifu.

Lakini, tunaishi katika jamii za kisekula. Hii inamaanisha tunakabiliwa na shida zinazokua na kuongezeka kwa haraka. Kujadiliana na Waislamu kote ulimwenguni kunaonyesha kuwa kila mtu anakabiliwa na shida sawa za kibinafsi, kijamii na kiuchumi, na kila mtu anatafuta suluhisho. Waislamu wanaungana pamoja kusaidiana, kushiriki maarifa na utaalam, na tuna nguvu kwa idadi! Walakini, shida zetu zitaendelea, hata wakati tunapopeana fahamu zetu za Kiislamu kutusaidia kuwa na subira na kufanya kazi kwa bidii kutatua maswala. Hii ni kwa sababu kadhia nyeti imekosekana.

Dola ya Khilafah, ambayo ni fardh (wajibu) juu ya Ummah ya Kiislamu haijasimamishwa tena ulimwenguni. Hii inamaanisha kwamba Dini ya Uislamu haijasimamishwa. Ummah inakua Mashallah, na hii ni rasilimali nzuri kwetu. Tunaweza kufanya kazi pamoja, na kutimiza faradhi ambazo Mwenyezi Mungu (SWT) ametulazimisha, ambazo endapo zitapuuzwa zitatuacha tuwe na madhambi. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote anayekufa na hana shingoni mwake bay’ah, amekufa kifo cha Kijahiliya.” [Muslim]

Hatuwezi kupuuza kuwa bila ya Dola ya Khilafah, kwa kweli hatujaunganishwa kimwili, kama dola moja, na jeshi moja, hazina moja ya dola na Khalifa mmoja. Hakuna njia ya sisi kuishi maisha yetu katika kila nyanja kulingana na Dini yetu. Haja ya kusimamisha tena Dola hakika ni kadhia nyeti kwa sisi sote, kwa ajili ya mafanikio katika maisha haya na Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An Nur 24:55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Iqbal

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu