Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jinsi ya Kujadili Mzozo wa Palestina Unaoendelea pamoja na Watoto Wako (na kila mtu mwengine)

(Imetafsiriwa)

1. Wazazi wanapaswa kuanzisha majadiliano yote kwa kutumia taswira ifuatayo ili kuwafanya watoto wao waelewe mzozo huu: Unaishi kwa amani ndani ya nyumba yako na ghafla siku moja, miaka 75 iliyopita, watu wengine wanaingia kwa nguvu, wanachukua nusu ya nyumba yako, kuwafukuza Nusu ya familia yako, kuwaweka nusu waliobakia chini kizuizi cha kinyumbani katika nusu iliyobaki ya nyumba. Halafu, wanaendelea kuchukua vyumba kutoka nusu hiyo pia, kusukuma familia yako iliyobaki nyuma zaidi, na mwishowe, unajikuta umefungiwa katika bafu ya nyumba yako. Kana kwamba ubaya huo hautoshi, wavamizi wakati mwingine wanakata umeme wako, maji, na usambazaji gesi na hawaruhusu chochote kuingia bafuni kutoka kwa ulimwengu wa nje. Sasa wanafanya mazungumzo na wewe kwamba ubakie na bafu, labda pia jiko, na ukubali kwamba nyumba sasa ni ya wavamizi. Je! Ungekubali mpango kama huo? Kutia kidonda msumari wa moto, wakati wowote unaporusha jiwe kwa kulaani na kuvunja dirisha la nyumba yako mwenyewe ambayo kwa sasa mvamizi anaishi, unabandikwa jina la gaidi.

2. Kwa hivyo haihusu tu kujadili hali nchini Palestina lakini pia juu ya kusahihisha hadithi ya kile kinachoendelea. Uangaziaji wa kimataifa umetawaliwa na upendeleo wa wazi wa vyombo vya habari vya Wazayuni. Wakati huo huo, hisia za Waislamu ulimwenguni kote zinaunganishwa na dhiki ya watu wa Palestina, na hamu ya kuona ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa, Al-Aqsa na Palestina nzima kutoka kwa ukaliaji haramu wa Wazayuni.

3. Matukio haya hayakuanzishwa siku mbili zilizopita au na watu wa Palestina. Badala yake haya yalianzishwa mnamo 1917 na Uingereza, ikifuatiwa na kuundwa kwa umbile haramu la Kizayuni mnamo 1947 kwa kulazimishwa juu ya watu wa Palestina. Huu ulikuwa ni wizi mkubwa katika karne ya 20 ambao ulihalalishwa na sheria ya kimataifa na Umoja wa Mataifa na bado ingali inaendelea. Wapalestina milioni 5 walilazimishwa kutoka nje, huku nyumba zao, ardhi, na biashara zikichukuliwa na zingali zinachukuliwa zaidi na walowezi wa Kizayuni kupitia kufurushwa kwa nguvu kwa msaada wa serikali ya Kizayuni na jeshi lake.

4. Kila na sehemu yoyote ya Palestina iliyochukuliwa ni ukaliaji haramu, hata ikiwa sheria za kimataifa zinasema sio. Uislamu unaona hivyo na hiyo ndio hukmu iliyoamuliwa na Mwenyezi Mungu (swt). Kila na sehemu yoyote ya Palestina inahitaji kukombolewa, hata kama Sheria ya Kimataifa inasema vyenginevyo, kwani Uislamu unataka hili na hiyo ni sababu ya kutosha kwa Waislamu.

5. Kwa sababu Palestina ni eneo linalokaliwa kimabavu, wavamizi, wakati mwingine huitwa walowezi, sio raia na kwa hivyo hawastahiki kupata haki za raia kwenye mzozo wa kisilaha. Palestina sio bustani ambalo unaweza kufanya sherehe wakati wowote, badala yake ni eneo linalokaliwa kimabavu, kwa hivyo ili kubakia salama, usionekane mahali usipostahiki, wakati usiostahiki.

6. Tangu uundwaji haramu wa umbile la Kizayuni na ukaliaji kimabavu wa ardhi ya Palestina, watu wa Palestina katika maeneo fulani kama Gaza – wanaishi katika gereza kubwa zaidi la wazi ulimwenguni, ambapo wananyimwa mahitaji ya kimsingi – iwe maji safi, ufikiaji wa vituo vya matibabu na usambazaji wa umeme kudumu. Uingiliwaji na uvamizi wa mara kwa mara wa angani na jeshi la Wazayuni ni kawaida kwa watu wa Palestina. Miundombinu ya kimsingi ikiwemo nyumba za watu inavunjwa na haiwezi kurekebishwa. Athari za kiakili ni kubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho cha Wapalestina.

7. Watu wa Palestina pia ni pamoja na Wakristo ambao pia wanateseka mikononi mwa umbile la Wazayuni na pia hutafuta ukombozi wa ardhi ya Palestina. Lakini hii ni kadhia ya Kiislamu na jukumu kwa Waislamu kuikomboa Palestina na kulinda haki za watu wote wa Palestina.

8. Siku chache zilizopita zimeonyesha kuwa nyuma ya nguvu zote za kijeshi na msaada wa kifedha na kisiasa wa Magharibi, umbile haramu la Kizayuni linaweza kuondolewa na Palestina kukombolewa. Tunapaswa pia kujua kuwa ukombozi wake hautakuja kupitia serikali yoyote ya Kiarabu katika kanda hiyo, kwa kuwa tawala/serikali hizi ni za wasaliti na ndio mstari wa mbele kulihami umbile la Kizayuni.

9. Ukombozi hautakuja kupitia suluhisho la dola mbili na wazo hili ni lazima likataliwe. Suluhisho la dola mbili linajaribu kudanganya ulimwengu kwamba hili liko kwa maslahi ya Wapalestina. Walakini, ukweli na kusudi lake ni kulinda uwepo wa umbile haramu la Kizayuni huku wakidumisha haki zilizozuiliwa kwa Wapalestina na kuwazuia kurudi katika ardhi zao. Hili sio suluhisho bali ni kusalimu amri na kuwaambia Wapalestina hawawezi kukipata kile kilicho chao. Uislamu haukubali suluhisho la dola mbili au kwa kweli suluhisho jengine lolote isipokuwa ukombozi kamili wa Palestina nzima. Kwa kuongezea, kama ambavyo hatuitambui 'Israel', pia haturuhusiwi kuitambua Palestina, dola nyingine ya kitaifa inayotokana na amani ya Westphalia, Azimio la Balfour, na Makubaliano ya Sykes-Picot. Tunakubali tu suluhisho la Dola Moja pekee, ambayo ni Dola ya Khilafah.

10. Waislamu wamelishwa chakula cha udanganyifu kwamba sisi ni madhaifu na hatuna uwezo. Mchezo wowote wa kisiasa uliochezwa, siku chache zilizopita ni ukumbusho kwamba Waislamu sio madhaifu. Tunao uwezo na muhimu zaidi tunaye Mwenyezi Mungu (swt) na hakuna msaada mkubwa kuliko wakati Mwenyezi Mungu anapotoa msaada wake. Tunahitaji kutolegeza msimamo, na kutoshawishiwa na uvumi wa nguvu za Magharibi. Palestina au ardhi yoyote ya Waislamu iliyokaliwa kimabavu mithili ya Kashmir, ni mstari mwekundu, kama ulivyo ukandamizaji wa Waislamu mahali popote ulimwenguni.

11. Uhalisia huu wa unafiki unapaswa kuwa wazi. Wakati Ukraine inasaidiwa na kusifiwa kwa upinzani wake wa kinguvu dhidi ya uvamizi wa ardhi yake na Urusi, Wapalestina wamekataliwa haki hii kwa miaka 75. Waislamu hawapaswi kuwa wajinga au kudanganywa kuamini kwamba kutoa wito kwa Marekani, UN, Sheria ya Kimataifa, au Magharibi kuingilia kati kutasuluhisha kadhia hiyo. Hawa ni mbwa mwitu na wezi walioiiba Palestina na kulilinda umbile haramu la Kizayuni. Hawa ni mbwa mwitu wale wale wanaofungia macho janga la Kashmir mikononi mwa India inayotawaliwa na Mabaniani. Hawana aibu na wako dhahiri katika unafiki wao.

12. Msimamo wetu unapaswa kuwa wazi. Hatuna unafiki. Tunafahamu kuwa huu ni mgongano wa hadhara, itikadi na mifumo. Madai yetu ya kweli ni kwamba sisi ni wafuasi wa al-Haq, kwamba tunausalimisha utashi wetu kwa Mwenyezi Mungu na hatusemi katika jambo lolote katika yale ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) wameshaamua. Na Mwenyezi Mungu ametaka Palestina na ardhi yote ya Waislamu ikombolewe na kuregeshwa chini ya zizi na mamlaka ya Uislamu.

13. Badala ya kuwaambia Wapalestina kuwa jasiri katika kupambana na dhulma hii na sio kufanya kitu chochote kitakachofanya wavamizi wakasirike, tunawapongeza katika mapambano yao. Tunawaomba waendelee kuwa thabiti na tunawaomba msamaha kwa kupuuza kwetu na khiyana, kutokuwa na uwezo, na kutochukua hatua kwa watawala wetu kuelekea masaibu yao. Tunayatazamia majeshi ya Waislamu, ambayo tunayaita na kuyakumbusha jukumu lao, ambalo ni kuzikomboa ardhi zote za Waislamu.

14. Inapaswa pia kusisitizwa kuwa ingawa Wapalestina wanakufa, wao sio wanaolalamika. Badala yake, wako tayari kufa kwa sababu hii. Wanaamini kuwa kupitia hai wao na damu yao, wanaweza kutikisa dhamiri ya Ummah wa Kiislamu na majeshi yake. Wanaamini kafara yao inastahili na ina uwezo wa kuzuia usaliti wa watawala wa Kiislamu katika jaribio lao la kuhalalisha mahusiano na dola ya Wazayuni. Na huku wanakufa, nyumba zao zinavunjwa, watoto wao wanauawa, na wanalipia gharama kamili ya vita hivi, hawalalamiki. Lakini, wengi kati yetu, ambao jukumu lao la pekee ni kupaza sauti zetu kwa majeshi yetu kusonga badala yake tunalalamika! Je! Hii inatuambia nini kuhusu jukumu letu? Kwamba Wapalestina wanapaswa kutoa uhai wao ili kupata umakinifu wetu? Je, maisha yao mabaya na mateso hayatoshi kwa watawala wetu na majeshi yetu. Badala ya kuona aibu, tunalalamika juu ya kwa nini walivuruga mambo. Je! Hili ni suala la mkakati wa kijeshi au Iman? Hii ndiyo shida ya Wahn, wakati unapopenda Dunia hii sana kiasi kwamba unaanza kuogopa kifo. Kwa hivyo muogope Mwenyezi Mungu, na uzingatia jukumu lako. Toa wito kwa majeshi ya Waislamu kunusuru Palestina na al-Aqsa.

15. Tunapaswa kujikumbusha nafsi zetu na kuwaambia watoto wetu kuwa ilikuwa chini ya ukombozi wa Uislamu pekee kwamba Palestina na watu wake wote wakiwemo Wakristo na Mayahudi waliishi kwa usalama, amani, na utulivu. Hili ndilo suluhisho la kudumu kwa Palestina na kwa hakika ulimwengu mzima.

16. Na ndio, kama hatua moja ya mwisho, waambie watoto wako kwamba makombora ya 'Kutengezwa nyumbani' ambayo Hamas aliyarusha kwa dola ya Kizayuni kimsingi yalitengenezwa kutokana na silaha za Wazayuni ambazo hazikuwa zimelipuka ambazo awali walifyatuliwa kwazo na Makombora yanapeperushwa na mchanganyiko thabiti wa sukari na potassium nitrate, mbolea ya maarufu. Ndio, Wapalestina wanapigana na moja ya majeshi yaliyo endelea zaidi kiteknolojia kwa mikono yao mitupu, huku wakiishi katika hali mbaya zaidi, chini ya vikwazo  na vizuizi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdul Baseer Qazi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu