Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nini Jihad? Sehemu ya 1

Ufahamu wa jambo msingi katika Uislamu la Jihadi umetatanishwa kwa makusudi. Mataifa ya kikoloni na viongozi wao vibaraka wamekuwa mstari wa mbele katika njama hizi. Wale waitwao wanafikra na wanachuoni pia wametumiwa kupitia vyombo vya habari kueneza fikra za uongo juu ya Jihadi na hukmu zake, kiasi kwamba Ummah umechanganyikiwa kuhusiana na hukmu hizi. Kwa hivyo, imekuwa ni hitajio kubwa la wakati kuelezea hukmu hii muhimu ya Kiislamu kwa muongozo wa Qur’an na Sunnah.

Japokuwa neno Jihadi asili humaanisha “utumiaji wa juhudi”, lakini katika shari’ah ya Uislamu, istilahi hii maana yake ni “kupigana au kuua, yaani vurugu inayofanywa ili kunyanyua na kuthibitisha neno la Mwenyezi Mungu”. Hii ni kama mfano wa neno Shahidi linalomaanisha “mshuhudiaji” ikiwa litachukuliwa kwa maana ya kawaida ya kilugha, lakini neno hilo hilo hubeba maana tofauti kabisa ya “shahidi” kwa mujibu wa shari’ah za Uislamu. Ni sawa sawa katika neno “Hudood”, ambapo maana yake ya kilugha ni ukomo, lakini katika shari’ah ya Uislamu humaanisha aina za adhabu kwa uhalifu aina saba maalumu. Vivyo hivyo, Jihadi pia ni istilahi ya kisharia ya Kiislamu ambayo hutakiwa kuchukuliwa kwa maana yake ya kishari’ah na sio kwa maana ya kilugha. Maana ya kiistilahi ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama Mtume (saw) alivyotaja katika hadith ifuatayo. Iliulizwa kwa Mtume (saw): “Ni yupi anayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume (saw) akajibu, «من قاتل لتكون کلمة اللہ هي العلیا، فھو فی سبیل اللہ “Anayepigana ili Neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu.” (Bukhari na Muslim)

Maana ya Jihadi

Mwanachouni maarufu Ibn Abideen alisema, (الجهاد هو بذل الوسع فی القتال فی سبیل اللہ),“Jihadi ni kutumia juhudi kubwa kadri inavyowezekana katika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt)”. Imam Ibn Abi Zaid Al-Qairwani ameifasiri kuwa ni (وھو قِتال الكفار لِإعلاء کلِمةِ اللہِ)  “Mapambano dhidi ya Makafiri ili kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, kwa mujibu wa shari’ah ya Kiislamu, Jihadi ni kupambana na kutia juhudi katika mapigano ili kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu, ima Jihadi hii ni ya moja kwa moja (yaani mapigano ya wazi wazi) au kupitia mali (yaani kutoa gharama ili kuendesha vita) au kupitia matamshi (yaani kuwashajiisha watu kupigana kwa nafsi zao au kugharamia). Kwa hivyo itakuwa ni Jihadi pindi ikitekelezwa kupitia jitihada ya kimwili, mali na matamshi, lakini ikiwa juhudi hizi hazikufanywa moja kwa moja dhidi ya mapambano na makafiri, basi kwa mujibu wa shari’ah haitambuliki kuwa ni Jihadi, hata kama kutatumika juhudi kubwa kiasi gani katika utekelezaji huo. Vile vile katika kauli au maandishi yaani, yawe yamehusishwa moja kwa moja na Jihadi. Kutaja tu jambo la kiroho au kutamka neno la haki mbele ya watawala haiambiwi kuwa ni Jihadi katika sharia. Kwa hivyo, kuwatia moyo wanajeshi na Ummah kwa ajili ya Jihadi, kuwatumainisha, kutaja malipo ya kuhujumu jeshi la adui mbele yao nk. huzingatiwa kuwa ni Jihadi kwa matamshi. Mapambano ya kisiasa yanayofanyika kwa ajili ya dini na kuwawajibisha watawala bila shaka ni matendo yenye malipo makubwa na Ummah hunufaika sana kwayo; hata hivyo, hayaingii katika tafsiri ya Jihadi kwa mujibu wa shari’ah. Zaidi ya hayo, ubainifu huu ni muhimu hapa kwa sababu tunaona juhudi dhidi ya kansa, polio na uchafu yote hutambulishwa kuwa ni Jihadi, ambapo sio hivyo. Vile vile, kulichukulia neno Jihadi na matendo hayo sio tu kumekatazwa lakini pia ni hatari, kwa sababu kufanya hivyo kunahafifisha ufahamu sahihi na istilahi ya kishari’ah ya Jihadi katika jamii. Hivyo hivyo, Jihadi dhidi ya nafsi au kuthibiti juu ya haki katika mazito ya enzi za sasa pia sio Jihadi japokuwa haya pia ni matendo yenye malipo makubwa. Kwa mujibu wa hadith kutoka kwa Sayyida Aisha (ra), Mama wa waumini, ukweli huu umeelezwa wazi kabisa, wakati Yeye (ra) alipomuuliza Mtume (saw) kama kuna Jihadi kwa wanawake? Mtume (saw) akasema: «نعم علیھن جهاد لا قتال فیه، الحج والعمرةNdio! Jihadi ipo kwao lakini haihusishi mapigano, (ni) Hajj na Umra” (ibn Majah). Hadith kama hiyo pia imeripotiwa na Bukhari. Kwa hivyo, inathibitika kwamba “Jihadi” inakuwa na mapigano halisi. Imevuliwa pekee kwa wanawake, kama ilivyoelezwa na Mtume (saw) kuwa Jihadi yao haijumuishi mapigano; bali wanawake hupata malipo sawa na Jihadi kupitia Hajj na Umrah.

Wajibu wa Jihadi

Jihadi ni wajibu unaotokana na dalili za wazi katika Qur’an na Sunnah. Mwenyezi Mungu (swt) ametaja katika Qur’an:

[كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ ] “Mmeandikiwa kupigana vita.” (Al-Baqara: 216)

[وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ]

“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitna, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu” (Al-Baqara: 193)

[قَاتِلُواْ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلاَ بِالْيَوْمِ الآخِرِ وَلاَ يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَلاَ يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حَتَّى يُعْطُواْ الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]

“Piganeni na wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiyari yao, hali wametii” (Al-Taubah: 29)

[إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ] “Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu.” (Al-Taubah: 39)

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ قَاتِلُواْ الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلِيَجِدُواْ فِيكُمْ غِلْظَةً]

“Enyi mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu” (Al-Taubah:123)

Al-Nisai amepokea kutoka kwa Anas (ra) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«جَاهِدُوا الْمُشْرِكِينَ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ وَأَلْسِنَتِكُم»

“Piganeni na Washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na kwa ndimi zenu”

Mtume (saw) pia alisema,

«الجِہادُ ماضٍ الی یومِ القِیامة» “Jihadi ni yenye kuendelea hadi siku ya Kiyama”

Bukhari amepokea kutoka kwa Anas (ra) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,

«لَغَدْوَةٌ في سبِيلِ اللَّهِ، أوْ رَوْحَةٌ، خَيْرٌ مِن الدُّنْيَا وَمَا فِيها»

Kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (yaani Jihadi) kwa siku moja au usiku mmoja ni bora kuliko dunia na vyote vilivyomo ndani yake”. Bukhari na Muslim ameinukuu Hadith kwamba Mtume (saw) alisema,

 «أمرت أن أقاتل الناس حتی یشھدو أن لا إله إلا اللہ، فإذا فعلوا ذلك عصموا مني دماءھم وأموالھم إلا بحقھم»

“Nimeamrishwa kupigana na watu hadi watakaposhuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) na Muhammad (saw) ni Mjumbe wake, na kusimamisha salah na kutoa zaka. Pindi wakifanya hivyo, watasalimika nami maisha yao na mali zao, isipokuwa kwa haki ilio juu ya Shari’ah”

Katika hadith nyingine kutoka kwa Abu Hurairah, yeye (saw) alisema,

«مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَغْزُ وَلَمْ يُحَدِّثْ بِهِ نَفْسَهُ مَاتَ عَلَى شُعْبَةٍ مِنْ نِفَاقٍ»

“Yeyote anayekufa bila kushiriki Jihadi wala kuitamani, anakufa katika unafiki” (Sahih Muslim)

Abu Dawood amepokea kutoka kwa Imam Hussain (ra) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,

«لا تزال طائفة من أمتي يقاتلون على الحق، ظاهرين على من ناوأهم، حتى يقاتل آخرهم المسيح الدجال»

“Halitoacha kundi katika Ummah wangu wakipigana juu ya haki, na watawashinda wanaopigana nao, hadi wa mwisho wao atapigana na Masih Dajjal”.

Na katika hadith nyingine iliyopokewa na Imam Ahmad bin Hanbal, Mtume (saw) alisema, “Mimi ni Mtume na nina majina kumi”.

«أنا محمَّدٌ وأحمدُ والمُقفِّي والحاشرُ ونَبيُّ الرَّحمةِ ونَبيُّ المَلحمةِ»

“Mimi ni Muhammad, na Ahmad, na Al-Muqfaa na Al-Haashir, na ni Nabii wa Rahma na Nabii wa Jihadi”.

Hali tofauti za Jihadi:

Jihadi ya mashambulizi ni faradhi ya kijumuiya (Fard Kifaya) juu ya Ummah. Hii humaanisha kuwa Jihadi itaanzishwa na sisi dhidi ya adui, japokuwa adui hajaanzisha uvamizi wowote dhidi yetu ili kuifanya ardhi hiyo kuwa ni sehemu ya Dola ya Kiislamu, na ili Uislamu uweze kutekelezwa juu ya watu wa ardhi hiyo na ndipo hapo Uislamu utakapojitokeza kwao katika hali yake ya kivitendo. Dalili ya ufaradhi wa kijumuiya ni aya hii,

[لاَّ يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُوْلِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فَضَّلَ اللّهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً وَكُـلاًّ وَعَدَ اللّهُ الْحُسْنَى وَفَضَّلَ اللّهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا]

"Hawawi sawa Waumini wanao kaa tu wala hawanadharura, na wale wanao pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewatukuza cheo wale wanaopigana kwa mali yao na nafsi zao kuliko wale wanao kaa tu. Ingawa Mwenyezi Mungu amewaahidi wote mashukio mema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhili wanaopigana kwa ujira mkubwa kuliko wanao kaa tu." (An-Nisa: 95)

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu (swt) hakuwaonya wale wasiotekeleza Jihadi; bali, pia “amewaahidi mazuri”. Ikiwa aina kama hiyo ya Jihadi imekuwa ni wajibu wa mtu binafsi, watu wasiokwenda wameahidiwa adhabu. Vile vile, aya nyingine pia inathibitisha wajibu wa pamoja wa Jihadi.

      [وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً فَلَوْلاَ نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُواْ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ]

“Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakaporejea, ili wapate kujihadharisha? (Al-Taubah: 122)

Aya hii inaeleza kuwa Waislamu wote kwa pamoja hawahitajiki kwa ajili ya Jihadi ya mashambulizi. Kwa kuwa si jukumu la mtu mmoja mmoja, sio Waislamu wote wameamrishwa kwenda. Hata hivyo, ikiwa Waislamu hawatojishughulisha katika Jihadi ya mashambulizi dhidi ya taifa au nchi katika kipindi fulani, basi Waislamu wote huchukuliwa ni wenye kutenda dhambi, lakini ikiwa wajibu huu hutekelezwa kupitia ushiriki wa Waislamu wachache, basi huchukuliwa kuwa ni wajibu wa kijumuiya unaoweza kutekelezwa pia na Waislamu waliobaki.

Japokuwa hukmu za Jihadi ni za uwazi na hazikufungwa na kitu chochote chengine, lakini kwa kuwa Jihadi ya mashambulizi hufanyika ili kutanua mipaka ya ardhi ya Dola ya Kiislamu, kwa hivyo uwepo wa Ardhi ya Kiislamu ni sharti kwa Jihadi. Hii ndio sababu ya kuwa ni utawala wa Kiislamu tu unaoweza kutekeleza Jihadi ya mashambulizi kwa namna inayofaa.

Kwa jinsi Jihadi ya kujihami inavyozingatiwa, hiyo ni wajibu juu ya kila Muislamu wa eneo lolote linaloshambuliwa na adui. Kwa Waislamu waliobakia, huwa ni wajibu wa kijumuiya. Wajibu huu hubakia hadi adui atolewe na ardhi ya Waislamu isafishwe kutokana na Makafiri. Wajibu huu pia huanzia kwa Waislamu waliokaribu kisha huendelea hadi kuwakusanya Waislamu wote Ulimwenguni. Kwa hivyo, kuwatoa Amerika ndani ya Afghanistan na Iraq, kwanza ni wajibu kwa Waislamu wa Afghanistan na Waislamu wa Iraq kisha huwa wajibu kwa Waislamu walio karibu, mfano Waislamu wa Pakistan, Iran na Saudi Arabia, na hasa majeshi yao. Wanahitajika kushiriki kimwili katika Jihadi, na juhudi hizi huhitajika kuwepo hadi wawe na uwezo wa kuwatoa Amerika moja kwa moja kutoka katika ardhi. Jihadi ya kujihami haihitaji Waislamu kuomba ruhusa kutoka kwa kiongozi, mtawala, au hata Khalifah, kiasi kwamba, hata mtumwa hahitaji ruhusa kutoka kwa bwana wake, wala mke hahitaji ruhusa kutoka kwa mumewe (kama ana uwezo wa kupigana), wala mtoto kuhitajia ruhusa kutoka kwa wazee wake.

Katika tukio la kuvamiwa ardhi ya Waislamu, baadhi ya nukta zinahitaji kufafanuliwa:

1.Inapokuwa ardhi ya Waislamu inavamiwa na adui, wanajeshi wake ni wa mwanzo kuihami. Kama wataweza kusimamisha mashambulizi ya adui na kuihami nchi, bado itakuwa ni wajibu juu ya waliobakia kuwaunga mkono. Imam Al-Mawardi amesema, “kwa kuwa hii ni Jihadi ya kujihami, hivyo wajibu huu utabakia kwa kila mtu na kwa kila Muislamu muweza katika eneo”. Kwa mfano, katika vita vya mwaka 1965, raia walilisaidia jeshi kwa njia zote zilizowezekana kwenye medani ya mapambano ya Lahore.

2.Suala la kuwa huu ni wajibu juu ya Waislamu wote katika eneo humaanisha kuwa ni wajibu wa kila mtu muweza kama majeshi au makundi mengine, na juu ya watu binafsi au makabila yenye kumiliki uwezo wa kijeshi. Hii ni kwa sababu uwepo wa uwezo huwa ni, matokeo ya hitajio kwa utekelezaji wa hukmu ya sheria yoyote, kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

    [لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا] “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo” (Al-Baqarah: 286)

Hii hufanya kazi katika mambo yote. Kwa hivyo, sio sahihi kusema, kwa kubadilisha maana, Jihadi imewajibishwa tu kwa watu binafsi juu ya wanajeshi, vikundi vilivyojiandaa vya wapiganaji na makabila yenye nguvu, kwa sababu neno Muislam ni la jumla na liko wazi katika maana yake kuwa hii ni wajibu juu ya wale Waislamu walio na uwezo na wale wenye kubeba stadi za kutekeleza Jihadi kama inavyotakiwa na sheria. Hivi leo, majeshi yote ya nchi za Waislamu kivitendo hutumiwa kama ni mamluki kwa ajili ya maslahi ya wakoloni na watawala vibaraka. Hivyo, wajibu huu huwaangukia watu waaminifu katika Ummah ambao watatekeleza mapambano ya kisiasa kuyakomboa majeshi kutoka kwenye utumwa huu, ili waweze kutumiwa kwa ajili ya Jihadi kwa mara nyingine kwa kuondoa ushawishi wa kisiasa. Lengo hili linaweza kufikiwa tu kwa kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Ni ngao tu ya Khilafah inayoweza kupangilia Jihadi na kuweza kivitendo kukomboa ardhi zote za Waislamu zilizovamiwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,

 «إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّة یُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَیُتَّقٰی بِه»

“Khalifah ni ngao, Waislamu hupigana na hujikinga nyuma yake” (Muslim)

3.Jihadi ina lengo maalumu na vita hivi sio kwa lengo la mapigano, na wala sio kwa ajili ya kuua wasiokuwa Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Qur’an,

[وَأَعِدُّواْ لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدْوَّ اللّهِ وَعَدُوَّكُمْ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili kuwatisha maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.” (Al-Anfal: 60)

[يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُواْ مِئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّئَةٌ يَغْلِبُواْ أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لاَّ يَفْقَهُونَ * الآنَ خَفَّفَ اللّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّئَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُواْ مِئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُواْ أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللّهِ وَاللّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ]

“Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo ishirini kati yenu wanaosubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika waliokufuru. Kwa sababu wao ni watu wasiofahamu. Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo ikiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwepo alfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.” (Al-Anfal: 65-66)

Katika aya ya mwanzo, lengo la matayarisho ni kuwatia hofu maadui ambayo ni muhimu kwa kumshinda adui. Hivyo hivyo, katika aya ya pili na ya tatu, Mwenyezi Mungu (swt) anatujuilisha idadi inayohitajika kuweza kuwashinda maadui. Hivyo, Jihadi hutekelezwa kwa lengo, na sio tu kwa mapambano. Hivyo hivyo, imepokewa katika Sahih Muslim kutoka kwa Suleman bin Bariid kutoka kwa baba yake kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kila anapomchagua Amiri wa jeshi au kikosi, humnasihi kumcha Mwenyezi Mungu na kuwatendea Waislamu wenzake wema. Yeye Mtume (saw) alikuwa akisema,

«...ولا تغلوا، ولا تغدروا، ولا تمثلوا، ولا تقتلوا وليدًا، وإذا لقيت عدوك من المشركين فادعهم إلى ثلاث خصال، فأيتهن أجابوك إليها، فاقبل منهم، وكف عنهم: ادعهم إلى الإسلام، فإن أجابوك فاقبل منهم...فإن هم أبوا فاسألهم الجزية، فإن هم أجابوك فاقبل منهم»

“…wala msifanye ufisadi katika ngawira, wala msivunje ahadi, wala msiwakate maiti, wala msiue watoto, unapokabiliana na adui katika washirikina basi watake mambo matatu, kama watakujibu kwa lolote, basi wakubalie, na usiwadhuru. Walinganie Uislamu, pindi wakikubali basi wakubalie na ujitenge na mapigano…kama hawakukubali Uislamu basi watake watoe Jizya. Kama wakikubali basi wakubalie na ujitenge na vita…” (Sahih Muslim 4294). Hadithi hii ni dalili nyingine ya lengo la Jihadi. Kwa kuwa Jihadi ina malengo kadhaa, kama ilivyo lengo la Jihadi ya kushambulia ni kugeuza eneo kuwa ni Ardhi ya Kiislamu kwa kuondoa mfumo wa Kikafiri na kusimamisha mfumo wa Uislamu. Kwa hivyo, ikiwa kufikia lengo hilo hakuwezekani, basi vita hivi havianzishwi; bali matayarisho hufanywa kupata uwezo unaohitajika ili lengo lifikiwe. Hivyo hivyo lengo la Jihadi ya kujilinda ni kuikomboa ardhi ya Waislamu kutokana na uvamizi wa nje. Hata hivyo kama vita vya msituni havitoshelezi kufikia lengo hili, basi ni lazima kuja na njia za kuwezesha kufikia lengo hilo. Waislamu wameshuhudia kwa miongo kadhaa tokea wajitolee kwa ajili ya Dini hii, kwa ajili ya Waislamu wanaodhulumiwa na dhidi ya uvamizi wa kigeni; hata hivyo, jitihada zote hizi zilikuwa bure kutokana na khiyana ya watawala vibaraka wa Waislamu. Walikuwa wakiwasaliti, kama ilivyofanywa kwa kuwekwa vizuizi Kashmir au kama ilivyofanywa kwa Taliban au kama inavyopangwa wakati huu dhidi ya vizuizi Afghanistan. Hii ndio sababu ya kwa nini ni lazima kwa Waislamu kuwaondoa watawala hawa wasaliti na kusimamisha Dola ya Khilafah; vinginevyo (Mwenyezi Mungu aepushe mbali) lengo la Jihadi halitofikiwa juu ya kuwa Waislamu wanaendelea kujitoa muhanga!!!

4.Lau adui amesimamisha utawala wake katika maeneo ambapo huweza kivitendo kutawala Waislamu, basi Waislamu huwa kama wafungwa wa kivita katika hali kama hii japokuwa katika hali halisi sio wafungwa wa kivita na hivyo Jihadi haibakii kuwa ni wajibu wa kibinafsi juu yao, kwa sababu hawana uwezo wa kulikomboa eneo hilo. Hii ndio hali kama iliyoko Gaza na Kashmir, na ni kama iliyokuwako katika sehemu kubwa ya Bara katika India baada ya vita vya 1857 vya Uhuru. Katika mazingira kama haya, wajibu huu unahamia kwa Waislamu walio karibu kuanzisha Jihadi ili kuyakomboa maeneo haya ya Waislamu kutoka kwa uvamizi wa Makafiri. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an,

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anayetoka kwako.” (An-Nisa: 75)

Wakati wowote mtawala, Imam au Khalifah wa Waislamu akitangaza Jihadi, huwa ni uwajibu wa kibinafsi juu ya wote isipokuwa wale waliovuliwa naye. Hukumu hii ni kwa Jihadi zote mbili ya kushambulia na ya kujilinda, kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) alisema,

  [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]

“Enyi mlioamini mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” (Al-Taubah: 38)

[انْفِرُواْ خِفَافًا وَثِقَالاً وَجَاهِدُواْ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللّهِ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” (Al-Taubah: 41)

Kutoka kwa Masheikh wawili, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,

«وإذا استنفرتم فانفروا» “Na mnapotakiwa kutoka basi tokeni”

Mahala hapa ni muwafaka kutaja nukta hii muhimu kuwa sababu ya kishari’ah ya hukumu ya Jihadi ni kuwepo kwa Makafiri wanaokataa ulinganizi huu. Hivyo hivyo sababu ya kishari’ah ya kusitisha Jihadi ni malipo ya Jizya kutoka kwa Makafiri baada ya kutenzwa nguvu. Kwa hivyo, muda wa kupatikana Makafiri katika ulimwengu wanaokataa da’wah ya Uislamu wanaofikishiwa, Jihadi ya kushambulia itabakia kuwa ni wajibu wa kijumuiya juu ya Waislamu na Waislamu wataulizwa na Mwenyezi Mungu (swt) juu ya wajibu huu muda wote. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Qur’an,

   [وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ]

“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitna, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu” [Al-Baqara: 193]

[قَاتِلُواْ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلاَ بِالْيَوْمِ الآخِرِ وَلاَ يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَلاَ يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حَتَّى يُعْطُواْ الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]

“Piganeni na wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiyari yao, hali wametii” [Al-Taubah: 29]

[إِلَّا تَنفِرُواْ يُعَذِّبۡڪُمۡ عَذَابًا أَلِيمً۬ا] "Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu  chungu"

 [Al-Taubah: 39]

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ قَاتِلُواْ الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلِيَجِدُواْ فِيكُمْ غِلْظَةً]

“Enyi mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. (Al-Taubah:123)

Bukhari na Muslim wamepokea hadith ifuatayo,

«أمرت أن أقاتل الناس حتی یشھدو أن لا إله إلا اللہ، فإذا فعلوا ذلك عصموا مني دماءھم وأموالھم إلا بحقھم»

“Nimeamrishwa kupigana na watu hadi watakaposhuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) na Muhammad (saw) ni Mjumbe wake, na kusimamisha salah na kutoa zaka. Pindi wakifanya hivyo, watasalimika nami maisha yao na mali zao, isipokuwa kwa haki ilio juu ya Shari’ah”

Aya na Hadith hizi zinafafanua kuwa sababu ya kishari’ah ya Jihadi ni uwepo wa Makafiri wanaokataa Uislamu; hata hivyo, sababu ya kishari’ah ya kusimamisha Jihadi ni kulipa kwao Jizya na kukubali mamlaka ya Uislamu.

Jihadi sio tu kwa ajili ya Kujilinda

Hizi ni njama nyingine za masekula Wamagharibi na taratibu zao ili kuifunga Jihadi kuwa ya kujikinga tu. Hii ndio sababu kila nchi ya Waislamu ina wizara ya Ulinzi, lakini hakuna yenye wizara ya vita au Jihadi. Japokuwa Wamagharibi pia hutaja wizara zao kuwa ni ulinzi lakini kwa kweli, wizara zao ni za vita, sio ulinzi.

Qur’an, Hadith, Maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Ijma’i sahaba hutafsiri Jihadi ya kushambulia na kujilinda kwa maana ya uwazi. Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Qur’an,

[وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ]

“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitna, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu”

(Al-Baqara: 193)

 [قَاتِلُواْ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلاَ بِالْيَوْمِ الآخِرِ وَلاَ يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَلاَ يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حَتَّى يُعْطُواْ الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]

“Piganeni na wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiyari yao, hali wametii” [Al-Taubah: 29]

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ قَاتِلُواْ الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلِيَجِدُواْ فِيكُمْ غِلْظَةً]“Enyi mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. (Al-Taubah:123)

Hizi ni hukmu zilizo wazi na hakuna Ayah iliyofutwa au iliyozifunga, kumaanisha kwamba aya hizi hazionyeshi kuwa mapigano ya kuwashambulia Waislamu au wasiokuwa Waislamu wanaotekeleza mapigano dhidi ya Waislamu; bali, zinawalazimisha Waislamu kupigana “hadi kusiwepo fitna”. Zaidi ya hayo, zinawalazimisha Waislamu kuendeleza Jihad hadi Makafiri wajisalimishe kwa mamlaka ya Waislamu na hukmu za Kiislamu kwa kulipa Jizya. Bukhari na Muslim wamepokea hadithi ifuatayo,

«أمرت أن أقاتل الناس حتی یشھدو أن لا إله إلا اللہ، فإذا فعلوا ذلك عصموا مني دماءھم وأموالھم إلا بحقھم»

“Nimeamrishwa kupigana na watu hadi watakaposhuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) na Muhammad (saw) ni Mjumbe wake, na kusimamisha salah na kutoa zaka. Pindi wakifanya hivyo, watasalimika nami maisha yao na mali zao, isipokuwa kwa haki ilio juu ya Shari’ah”

Hadithi hii imepokewa na Ibn Umar, Abu Hurairah, Jabir bin Abdullah, Aus bin Abu Aus, Abu Abbas, Sahl bin Saad, Noman ibn Bashir, Tariq ibn Asheem, Abu Bakrah, Muaz ibn Jabl, Samrah bin Jundub. Hivyo hadith hii ni Mutawatir, ambayo iko katika kiwango cha juu kabisa cha Hadith. Katika Hadith hii pia, Yeye (saw) hakuifungamanisha Jihadi na uvamizi wa Makafiri. Matendo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Makhalifah Waongofu pia wameikiri Jihadi ya kushambulia. Vita vya Badr, Hunain, Muta na Tabuk vyote vilianzishwa na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), na mifano yake inaonekana wakati wa Makhalifah Waongofu ambayo imewafikiwa na Masahaba wote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Imran

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu