- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Janga la Virusi vya Korona: Wacha Urasilimali Umalizike na Khilafah Isimame
Ramadhani hii, 1441 Hijria, inaingia duniani katika hali ya kipekee. Mateso katika aina ya mojawapo ya viumbe vidogo kabisa vya Mwenyezi Mungu (swt), kirusi, kimefichua batili ya Urasilimali na itikadi ya kisekula ambayo kwayo umejengwa juu yake, utenganishaji wa dini na maisha.
Binaadamu licha ya maendeleo yao makubwa ya sayansi, teknolojia na matibabu wamekuwa wamenyongeshwa na kiumbe kidogo kabisa, ambapo inathibitisha ukubwa wa Mwenyezi Mungu (swt) na Utawala Wake juu ya vyote ambavyo Yeye (swt) ameviumba wakati kamwe havikuwepo.
Wanadamu wameingizwa katika hofu, kukata tamaa na hasara, lakini kwa wale wanao muamini Mwenyezi Mungu (swt) na kutekeleza matendo mema, katika maafa, huwa na subra kupitia matarajio ya Malipo Yake kwa kila hasara na huwa katika hali ya kuomba afueni kutokana na maafa.
Licha ya rasilimali nyingi, tisho la njaa limeeneza kivuli chake cheusi kilicho kirefu juu ya sehemu kubwa ya ardhi, kwani maradhi haya yamefichua urundikaji mchafu wa utajiri kwa matajiri wakubwa mno kupitia utabikishaji Urasilimali. Kukiwa na tofauti kubwa sana na zama ambazo hukumu zilikuwa kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ambapo angalizo juu ya usambazaji wa utajiri lilikuwa mkubwa mno, kiasi ya kuwa katika kulikuweko na nyakati ambapo masikini hawakupatikana.
Licha ya maendeleo katika matibabu na watoaji huduma hodari, mifumo ya huduma za afya imezidiwa na mkurupuko wa maradhi haya. Mkurupuko huu umefichua namna gani huduma za afya zilivyo lemazwa na kupuuzwa na warasilimali wasio na huruma kwa kung'ang'ania kutoa huduma za afya kwa misingi ya faida pekee, katika hali zote mbili za huduma za afya za kibinafsi na makampuni binafsi yanayo sambaza huduma za afya za dola. Zaidi ya hivyo, chini ya urasilimali, huduma za afya za dola zimeendelea kupuuzwa vibaya mno kupitia shinikizo la hali ngumu ya uchumi na kubana matumizi. Ni tofauti kabisa na zama za Uislamu, ambapo ilikuwa ni wajibu juu ya dola kutoa matibabu bila ya gharama yoyote, kiasi ya kuwa ardhi za Waislamu zilikuwa ni kituo cha utalii wa matibabu.
Ni kama ambavyo fimbo ya Musa (as) ilivyo fichua batili ya kiini macho cha wachawi wa Firauni, mkurupuko wa maradhi ya virusi vya Korona umefichua dosari ya mfumo ulioundwa na mwanadamu wa Urasilimali na Mafirauni wa leo ambao wanautabikisha. Hakika, hii hali na fursa ya kipekee kwa Ummah wa Kiislamu kuwasilisha mtazamo wake wenyewe wa usimamizi wa mambo ya watu kwa ulimwengu.
Ramadhani hii, 1441 Hijria, pamoja fadhila zake nyingi, Waislamu nawafanye bidii kwa ajili ya kuregesha ngao yetu, Khalifah juu ya njia ya Utume. Muislamu wa kawaida na anyanyue sauti yake katika kutaka atawaliwe kwa yote aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Afisa Muislamu wa majeshi na atoe Nusra yake kwa Khilafah, ili kazi ya kivitendo ya kutabikisha Uislamu ianze mara moja. Urasilimali na umalizike na Khilafah na isimame.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair - Pakistan
#Covid19 #Korona كورونا#