Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Maulamaa – Warithi wa Mitume

Maulamaa (Wenye elimu) ni warithi wa Mitume (as), cheo ambacho hakitolewi kwa sababu tu ya kuidhinishwa na chuo kikuu chochote au madrasah, wala sio kwa elimu yenyewe ambayo wameipata. Bali cheo hicho hutolewa kikiwa ni jukumu kubwa kutokana na uzito wa kazi yao ya kueneza ujumbe (تبليغ الرسالة) kwa kutokuwepo Mtume (saw) pamoja na watu kwa kile walichokibeba katika elimu safi kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume (saw). Ufikishaji huu unajumuisha kuuhuisha Ummah kwa mwangaza wa elimu wakati Ummah umeganda katika giza la ujinga. Kwa hivyo, kifo cha mwanachuoni yeyote mkubwa ni hasara kubwa kwa Ummah kama Mtume (saw) alivyosema,

«إن الله لا يقبض العلم انتزاعًا ينتزعه من الناس ولكن يقبض العلم بقبض العلماء حتى إذا لم يبقِ عالمًا، اتخذ الناس رءوسًا جهالا، فسئلوا فأفتوا بغير علم، فضلوا وأضلوا»

“Hakika Mwenyezi Mungu haiondoshi elimu kwa kuinyakua kutoka kwa watu, bali huiondosha elimu kwa kuwaondosha maulamaa hadi kusibakie mwanachuoni yeyote, watu huchukua wajinga kuwa viongozi wao, wanapoulizwa hutowa fatwa bila elimu, basi hupotea na huwapoteza wengine.” (Bukhari na Muslim)

Maarifa katika Uislamu sio kama ukasisi katika dini nyengine kuweka sheria kutokana na matamanio yao na kwa manufaa yao binafsi, wakidai kuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu, kama watu wa Kitabu (Ahlul Kitab) walivyokuwa wakifanya. Bali, ni jukumu kubwa la kulingania ujumbe kwa watu kwa kutokuwepo Mtume (saw) bila kuficha chochote. Jukumu la ulinganizi halitekelezwi kwa ulinganizi wa sehemu ya ujumbe tu kwa mtu kujifunga na mahubiri ya kibinafsi, kufundisha na uongozi. Pia halitekelezwi kwa mtu kujitosheleza binafsi katika kazi ya da’wah kwa kile anachokiweza kama kuwalingania watu mmoja mmoja kwenye Uislamu, kuhubiri maadili ya Uislamu au kuanzisha madrasa na mengineyo. Bali zaidi inahitajia kazi ya kisiasa ya umakini kama ilivyo linganiwa na Mtume wetu Mpendwa (saw), ambayo inaweza kuonekana wazi wakati Mwenyezi Mungu (swt) alipomuamrisha kutoka wazi kulingania wakati wa hatua ya mwanzo ya Utume kwa kusema, (إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلاً) “Kwani hakika mchana una shughuli nyingi” [TMQ 73:7). Neno 'سبحا طويلا’ maana yake kilugha ni kuogelea kipindi kirefu (katikati ya bahari) bila kuwa na mapumziko au kulala. Hii inaonyesha ukali wa ulinganiaji wa ujumbe na Mtume (saw) amelingania kwa zaidi ya miaka 23 kwa bidii ile ile kama alivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu (swt) hadi alipopata thibitisho kutoka kwa watu siku ya Arafah kwa kusema, «ألا هل بلغت... اللهم فاشهد»  “Je nimefikisha kwenu… Ewe Allah shuhudia”. Kwa hivyo, kurithiwa Mitume na Maulamaa hakupatikani kwa ulinganizi wa sehemu sehemu tu za Uislamu, wala kwa utoshelezwaji wa mtu pekee kwa kulingania kile anachokiweza. Bali kunahitajika kazi makini ya kisiasa ya kuulingania Ummah kwa kusimamisha Khilafah, kuwahesabu watawala, kufundisha Uislamu kwa watu kiujumla, bila kuficha chochote, kama Mtume wetu (saw) alivyofikisha.

Kushindwa kufikisha haya kwa kuficha au kugeuza huleta makemeo na laana kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt),

(إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ أُولَٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ)

“Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha – nazo ni hoja zilizo wazi   na uongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni – hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.” [TMQ 2:159]

Kwa hakika, aya hii ni ukumbusho wa wazi, bali ni kemeo kubwa kwa wanachuoni kutoficha au kugeuza Hukmu za Mwenyezi Mungu, hasa kile ambacho kipo na kilicho wazi katika mazingira yoyote, ima yawe kutokana na mbinyo wa watawala madhalimu au kwa kupata faida chache ya kidunia. Abu Hurayra (ra) amesimulia yote aliyoyasikia kutoka kwa Mtume (saw) kutokana na maonyo makali ya aya hii. Alisema (ra), "لولا آية في كتاب الله تعالى ما حدّثتكم حديثاً" “Lau kama sio aya katika kitabu cha Allah, nisinge kuelezeeni hadithi yoyote”. [1]

Aya hii iliteremshwa katika muktadha wa makemeo kwa wanachuoni miongoni mwa watu wa Kitabu wanaoficha kile kilichoteremshwa kwao juu ya kuja kwa Mtume (saw). Hata hivyo, ujumla wa aya umeenea kwa wote wanaoficha. Pia aya hii inatiliwa nguvu  na hadith ambapo Mtume (saw) amesema, «مَن كتَم علما ألجمه الله بلجام من النار» “Yeyote anayeficha elimu, Mwenyezi Mungu atamvisha lijamu katika lijamu za moto siku ya kiama” (Imepokewa na Abu Ya’la na Tabarani katika isnad sahih kutoka kwa Ibn Abbas (ra)) [2].

Maneno katika aya (من البينات والهدى) inahusu kile chenye kuonekana na kwa dalili ya wazi ambayo imefafanuliwa na Mwenyezi Mungu (swt) bila ya kuwa na tafauti za rai. ‘Al-Bayyinah’ inahusisha halali, haram, kulingania na Hukmu zilizofafanuliwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kama ilivyosemwa na Imam Qurtubi [3]. Bila shaka, hii inahusiana na kuficha yale yote ambayo ni ya wazi na yasio na shaka katika sharia kama ‘kuhukumu kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiteremsha’ kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt),

(وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ)

“Na tumekuteremshia wewe kwa haki, Kitabu hiki kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyokujia. (TMQ 5:48). Hii pia inahusisha hukmu za kisharia zilizo katikiwa za kukataza kuwafanya Makafiri kuwa ni vipenzi kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

 (لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّهُ نَفْسَهُ وَإِلَى اللَّهِ الْمَصِيرُ)

Waumini wasiwafanye Makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anayefanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhaharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.” [TMQ 3:28]

Hii pia imekusanya hukmu za kisharia zinazohusiana na Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ambayo inahitaji tafsiri isio potoshwa kama ilivyokuja katika aya nyingi za Quran. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihad kwa mali yenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.”  [TMQ 9:41]

Hii pia inahusisha kukiuka mipaka (hudud) ya Mwenyezi Mungu kama kupigwa bakora wazinifu, kukatwa mikono wezi na mengineyo.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Hii ndio mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakaoikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhalim.” [TMQ 2:229]. Hivyo hivyo, haipaswi kwa mwanachuoni kuficha chochote katika mambo yalio na dalili za wazi (bayyinat) na uongofu ambao Mwenyezi Mungu ameufafanua katika Kitabu Chake.

Kwa bahati mbaya, kuna wanachuoni wanaoficha au kugeuza sheria za kuhukumu kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiteremsha na kukataza kuhukumu kwa sheria za kikafiri kwa kuwaridhisha watawala Waislamu wanaotawala kwa kisichokuwa Uislamu, wakati Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya kuwa ni dalili ya wazi (bayyinah) katika Kitabu Chake!

Kuna wanachuoni wanaotoa fatwa kwa maslaha ya watawala Waislamu katika kushirikiana na makafiri kwa kuwauwa Waislamu, wakati Mwenyezi Mungu amebainisha wazi katika Kitabu Chake! Kuna wanachuoni wanaofasiri aya za Jihad kwa kuafikiana na sheria za kisekula na kuzificha ili kuwaridhisha makafiri! Ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, ni juu yao kujirekebisha kwa kukata utiifu wao kwa watawala Waislamu wanaotawala kwa sheria za kikafiri na kutangaza kwa watu kile ambacho Mwenyezi Mungu amekifanya kuwa ni dalili ya wazi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

  إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ

“Ila wale waliotubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni mwenye kupokea toba na mwenye kurehemu.”   [TMQ 2:160]

Mwisho, ni kuwa, ujumbe huu wa Uislamu na wito hauwezi kulinganiwa kwa watu bila uongozi wa wanachuoni wema waliorithi elimu safi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume (saw). Historia imeshuhudia wanachuoni wengi walioihifadhi Dini ya Uislamu kifikra na kimada kutokana na maadui wa Uislamu. Wakati Uislamu unashambuliwa na fikra na dhana ngeni, wanachuoni wema walikuwa mstari wa mbele kuzipinga fikra hizi ovu. Vile vile, wakati ardhi za Waislamu zikishambuliwa na maadui wa Uislamu, wanachuoni wema walikuwa mstari wa mbele kuwashawishi watu kwa ajili ya Jihad kuwatoa makafiri katika ardhi za Waislamu. Hivyo, kwa kukosekana Khilafah, ni wajibu kwa wanachuoni waliopo kuihifadhi Dini kwa kuushawishi Ummah kusimamisha Khilafah kufukuza fikra ngeni na makafiri wakoloni kutoka katika ardhi za Waislamu. Enyi wanachuoni wanyenyekevu wa Uislamu, warithi wa Mitume! Unganeni na wito wa kilimwengu wa kusimamisha Khilafah kwa kuwa mstari wa mbele, ambayo kupitia kwake Uislamu utatekelezwa na kubebwa ulimwenguni.

وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ

“Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.” [TMQ 51:55]

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammed Bin Farooq

 Marejeo:

[1] Tafsir Qurtubi (Al-Baqara: aya 159)

[2] Taysir fi Usuli Tafsir, ya Sheikh Ata bin Khalil Abu al-Rashta (Al-Baqara: aya 159)

[3] Tafsir Qurtubi (Al-Baqara: aya 185)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu