Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Juu ya Tukio la Ukumbusho wa Ukombozi wa Konstantinopoli mnamo 857 H – 1453 M
- Imepeperushwa katika Hotuba
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Zipo siku zinazong’aa katika historia za mataifa ambazo ni chanzo cha ufahari wa mataifa hayo. Kwa hiyo itakuwaje ikiwa siku hizo zitakuwa ni katika kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)? Bila shaka zitakuwa ni nyota zenye kung’aa angani, bali ni jua linalotoa nuru kwa ulimwengu na kulinyanyua taifa hilo juu angani… Na katika siku hizo tukufu, zipo siku za ukumbusho wa ukombozi wa Konstantinopoli…