Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Amerika

Kongamano la Mtandaoni la Khilafah 2020: "Kutoka Vurugu la Kiulimwengu Hadi Utulivu wa Kiulimwengu"

Chini ya muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, Hizb ut Tahrir ilizindua kampeni pana ya kiulimwengu ya kumbukumbu ya 99 ya Kuanguka Khilafah. Tarehe 28 Rajab Al-Muharram 1441 H – sawia na 2020 M. Hizb ut Tahrir / Amerika ilifanya Kongamano la Mtandaoni la Khilafah 2020: "Kutoka Vurugu la Kiulimwengu Hadi Utulivu wa Kiulimwengu". Lilipeperushwa moja kwa moja kutokana na janga la virusi vya Korona.

Jumapili, 12 Shabaan 1441 H - 5 Aprili 2020 M

Kongamano la Mtandaoni la Khilafah 2020 la Hizb ut Tahrir / Amerika:

"Kutoka Vurugu la Kiulimwengu Hadi Utulivu wa Kiulimwengu"

Katikati ya janga, mgogoro mwengine wa kiuchumi umewaathiri mabilioni ya watu kote duniani. Ufutaji kazi mkubwa na mamilioni ya watu walio chini ya vizuizi vya kukaa nyumbani yameathiri maisha kiasi ambacho ulimwengu haujapata kuona. Haya yanajiri huku kukiwa na mandhari ya kuongezeka kwa ukosefu wa usawa katika utajiri na ongezeko la vurugu za kisiasa na migogoro ya kibinadamu ambayo yameutawala ulimwengu kwa miongo mingi. Umma wa Kiislamu uko chini ya unyanyasaji mkubwa bila ya kujali uchache wala wingi wao. Kuanzia Mashariki hadi Magharibi, serikali za Kisekula za Kirasilimali zimeshindwa kujenga mujtamaa zenye utulivu na zimefeli kudhamini mahitaji msingi ya mabilioni ya watu. Ulimwengu una hamu ya suluhisho badali. Suluhisho la kiulimwengu ni kutabikisha Uislamu chini ya Khilafah. Ungana nasi tujadili masuluhisho thabiti ya matatizo ya leo na upate mtazamo wa kipekee wa mustakbali.  

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru tovuti za Hizb ut Tahrir / Amerika:

Ukurasa Rasmi Hizb ut Tahrir/ Amerika
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir/ Amerika
Akaunti ya Twitter Account ya Hizb ut Tahrir/ Amerika

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir/America

Kongamano Kamili la Mtandaoni

#ReturnTheKhilafah   #YenidenHilafet   #TurudisheniKhilafah         أقيموا_الخلافة#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 20 Mei 2020 06:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu