Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 10/01/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 28 Jumada Al-Akhir 1445 H sawia na 10 Januari 2024 M

Palestina na Kashmir Haja ya Kurusha Makombora katika Kuzinusuru, Sio kwa Ajili ya Majaribio yake Pekee

Pakistan ilifanya majaribio yaliyofanikiwa ya urushaji kombora la Fateh II mnamo Disemba 27, 2023 kulingana na mrengo wa vyombo vya habari vya Jeshi. Hapo awali, Pakistan pia ilikuwa imefanya majaribio kombora la Ababil mnamo Oktoba 2023. Kwa kweli, madhumuni ya majaribio haya hayakuwa kulionya umbile la Mayahudi na Dola ya Kibaniani kutangaza vita. Jeshi la Kiislamu la Khilafah halirudi nyuma wala kujisalimisha kwa ukandamizaji. Linasonga mbele, liwe na vifaa vizito au vyepesi. Mwenyezi Munguﷻ  amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ]

  “Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo.” [Surah Al-Anfal, 8:15]. Enyi wana wa Salahudin! Simamisheni tena Khilafah kwa Njia ya Utume ili muweze kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu ﷻ.

22 Jumada Al-Akhir 1445 H - 03 Disemba 2023 M

Manufaa ya Ukuaji chini ya Urasilimali Yamefungika kwa Kipote cha Wachache wenye Nguvu

Mkurugenzi wa nchi wa Benki ya Dunia, Najy Benhassine, alisema mnamo Disemba 28 kwamba muundo wa sasa wa uchumi wa Pakistan haufanyi kazi. Aliongeza kuwa matunda ya maendeleo yamefungwa kwa sehemu ndogo. Pakistan sio mwathirika wa pekee wa utofauti mkubwa wa utajiri. Popote ubepari ulipo, uwe chini ya nchi ya demokrasia au la, iwe dola ya Magharibi au la, kuna mrundiko mkubwa wa utajiri mikononi mwa wachache. Ubepari hauhakikishi usambazaji adilifu wa utajiri. Kulingana na takwimu za Mikopo za Suisse 2020, asilimia 45.8 ya utajiri wa ulimwengu wote unashikiliwa na 1.1% ya idadi ya watu ulimwenguni. Mfumo wa uchumi wa Kiislamu unahakikisha usambazaji wa utajiri. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ]

“ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Surah Al-Hashr 59:7]

23 Jumada Al-Akhir 1445 H - 04 Disemba 2023 M

Watoto wa Gaza watatoa Hoja dhidi ya Watawala wa Waislamu Mbele ya Mwenyezi Mungu

Gavana wa Sindh ametoa Agizo la Sekta  ya Uigizaji ya Watoto wa Sindh 2023. Kwa kuwa hakuna kikao cha Bunge la Kitaifa, lilitolewa kwa msingi wa "dharura". Sasa waigizaji watoto hawataweza kuigiza katika michezo ya kuigiza wakati wa masaa ya shule. Utoaji wa sheria hii unaonyesha vipaumbele vya watawala hawa. Sheria hii ya "dharura" imetolewa, huku watoto wa Gaza wakipoteza vita kwa ajili ya maisha yao. Kwanza walianikwa wazi kwa mabomu ya umbile la Mayahudi. Sasa wanaanikwa wazi kwa njaa na magonjwa yaliyolazimishwa na vita. Watawala wa Pakistan hawaizingatii hii kuwa ni dharura. Vipaumbele vyao viko wazi havizingatii juu ya Ummah wa Kiislamu au Msikiti wa Al-Aqsa. Mwamko wa Ummah wa Kiislamu hauwezekani bila kuondolewa kwa watawala hawa waliopandikizwa juu ya Ummah leo.

24 Jumada Al-Akhir 1445 H - 05 Disemba 2023 M

Ewe Jenerali! Kilimo sio Badali ya Jihad

Wakati akihutubia Mkutano wa Kitaifa wa Kilimo mnamo 29 Disemba 2023, Mkuu wa Jeshi la Pakistan alisisitiza kujitolea kwa jeshi kuunga mkono kilimo cha nchi hiyo. Uamuzi wa Kamanda wa Jeshi la Sita kwa ukubwa ulimwenguni kuzipa mgongo Kashmir na Palestina, na kuzingatia kilimo, ndio sababu ya kudhalilishwa kwa Waislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, إِذَا تَبَايَعْتُمْ بِالْعِينَةِ وَأَخَذْتُمْ أَذْنَابَ الْبَقَرِ وَرَضِيتُمْ بِالزَّرْعِ وَتَرَكْتُمُ الْجِهَادَ سَلَّطَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ ذُلاًّ لاَ يَنْزِعُهُ حَتَّى تَرْجِعُوا إِلَى دِينِكُمْ  Mnaposhiriki katika riba, mkashikilia mikia ya ng'ombe, mkaridhika na kilimo na kuachana na Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atakuleteeni udhalilifu na hatauondoa hadi murudi kwenye dini yenu.”  [Abu Dawud]. Enyi Jeshi la Pakistan! Ipeni Hizb ut tahrir Nusrah yenu ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume ili muweze kurudi kwenye Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ﷻ, na kumaliza udhalilifu unaosababishwa na uongozi wenu wa sasa wa kijeshi.

25 Jumada Al-Akhir 1445 H - 06 Disemba 2023 M

Enyi Majeshi ya Waislamu! 70% ya Gaza Imeangamizwa Lini Mutasonga?

Kwa mujibu wa makala moja yaliyochapishwa mnamo tarehe 30 Disemba 2023 katika Jarida la Wall Street, karibu nyumba 300,000 kati ya 439,000 za Gaza zimeharibiwa. Umbile la Kiyahudi limeangusha mabomu 29,000. Zaidi ya asilimia 90 ya wenyeji 2,300,000 sasa wamehamishwa. 21,500 wameuawa. 70% ya mashahidi ni watoto, wanawake na wazee. 55,000 wamejeruhiwa. Hii ndio inaripotiwa, ilhali uhalisia ni mbaya zaidi. Je! Vikosi vya Waislamu vitasonga wakati Gaza yote itapokuwa makaburi? Umoja wa Ummah mtukufu wa Kiislamu umebadilishwa na mgawanyiko katika dola 57 za kitaifa. Enyi majeshi ya Waislamu! Hamasikeni kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume ili muweze kuinusuru Palestina. Vyenginevyo, Makafiri watazifanya nchi zengine zilizosalia za Waislamu kuwa makaburi, moja baada ya moja.

26 Jumada Al-Akhir 1445 H - 07 Januari 2024 M

Ni Faradhi Kutumia Nguvu za Kijeshi Dhidi ya Maadui Wote wa Mwenyezi Mungu ﷻ

Mnamo  2 Januari 2024, Jeshi la Anga la Pakistan liliongeza shehena mpya ya ndege za kivita aina ya  J-10C kwa hazina ya ndege zake. Jukumu la majeshi ya Waislamu ya Pakistan sio tu kuilinda ardhi ya Pakistan pekee. Ni kupigana dhidi ya maadui wote wa Mwenyezi Mungu ﷻ, kwa maandalizi. Mwenyezi Munguﷻ  amesema,

[وَاَعِدُّوۡا لَهُمۡ مَّا اسۡتَطَعۡتُمۡ مِّنۡ قُوَّةٍ وَّمِنۡ رِّبَاطِ الۡخَـيۡلِ تُرۡهِبُوۡنَ بِهٖ عَدُوَّ اللّٰهِ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.” [Surah Al-Anfal: 60]. Kwa kukosekana Khilafah, watawala wa Waislamu wanayazuia majeshi kutokana na kupigana na maadui zetu wote. Khilafah kwa Njia ya Utume itayahamasisha majeshi ya Ummah dhidi ya maadui wa Mwenyezi Munguﷻ  huko Kashmir na Palestina.

27 Jumada Al-Akhir 1445 H - 09 Januari 2024 M

Kutuma Misaada Badala ya Majeshi na Vifaru Hutia Chumvi Vidonda vya Waislamu wa Gaza

Ndege maalum ya jeshi la Pakistan ilifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa El-Arish nchini Misri mnamo 2 Januari 2024. Ilibeba tani 20 za misaada ya kibinadamu na ya matibabu kwa Gaza. Ikiwa umbile la Mayahudi litaruhusu mahitaji kuingia Gaza, watu watabaki kati ya kifo na njaa na magonjwa, na kifo cha kupigwa mabomu na risasi za wadenguzi. Watawala wa Waislamu ni washirika wa dola za Magharibi na mradi wao, umbile la Mayahudi. Ummah unahitaji mlezi na mlinzi. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ndiyo itakayotuma vikosi angani, na vifaru kwenye meli kupitia bahari na kisha ardhini. Enyi wana wa Salahudin! Wapindueni wasaliti. Toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah. Jeraha  liko wazi na linatoka damu. Lifungeni kwa moto wenu na chuma.

28 Jumada Al-Akhir 1445 H - 10 Januari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu